Kuhusu China, Correct Me If Am Wrong

Kuhusu China, Correct Me If Am Wrong

Character X

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
331
Reaction score
382
katika Post hii, natafuta kuwashirikisha wana JF maswala kadhaa yanayo jionyesha sasa katika siasa za Tanzania kimataifa., lakini kwanza nataka kuanza na ziara hii ya Raisi Xi wa China na Mikataba ya makubaliano kadhaa iliyo fanyika hapa nchini hivi majuzi.

Kwanza nadhani swala hili (la mikataba) linahitaji kuangaliwa kwa makini sana kabla ya ku comment kwanamna yoyote ile.
Ukiiangalia mikataba hii kwa jicho la kibiashara zaidi kuliko jicho la kimsaada, utagundua SIO mikataba mibaya hatakidogo kibiashara. Ila kama uki itazama kwa jicho la kimsaada zaidi basi unaweza kusema mikataba hiyo SIO msaada wowote kwa Tanzania., nasema haya kwa sababu zifuatazo:

Msaada mtuhutoa pasipokufaidika yeye hasa, ila akitaraji kusaidia zaidi yule anayepokea msaada ule.,lakini katika biashara hutegemei kupewa kitu in your favor bila chochote in return kwa partner in business. kwahiyo hapa tuta angalia kwa undani (angalau ninaoweza kuwanao kwa sasa) nini tunachopata kwenye mikataba ile na kipi tunacho kitoa ili kupata tutakacho pata., yaani nini tutafaidi na kipi wata faidi waChina.
kufikia hapa tutakubaliana Wote kwamba mikataba ile ni ya kibiashara zaidi (exchange of goods and/or Services) kuliko ya kimsaada.

kwa madhumuni ya mjadala huu tuta tumia sehemu ya makubaliano baadhi ambayo tunayafahamu tayari juu ya mkataba wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo kama case study.

Itazame mikataba ile (hasa sehemu zilizo wahi kuwa posted hapa JF) utagundua china ina weka picha ya kimataifa kwamba makubaliano haya ni ya kimsaada kwamfano sasa msaada wa ujenzi wa bandari hiyo ya bagamoyo lakini sasa maswali ya kujiuliza hapo ni wame toa msaada huu ILI IWEJE?

Ndugu zangu nime tazama swala hili kwa umakini (angalau kwa kiasi nilicho weza kwa sasa) yapo mambo ambayo ninataka kuya onyesha hapa, na haya yatakua katika makundi mawili.

Moja, (kibiashara)

Makubaliano hapa si kwamba tu yanataka bandari hiyo ijengwe na kandarasi za ki china ila pia ikikamilika iendeshwe na wachina kwa miaka 50 ili kurudisha mkopo wao., maana yake nini?

Hapa swala la interest kwa Uchina ni lipi? ni vyema kujua kwamba china contractors ni wengi na wana uwezo mkubwa lakini wana soko limited lenye competition kubwa sana sasa interest ya China hapa ni kuwatafutia soko contractors wao nje ya nchi, hili litakua na impact sio tu kibiashara lakini pia hata kiutamaduni, ushirika wa kimataifa na ukienda mbali zaidi hata ki intelijensia.

lakini pia, China ni kati ya nchi zenye population kubwa sana kuliko resources walizo nazo, in essence wanatatizo kubwa la unemployment huenda kubwa kuliko tulilo nalo hapa kwetu., Hapa wame tafuta ajira kwa ma engineers wakichina wanao ongezeka kila kukicha huku nafasi za kazi zimeendelea kujaa huko nyumbani sasa wamefungua mlango wa ajira kadhaa nchi ya mbali. Hii ni nchi inayojua kuwekeza si tu ndani ya nchi lakini hata nje nakufungua milago zaidi ya ajira ya watu wake., hiyo ni moja.

lakini pili, makubaliano ni kwamba waendeshe bandari hizi kwa miaka 50 baada ya kukamilika., hii inakuambia nini?

kwamba moja, wanaendelea kuongeza ajira za wachina hata nje ya china kwa miaka 50 zaidi lakini pia, wanajua kuhusu ubabaishaji wa nchi za ki africa katika uendeshaji wa mashirika ya umma na ulipaji madeni., sasa wanataka waendeshe wenyewe ili pamoja na kwamba wachina wengi zaidi wataendelea kupata ajira lakini pia pesa yao waliyo invest pale irudi.

utagundua haiishii tu kenye kutaka kuiendesha wenyewe, lakini pia wame weka clause inayo bind Tanzania katika kuhakikisha bandari watakayo ijenga itakua kubwa zaidi ya nyingine yoyote., maanake isije ikaundwa bandari kubwa zaidi ya hiyo ndani ya kipindi hicho kiasi chatengeneza competition ambayo huenda ika sababisha hii watakayo jenga kwenda out of business nakusababisha watu wao wasi pate ajira, au mkopo wao usilipike.

lakini hapa hasa swala sio kuangalia tu wao watapata nini katika biashara hii, lakini tujiulize je? tusipo kubali mikataba hii tunauwezo wa kujenga bandari hiyo kwa resources tulizo nazo wenyewe? nadhani hapa jibu ni HAPANA! nakama hatuna je tuendelee tu kukaa bila kua na maendeleo eti kwasababu hatutaki wachina waiendeshe kwa miaka 50 na kutumia mda huo kulipa mkopo huo? na kwamba hatutaki watumie contractors wao? je tukipewa sisi wapo ma contractors wazawa watakao weza kusimamisha project ya ukubwa huo??

