Panzi Mbishi
JF-Expert Member
- Mar 8, 2021
- 2,055
- 2,673
Wadau kama kichwa kinavyojieleza hapo juu, tunapoelekea mwisho wa mwaka nimejipanga mwaka ujao nijaribu bahati yangu nje ya nchi, nahitaji kujua namna gani nitapata full funded scholarship hasa katika nchi nazoweza kusoma huku nikijishughulisha na vibarua hata kubeba box. Kuna jamaa yangu alisema kuna namna ambayo watumishi wanapata visa kirahisi sasa hapatikani tena kwenye simu zake na kwa kuwa nia yangu iko palepale nikaonelea nije kuomba msaada hapa.
Sababu za kuomba:
-Nina diploma, nahitaji kumalizia degree yangu lakini kutokana na majukumu ya kifamilia nadhani sitamaliza degree yangu. Degree ni ndoto yangu siko tayari kuachana nayo ndio maana nataka kusoma bure, kujilipia nimeshindwa.
-Nataka kupiga ndege wawili kwa jiwe moja, kusoma huku nikifanya kazi, mimi naamini elfu kumi ya nje si sawa na elfu kumi ya hapa. So, siendi kizembe.
-Kupata exposure zaidi na kupanua ufahamu juu ya masuala kadha wa kadha.
Kutokana na sababu hizo hapo juu wakuu wangu niko chini ya miguu yenu, najua JF hapakaukiwi taarifa na maarifa. Naombeni msaada wenu wakuu.
Nawasilisha