Nadhani mikataba hii uki itazama kwa jicho la kibiashara ni mikataba nafuu sana., inayo lenga tukuwapa wachina wachache ajira nje ya nchi na kulipa mkopo wao lakini upande mwingine kuiachia tanzania bandari kubwa itakayo zalisha kwaajili ya watanzania miaka mingi baada ya miaka hiyo hamsini ya kurejesha mkopo huo.,
na kwa hakika tunge taka tuiendeshe wenyewe bandari ile na kulipa mkopo ule wenyewe huenda tungelipa mkopo huo kwa miaka mia mbili.,

kama pesa za kujenga daraja tu zinalipwa kwa miaka 40, sembuse bandari na installation ya vifaa vyote?
ndugu zangu kibiashara kilicho fanyika ni win-win situation KABISA!!

Kimahusiano
China ni rafiki wa Tanzania kwa miaka yote toka baada ya uhuru. Urafiki wa China na Tanzania haukuanza leo wala jana. yako mambo mengi ambayo yame kwisha fanyika na marafiki hawa wawili,. viwanda kama URAFIKI ni mfano mmoja tu. Huu ni wakati ambapo Tanzania inatunukiwa na rafiki zao hao kwakuendeleza urafiki huo.

lakini kubwa zaidi ni hili, kwa kawaida mataifa haya makubwa huwa na allies katika kila bara dunia nzima., hii inatengeneza nguvu situ ya sauti ya taifa katika forums mbali mbali lakini pia hutengeneza nguvu katika Representative Forums mbalimbali za kimataifa. allies hawa huonyeshwa ceremonially kwa matukio ya wazi kama haya., hotuba ya kwanza ya raisi, au/na safari ya kwanza baada tu ya kuchukua kiti., huonyesha symbolically huyu mtu au hili taifa lina fungamana na watu gani., hutafuta kuwaweka wazi marafiki zake na kwanamna flani hutafuta kuonyesha kuwatambua adui zake.

safari ya kwanza ya Raisi wa China anaamua kuifanya yakuja Tanzania.,

kwakifupi, raisi bush aliwahi kuja hapa pia na katika safari yake, mengi yalijiri lakini yote yalionyesha ushawishi flani., ziko fedha nyingi zilizo tolewa kwa tanzania kipindi kile.,na watu wengi wali hoji kulikoni? tena ukitafiti utagundua Tanzania kipindi flani hapo nyuma ndiyo ilikua nchi inayo pokea fedha nyingi kama msaada kutoka Uingereza kuliko nchi nyingine yoyote Duniani.

kama hiyo haitoshi raisi wa kwanza kualikwa na Obama mara tu baada ya kuapishwa kwake awamu ile ya kwanza alikua Raisi Kikwete (unaweza kusema labda kwakua alikua mwenyekiti wa AU kwa kipindi kile lakini je, alipo maliza mda wake aliye pokea kijiti naye alienda?), ukiyatazama haya kwaundani naukakumbuka juu ya siasa ya Tanzania ya kipindi cha mwalimu yakuto fungamana na upande wowote, utagundua kulikuwapo mvutano au ushawishi hapa., upande mmoja wa marekani inayo fahamu China kama uchumi unaokuwa kwa kasi sana sana kiasi cha kua tishio kwake hata ki tecnology na ki jeshi, na upande mwingine China ambayo imekua rafiki wa Tanzania kwa muda mrefu toka kipindi cha Uhuru, na siasa zinazo karibia kufanana.

lakini katika kutilia mkazo hili, itafute hotuba ya raisi kikwete bungeni Dodoma juzi katika Ziara hii ya Raisi Xi wa China ilikua hotuba kwanza ya kiingereza., kwanini? angeweza kuongea kiswahili, mbona hata Raisi Xi alikua akiongea kichina na kutafsiriwa., yaani maanake Raisi Xi hata kiingereza hajui., sasa unaongea kiingereza ili iwaje wakati unaeongea nae hajui hata icho kiingereza., utasema labda watafsiri wakichina hawajui kiswahili lakini sikweli ukitembelea ualozi wa china utashangaa sana kuna wachina wanaongea kiswahili kama wa pemba., maanake nini? aliongea kiingereza kwasababu kabisa., kwamakusudi kabisa., ile haikua hutoba tu kama nyingine ile ilikua NI HOTUBA YA KUSIKILIZWA NA DUNIA NZIMA, nihotuba yakutangaza msimamo.

itafute hotuba ile utagundua pia ni hotuba yenye utafauti mkubwa na hotuba nyingine nyingi za Raisi kikwete., hotuba ile ilikua kakamavu yenye kutafuta kuonyesha msimamo wa nchi., ikiwa na phrases "kama mtu asi tuhukumu juu ya urafiki au uadui wetu na mtu mwingine yoyote" (not an exact quote)., ikiwa namaana tumeamua kuwa marafiki wa China nahuo ndiyo msimamo wetu.

Kwamtu mwenyekutafiti siasa za dunia utagundua Si tu hotuba ya raisi kikwete lakini pia safari ya Raisi Xi zilikua staged Strategically Kabisa!
hapakua na wakati bora zaidi wa kutangaza wazi wazi ally wako wa sera zako za kimataifa kama Safari ya Kwanza ya Raisi Mpya wa Nchi kubwa kama China kufanyika kwenye nchi hiyo tena mapema kabisa baada tu yakua raisi. Hili limefanywa tukio la kihistoria., siotu ziara yakuaja kusign mikataba., No! hiyo mikataba ni ziada yake., lakini hasa nikutangazia dunia tumeamua nini, chakungoja sasa ni response ya wale wengine.

Baada ya kusema hayo mengi nije kwenye swala la China na maendeleo ya Tanzania., nina weza kusema China hapa haitoi msaada Sana kivile kama wengi wanavyo weza kufikiri., ila inafanya biashara, biashara ambayo inamanufaa kwao lakini pasipo kukosa shukrani lazima niseme itakua na manufaa kwetu pia.

Comrades,
ni hayo
 
All in all Unaweza kunisaidia kuwa nini Kipaumbele cha Tanzania ya leo?
Je Ni Kilimo?
Elimu?
Afya?
Usafirishaji?
Umeme?
Maji?
MakaZi?
Au ni kipi?

Na pia kama Tumekopa sisi wenyewe kwa moyo mkunjufu, Je ni sahihi kutekeleza hii miradi na kuacha kutekeleza yale ya muhimu kwa Taifa ili na Watanzania kwa Ujumla?

Tafakari chukua hatua.
 
kwa jinsi ccm wametimba nchi kila kitu kimekuwa kipaumbele.

Kupata elimu unahitaji hela na afya bora.kupata hela nako kunahitaji hela na elimu.mchezo wa kuku na yai.
 
lakini hapa hasa swala sio kuangalia tu wao watapata nini katika biashara hii, lakini tujiulize je? tusipo kubali mikataba hii tunauwezo wa kujenga bandari hiyo kwa resources tulizo nazo wenyewe? nadhani hapa jibu ni HAPANA! nakama hatuna je tuendelee tu kukaa bila kua na maendeleo eti kwasababu hatutaki wachina waiendeshe kwa miaka 50 na kutumia mda huo kulipa mkopo huo? na kwamba hatutaki watumie contractors wao? je tukipewa sisi wapo ma contractors wazawa watakao weza kusimamisha project ya ukubwa huo??
Mkuu hapo kwenye blue. hilo swali zuri sana umelijibu lakini ni rahisi sana kutoa jibu ulilotoa(kwenye red) kama usipofikiria kwa undani kidogo.
Hilo swali linatakiwa ujiulize kiundani kidogo, swali liwe hivi je tuna uwezo wa kujenga bandari hiyo kwa resources zetu kabla au ndani ya MIAKA 50?
Jibu ni NDIO.

Unapoingia mkataba wenye conditions za kuwabana kwa miaka 50 mfululizo (nusu karne for God's sake) just because serikali yako unayoiongoza sasa imekuwa corrupted na ubabaishaji wa kila aina una'assume hata Serikali zijazo(kipindi hiki cha miaka50) nazo zitakuwa hivyo hivyo kiasi kwamba hazitoweza kujenga bandari ya dizaini hiyo, That is WRONG, absolutelly wrong.

Nina mashaka na interests za huu 'msaada'.
Kiasi kwamba mpaka nakaribia kuamini zile tetesi kuwa kuna mtoto wa kigogo alishikwa na madawa ya kulevya kule China, ili kumtoa ikalazimu kugawa pwani ya Bagamoyo ijengwe hiyo bandari.
 
Mkubwa,

Kutokana na maandishi yako na hali halisi ya kibiashara ni kwamba China imeidharau sana serikali ya sasa na kuchukua hatua za kujiami kimkataba. Kitendo cha wao kudai ya kuwa bandari lazima hiwe chini ya uongozi wao ni kwamba hawatuamini watanzania kama tuna huwezo wa kuweza kufanya biashara kimaendeleo sisi wenyewe bila ya usimamizi hiyo ni dharau ya hali ya juu.

wakati sote tunajua chanzo ni madaraka ya kujuana na vyombo vya sheria visivyo ng'ata chini ya CCM ndio chanzo cha ubadhirifu. Hivyo huo mkataba unawakidhi viongozi wa sasa wa CCM ambao wamepachikana bila ya kupima madhara ya muda mrefu na kutofanya zoezi la kuteuwa watu kupitia ujuzi wao.

Wewe wapi umeona mtu anakwenda kukopesha halafu anawaambia, sisi ndio wasimamizi huo si ndio ukoloni mambo leo, halafu demand zao kama kweli ndio hizo ulizozielezea wanahukika gani kama biada ya miaka hamsini uchumi wetu utakuwa lelemama hivihivi au na nchi jirani zinazotumia hiyo bandari hazita kuza uchumi wao kiasi kwamba tuhitaji a bigger port?

Hapa naanza kuona nuksi ya mchina kwa mkopo wake, tunahitaji bandari kubwa na sipingani na area ambayo imechaguliwa kwa sasa kutokana na miundombinu iliyopo inaipa upendeleo bagamoyo. Hila kwanini waseme wajenzi lazima wawe wa china, wakati hawatofanya kazi ya kanisa. Hiwapo suala ni hilo kwanini tusichague sisi tutakaeona ni nafuu na atakaetupa vitu vyenye quality ya dunia ya leo kwa matakwa yetu. Jee hao wakandarasi wachina wanashindana kwa tender au hata hao serikali yao tayari imeshatuchagulia hivyo nikujirudishia mkopo wao mapema wao wenyewe.

Halafu mkataba wa miaka hamsini bila ya kujenga port nyingine na potential iliyopo inside Tanzania is pathetic in business terms and political terms (maana siasa za sasa tunaongozwa na watu wa ajabu ambao wapo kutafuta sifa at any cost who knows what will happend tommorow pengine hata huyo raisi wa miaka 30 ya mkataba bado ajazaliwa) fuatilia kasheshe ya 'Suez Canal' ambayo ilijengwa under colonial influence na kasheshe lake baadae, utajua naongelea nini; a little of home work sio kutafuniana kila kitu.
 
Kadaganye mkeo na watoto wako! What th hell r these contracts about? Had u known exactly what led to these contracts n y we Tanzanians were not involved before signing them n why were the hosters acted like kings families u would have deleted your thread and pray for this sold nation of Tanzania...! Do you have/ have you seen and read clearly th contracts? Think big!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Oh man .. excuse his / her ignorance mkuu... Amekurupuka .. plus ameweka siasa mbele
 
Miaka 50 hapa kilichoangaliwa ni kwao bagamoyo.kwamba ndani ya iyo miaka bagamoyo itakuwa sana kiuchumi.thats all.mengine ni maumivu tu
 
Kadaganye mkeo na watoto wako! What th hell r these contracts about? Had u known exactly what led to these contracts n y we Tanzanians were not involved before signing them n why were the hosters acted like kings families u would have deleted your thread and pray for this sold nation of Tanzania...! Do you have/ have you seen and read clearly th contracts? Think big!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Nadhani mtazamo wako ni kwamba mikataba hiyo haina manufaa kwa Taifa la Tanzania, na kwamba unadhani labda watanzania tunge shirikishwa katika maamuzi haya. Well, ni mtazamo ninao uheshimu hata kama ningeweza kuwa na mawazo tofauti na wewe, lakini la msingi hapa nadhani nikujenga hoja kueleza kile hasa unacho kiona kwenye ushirika huu, naamini ingekua jambo la maana zaidi na ingetosha kusema kama unge eleza tu ule uliomtazamo wako huru kama walivyo fanya watu wengine walio changia humu, the language used here was absolutely uncalled for. nevertheless kuhusu kushirikishwa kwa watanzania sijui ungependekeza kushirikishwa kwa namna gani? should have passed a referendum may be? na gharama za kuendesha hizo kura zingekuaje labda? ingechukua muda gani? halafu ikibidi kila mkataba unaoingiwa na serikali ya tanzania watanzania wote washirikishwe nchi hii ita sogea kwa speed gani?

nadhani fikiria kuhusu hili kwa mtazamo huu utagundua at the end of the day it all comes down to who do you choose to be your leaders., kwa sababu viongozi wana jukumu na dhamana ya kutazama wapi tuna taka kwenda na kutupeleka huko., sasa swala la kwamba umemchagua kiongozi asiye faa sasa anafanya maamuzi yasiyo na faida kwa Taifa ni swala jingine lakini swala na mamlaka yakufanya maamuzi nadhani tuliwapa.

kwaio kwa sasa, we can question the lucrativeness of the decisions they make for us but we can not question the authority with which they make decisions on our behalf.

comrade, pamoja na kwamba tuna mitazamo tafuati nadhani i can not over emphasize the importance of a sue of a good professional language in such forums.

with that.
Asante
 
Kinachojitokeza wazi katika mikataba ambayo imesainiwa, kama tukiutumia huo mkataba wa bandari kama kigezo, ni kuwa China inajua kwa uhakika kabisa inataka nini kutoka kwetu na imeshajipanga na kujiwekea mkakati unaoihakikishia kuwa itakipata hicho inachokitaka.
Tatizo langu sijaona kiuwazi katika deals hizi Tanzania inataka nini na imejipanga vipi kukipata hicho inachokitaka.
Kinachoonekana ni kuwa kwa sababu bwana mkubwa amekubali kutufanyia haya basi hewala, chochote kitakachopatikana ndicho hicho hico kitatufaa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu hapo kwenye blue. hilo swali zuri sana umelijibu lakini ni rahisi sana kutoa jibu ulilotoa(kwenye red) kama usipofikiria kwa undani kidogo.
Hilo swali linatakiwa ujiulize kiundani kidogo, swali liwe hivi je tuna uwezo wa kujenga bandari hiyo kwa resources zetu kabla au ndani ya MIAKA 50?
Jibu ni NDIO.

Unapoingia mkataba wenye conditions za kuwabana kwa miaka 50 mfululizo (nusu karne for God's sake) just because serikali yako unayoiongoza sasa imekuwa corrupted na ubabaishaji wa kila aina una'assume hata Serikali zijazo(kipindi hiki cha miaka50) nazo zitakuwa hivyo hivyo kiasi kwamba hazitoweza kujenga bandari ya dizaini hiyo, That is WRONG, absolutelly wrong.

Nina mashaka na interests za huu 'msaada'.
Kiasi kwamba mpaka nakaribia kuamini zile tetesi kuwa kuna mtoto wa kigogo alishikwa na madawa ya kulevya kule China, ili kumtoa ikalazimu kugawa pwani ya Bagamoyo ijengwe hiyo bandari.

Nime uona mtazamo wako na nadhani ni mtazamo wa wengi ambao unaweza kuwa na ukweli kwa kiasi flani. nina uheshimu. However, nadhani inahitaji experience ya kufanya kazi na multinational cooperations au kufanya negotiations at a national level kuelewa hasa haya ninayo ya eleza hapa., nivigumu sana kufananisha moja kwa moja transaction ya taifa na transaction ya kampuni au shirika dogo., ninafahamu wengi huangalia miaka hamsini kwa upande mmoja, kwamba itakua chini yao kwa miaka 50! na hivyo ni rahisi kwetu kupanic na kucomment negatively zaidi kuliko positively lakini swala situ kama tungeweza kuijenga bandari hiyo kwa kutumia resources zetu baada ya miaka hamsini swala ni je? kusubiri hadi baada ya miaka hamsini ndo tuweze kujenga hiyo bandari ni faida kwetu au hasara kwetu? hata kama tukifika hiyo miaka hamsini tukijikusanya ili tuijenge kwa resouses zetu., economist talk about "the time value of a project" project inayo simama leo nakuanza ku trigger economy positively ni far more profitable kuliko itakayo kuja kuanza baada ya miaka hamsini hatakama hiyo itaja anza kwa nguvu zetu wenyewe.

halafu kama hiyo haitoshi hapa lazima tuwe realistic., katika taifa kama Tanzania hakuna maswala ambayo yanachukuliwa kua items of national interest kwamba hata uongozi huu ukipita atakaye fuata atayaendeleza hadi kufika mwisho wake bila kujali anatoka chama kilekile alicho toka wakwanza ama lah, wamarekani na mataifa mengine kama wa china na waingereza wana kitu kama hicho, yapo mambo yanayo cut across parties, yako mambo ambayo hata aingie nani ikulu yana fanyika kwa muendelezo wake., hichi hatuna tanzania, ndo maana yale aliyo yaacha mwl. nyerere alipo kuja mwinyi aliachana nayo akaanza yake, kaja mkapa naye na yakwake, kikwete vilevile., je ikija ingia tlp madarakani yataachwa mangapi?

kwaio utagundua sirahisi sana kusema tujikusanye kwa miaka hamsini halafu tuje kujenga bandari hii kwa resources zetu wenyewe., kumbuka hapa pia iko mikataba kama kumi na saba iliyo tiwa sign pale hapa tuna zungumzia mmoja tu., sasa project kubwa kama hizi hazifanyikagi kwa mwaka moja alafu imekamilika badala yake huchukua muda mrefu wakati mwingine hukamilika katika uongozi tafauti na ule uliyo zianzisha.

ninacho jaribu kusema nikwamba project kumi na saba kubwa namna hii zisinge weza kufanyika zote kwa kusubiri tujikusanye kwa miaka hamsini ndo zije kufanyika hichi kisinge wahi kutokea kwasababu hatujui nani atakuja after 2015 na atakua na maono gani. kufanya hivyo ingekua nikupoteza zaidi kuliko kufaidi., HAPA LAZIMA TUKUBALIANE.

mwisho niseme tu pamoja na kwamba serikali yetu ime jaa watu wasio na uwajibikaji, watu wasio na vision sana lakini lazima tukubaliane pia kwamba wapo watu ndani ya serikali wenye uwezo mku sana sana sana!! wapo watu wenye ufahamu na uwezo professional wakupambanua haya.,

wanapokosea tuna wa kosoa., wanapo fanya vyema kwanini nione haya kusema hata kama watu wote wata fikiri vinginevyo?

tusifuate mkumbo ndugu zangu chukua muda tafakari kwa kina then sema opinion yako bila kujali nani anasema nini.
asante
 
Nadhani hatuelewani hapa,
Je ni kweli tunahitaji Bandari kubwa namna hiyo?
Jibu ni Hapana, Ila ukweli wachina wanaihitaji hiyo bandari kwa ajili ya shughuli ya kusafirisha Madini na base ya meli zao za kivita.
Kwanini sasa tukope kwa ajili yao?
Kwanini utumie kodi ya Mtanzania kupeleka Umeme, Maji na Barabara kwa ajili ya muwekezaji?

Mimi nadhani kama muwekezaji anaamini mradi unalipa basi ajenge na kupeleka hizo huduma zote kwa hela zake na serekali isimamaie thaman ya Miradi na tukatane kwenye Mapato. Na sisi tiza mapato sio KODI.

Leo tungechukua hayo ma Trilion ya Bandari tungeweza kufanya mambo mengi ya Maana na kwa faida kubwa kwa nchi yetu.
 
Miaka 50 hapa kilichoangaliwa ni kwao bagamoyo.kwamba ndani ya iyo miaka bagamoyo itakuwa sana kiuchumi.thats all.mengine ni maumivu tu

Ninakubaliana na wewe kwa kiwango flani na nina dhani ume tazama hili kwa jicho laki chumi zaidi., nadhani hatuwezi kupinga ukweli kwamba kwa miaka yote hiyo hatakama itaendeshwa na hao wa china bado ukweli ni kwamba ita trigger economy ya Tanzania kwa miaka yote hiyo. na hapa na sema Economy ya Tanzania na sio Economy ya bagamoyo kwa sababu uwezo wakufanya biashara na dunia utakua ume ongezeka kwa kiwango kikubwa sana kwa kipindi chote hicho, speed ya transaction bandarini itakua kubwa zaidi, hata ajira zaidi kwa watanzania zitapatikana kwa kuwepo kwa bandari hiyo kwa muda wote huo wa miaka hiyo hamsini hatakama itakua chini ya hao wa china na mengine mengi yote.,
 
Mkuu hapo kwenye blue. hilo swali zuri sana umelijibu lakini ni rahisi sana kutoa jibu ulilotoa(kwenye red) kama usipofikiria kwa undani kidogo.
Hilo swali linatakiwa ujiulize kiundani kidogo, swali liwe hivi je tuna uwezo wa kujenga bandari hiyo kwa resources zetu kabla au ndani ya MIAKA 50?
Jibu ni NDIO.

Unapoingia mkataba wenye conditions za kuwabana kwa miaka 50 mfululizo (nusu karne for God's sake) just because serikali yako unayoiongoza sasa imekuwa corrupted na ubabaishaji wa kila aina una'assume hata Serikali zijazo(kipindi hiki cha miaka50) nazo zitakuwa hivyo hivyo kiasi kwamba hazitoweza kujenga bandari ya dizaini hiyo, That is WRONG, absolutelly wrong.

Nina mashaka na interests za huu 'msaada'.
Kiasi kwamba mpaka nakaribia kuamini zile tetesi kuwa kuna mtoto wa kigogo alishikwa na madawa ya kulevya kule China, ili kumtoa ikalazimu kugawa pwani ya Bagamoyo ijengwe hiyo bandari.

Ndibalema hakuna mahala popote imeongelewa Mkataba wa ujenzi wa bandari na EPZ Bgamoyo utakuwa ni wa miaka 50. Hizo ni speculations za watu wanaotaka kujenga hoja za kuupinga mradi. Kilichosainiwa ni framework agreement, wala haina details zozote za gharama au muda wa kurudisha uwekezaji uliofanyika. Ile framework agreement ndio imetengeneza njia ya kuanza mazungumzo ya kina kuhusu namna ya kutekeleza mradi wenyewe.

Lakini for the sake of argument hata ingekuwa kweli kuna mkataba wa miaka 50, sio lazima iwe ni jambo baya,kitakacho determine miaka ni uwekezaji uliofanyika ni wa kiasi gani (thamani gani) na return of investment itachukua muda gani. Hizo ndio factors zinazo determine muda wa mtu kuendesha mradi chni ya utaratibu wa Build Operate Transfer (BOT).

Ipo mifano ya mradi kama wa Eurostar- reli ya kutoka Uingereza kwenda Ufaransa ambayo ujenzi wake uligharimu Pauni za Kiingereza Bilioni 5 (takriba dola za kimarekani Bilioni 10). Makisio ya awali ya mwekezaji kuendesha reli ile na kurejesha faida ilikuwa ni miaka 50. Lakini baada ya kuanza kazi, reli ile ilikumbwa na misukosuko kadhaa ikiwemo na abiria kutoitumia sababu ya uwepo wa other cheaper options kama low cost airlines (Easyjet, Ryan Air), ongezeko la gharama za uendeshaji kutokana na bei ya mafua kupata, mtikisiko wa uchumi barani ulaya n.k mwisho wake wale wawekezaji walirudi mezani na Serikali za Uingereza na Ufaransa wakakubaliana kwamba miaka 50 haitoshi kurejesha kiasi cha fedha kilichowekezwa...ikaamuliwa waongezewe miaka 40 mingine which means jumla miaka 90. (Ukitaka kusoma kwa undani kuhusu mradi huu nenda kwenye link hii:http://www.adbi.org/working-paper/2011/05/13/4531.financial.instruments.ppp.infrastructural.dev.eu/illustrative.examples.of.ppp.in.the.eu/

Nimelazimika kukusimulia ya Uingereza ili tupate picha kwamba suala la muda wa mwekezaji kuendesha mradi unakuwa determned na factors nyingi........ni vrma kuzielewa badala ya kukurupuka kushambulia hoja bila kuwa na facts za kutosha kuhusu mradi wenyewe.

Jambo la muhimu la kuzingatia ni kwamba mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo la viwanda utakuwa na manufaa mengi from day one utakapoanza. Wananchi wapatao 3000 watapata ajira za muda za moja kwa moja katika ujenzi wa bandari na EPZ, wananchi wengine wapatao 2000 na zaidi watapata ajira zisizo za moja kwa moja kama vile Mama Ntilie watakaouza chakula, wenye nyumba zao watakaowapangisha wajenzi, wauza vinywaji, watoa huduma za usafiri-daladala, taxi, maroli ya kusafirisha mizigo n.k

Faida nyinginezo za mradi huo ni kwamba mara utakapokamilika, thamani ya properties zilizopo eneo la mradi na maeneo ya jirani kama vile Bunju,Boko, Mbezi, Tegeta n.k yatapanda thamani na kuwafaidisha wamiliki endapo watahitaji kukodisha property zao au kuzitumia kuwekea rehani kupata mikopo benki n.k

Faida nyingine ni za moja kwa moja kwa Serikali......ukubwa wa bandari maana yake volume ya mizigo itakayopitia hapo itaongezeka ambapo Serikali itaongeza mapato kupitia IMPORT DUTY, customs Duty......bandari itakapokamilika itaajiri wafanyakazi wasiopungua 1000, eneo la viwanda litakapomilika-litawezesha viwanda vingi kujengwa (by the way Mwekezaji ndio atavutia viwanda kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuweka viwanda vyao kwenye eneo hilo na tayari ameshapata wawekezaji walio tayari kuwekeza provided kuna efficient port) na viwanda hivyo vitatoa ajira kwa wananchi wasiopungua 50,000 na zaidi.

Kwa faida ya wasiojua kwanini viwanda vingi vitakuja kuwekeza katika eneo hilo:
1) bidhaa zitakazozalishwa hapa Tanzania katika eneo hilo la viwanda zitaweza kufaidi misamaha ya kodi inayotolewa kwa Nchi masikini huko Marekani (Chini ya AGOA); Ulaya (Everything but Arms EBA), Japan (TICAD consession), na China yenyewe iliyotoa msamaha wa kodi kwa asilimia 95 ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania

2) Cheap labour- ukweli ni kwamba toka China uchumi wake umekua, factors of production zilizokuwa zinawa favour zimetoweka....Afrika ndio ina fursa ya kuziba pengo hilo la China

3) Kwakuwa viwanda vingi lengo lao ni kuzalisha bidhaa za kupeleka nje ya nchi- uwepo wa bandari kubwa yenye mtandao mkubwa duniani inakuwa ni kivutio kikubwa kwao.....mwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo anao mtandao wa bandari kadhaaa ulimwenguni....wao ndio wanamiliki bandari tano kati ya bandari kubwa kumi duniani....ikiwemo bandari ya Hongkong, Schenzen n.k

Ukiachilia ajira etc.....serikali inaweza kufaidika pia kwa kupata mrahaba (royalty) katika kipindi chote ambacho mwekezaji ataendesha bandari ili kurejesha uwekezaji aliofanya.

La muhimu hapa ni wataalam wetu watakao negotiate mkataba huo kuwa makini na kuhakikisha serikali inapata WIN-WIN deal na hao wawekezaji. Kwenye nchi nyingine kama Singapore, India, Ulaya, Marekani...zipo specialised firms zinazotoa huduma ya kuguide serikali zinazo negotiate na wawekezaji complex transactions za aina hii. Ipo haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa ku procure services za firm za aina hiyo.
 
Nadhani hatuelewani hapa,
Je ni kweli tunahitaji Bandari kubwa namna hiyo?
Jibu ni Hapana, Ila ukweli wachina wanaihitaji hiyo bandari kwa ajili ya shughuli ya kusafirisha Madini na base ya meli zao za kivita.
Kwanini sasa tukope kwa ajili yao?
Kwanini utumie kodi ya Mtanzania kupeleka Umeme, Maji na Barabara kwa ajili ya muwekezaji?

Mimi nadhani kama muwekezaji anaamini mradi unalipa basi ajenge na kupeleka hizo huduma zote kwa hela zake na serekali isimamaie thaman ya Miradi na tukatane kwenye Mapato. Na sisi tiza mapato sio KODI.

Leo tungechukua hayo ma Trilion ya Bandari tungeweza kufanya mambo mengi ya Maana na kwa faida kubwa kwa nchi yetu.

Oh Nadhani nime kupata sasa., na inapokuja kwenye swala la priorities sijui kama Sisi wa tanzania ni wazuri sana., sijui. ila ukiniuliza mimi hata kama kwenye scale of preference Bandari kubwa yakisasa inaweza isiwe namba moja in the line lazima niseme kwamba itakuwepo in the line.,

huku ndo kusema kwamba japo yako mengi ambayo tuna yahitaji sana huenda kuliko bandari lakini bandari pia tuna ihitaji., nina sema hivi kwa sababu ziko tafiti nyingi zilizo fanyika hapa nchini na kuonyesha namna ambavyo tanzania inapoteza fedha nyingi kutokana na kutokua na uwezo wa kuhudumia nchi zote zisizo kua na bahari ambazo inazibidi kwenda hadi mombasa ilihali ingekua raisi zaidi kwazo kufanya biashara na bandari ya dar ila udog wa bandari hii na volume ya trade inayo zungumziwa hapa ndiyo kimekua kikwazo miaka yote., mimi nadhani bandari bado inahitajika hata kama haihitajiki kama vile ambavyo tuna hitaji shule bora, huduma za afya na maji safi lakini ukweli ni kwamba bado bandari ni kitu kinacho weza kutufaa.,

lakini pia tujikumbushe tu kwamba bandari ni jambo moja kati ya mengi sana yaliyo wekewa sahihi siku ile sasa tusije tuka sahau huenda hayo tunayo ya waza kua ya muhimu zaidi kuliko bandari katika uhitaji wetu huenda ya meguswa tayari na mikataba hiyo mingine kwa namna moja au nyingine.

lastly naomba tu niseme hapa pia., A Nation is a very big Organisation! uongozi wake sio mrahisi kivile
 
Mkuu hapo kwenye blue. hilo swali zuri sana umelijibu lakini ni rahisi sana kutoa jibu ulilotoa(kwenye red) kama usipofikiria kwa undani kidogo.
Hilo swali linatakiwa ujiulize kiundani kidogo, swali liwe hivi je tuna uwezo wa kujenga bandari hiyo kwa resources zetu kabla au ndani ya MIAKA 50?
Jibu ni NDIO.

Unapoingia mkataba wenye conditions za kuwabana kwa miaka 50 mfululizo (nusu karne for God's sake) just because serikali yako unayoiongoza sasa imekuwa corrupted na ubabaishaji wa kila aina una'assume hata Serikali zijazo(kipindi hiki cha miaka50) nazo zitakuwa hivyo hivyo kiasi kwamba hazitoweza kujenga bandari ya dizaini hiyo, That is WRONG, absolutelly wrong.

Nina mashaka na interests za huu 'msaada'.
Kiasi kwamba mpaka nakaribia kuamini zile tetesi kuwa kuna mtoto wa kigogo alishikwa na madawa ya kulevya kule China, ili kumtoa ikalazimu kugawa pwani ya Bagamoyo ijengwe hiyo bandari.

Kaka asante na uko sahihi kabisa, nakushukuru kwa observation zako....T
 
Character X .. Kwanza nikupongeze kwa uchambuzi ambao Nahisi haufungamani na upande wowote.. I stand to be corrected.

  • Hatuwezi kujadili mikataba hii Kwani imefanywa Kuwa Siri na yote tunayojadili ni maneno ya watu ambayo Hafuna uhakika nayo... Hatuhitaji referendum ile mikataba kupostiwa hata kwenye web site ya serikali ilitosha kutoa Mwanya wa Wadau Wenye uelewa kuhihoji na kutoa advice kwa Faida ya Taifa hili.
  • Kuanza kujadili mikataba iliokwisha sainiwa ni kupoteza wakati na ni Matusi kwa watanzania ... Kumbuka tumesha I via mikataba Mingi mibovu huko nyuma na Imani ya wananchi kwa uongozi kuhusu kuingia mikataba imeshuka hivyo ni vyemma ushirikishwaji Sa wanainchi katika masuala haya ni lazima.. Kwa nini hata bunge lisitumike kabla ya kusaini ? Kuna haraka gani ya kusaini?
  • Nchi hii inahitaji vipaumbele na misingi ya kiuchumi Ambayo vyama vyote vya siasa vinatakiwa kuvienzi na kuviendeleza....
Nitarudi baadaye na Mengi zaidi...
 
Ndibalema hakuna mahala popote imeongelewa Mkataba wa ujenzi wa bandari na EPZ Bgamoyo utakuwa ni wa miaka 50. Hizo ni speculations za watu wanaotaka kujenga hoja za kuupinga mradi. Kilichosainiwa ni framework agreement, wala haina details zozote za gharama au muda wa kurudisha uwekezaji uliofanyika. Ile framework agreement ndio imetengeneza njia ya kuanza mazungumzo ya kina kuhusu namna ya kutekeleza mradi wenyewe.

Lakini for the sake of argument hata ingekuwa kweli kuna mkataba wa miaka 50, sio lazima iwe ni jambo baya,kitakacho determine miaka ni uwekezaji uliofanyika ni wa kiasi gani (thamani gani) na return of investment itachukua muda gani. Hizo ndio factors zinazo determine muda wa mtu kuendesha mradi chni ya utaratibu wa Build Operate Transfer (BOT).

Ipo mifano ya mradi kama wa Eurostar- reli ya kutoka Uingereza kwenda Ufaransa ambayo ujenzi wake uligharimu Pauni za Kiingereza Bilioni 5 (takriba dola za kimarekani Bilioni 10). Makisio ya awali ya mwekezaji kuendesha reli ile na kurejesha faida ilikuwa ni miaka 50. Lakini baada ya kuanza kazi, reli ile ilikumbwa na misukosuko kadhaa ikiwemo na abiria kutoitumia sababu ya uwepo wa other cheaper options kama low cost airlines (Easyjet, Ryan Air), ongezeko la gharama za uendeshaji kutokana na bei ya mafua kupata, mtikisiko wa uchumi barani ulaya n.k mwisho wake wale wawekezaji walirudi mezani na Serikali za Uingereza na Ufaransa wakakubaliana kwamba miaka 50 haitoshi kurejesha kiasi cha fedha kilichowekezwa...ikaamuliwa waongezewe miaka 40 mingine which means jumla miaka 90. (Ukitaka kusoma kwa undani kuhusu mradi huu nenda kwenye link hii:http://www.adbi.org/working-paper/2011/05/13/4531.financial.instruments.ppp.infrastructural.dev.eu/illustrative.examples.of.ppp.in.the.eu/

Nimelazimika kukusimulia ya Uingereza ili tupate picha kwamba suala la muda wa mwekezaji kuendesha mradi unakuwa determned na factors nyingi........ni vrma kuzielewa badala ya kukurupuka kushambulia hoja bila kuwa na facts za kutosha kuhusu mradi wenyewe.

Jambo la muhimu la kuzingatia ni kwamba mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo la viwanda utakuwa na manufaa mengi from day one utakapoanza. Wananchi wapatao 3000 watapata ajira za muda za moja kwa moja katika ujenzi wa bandari na EPZ, wananchi wengine wapatao 2000 na zaidi watapata ajira zisizo za moja kwa moja kama vile Mama Ntilie watakaouza chakula, wenye nyumba zao watakaowapangisha wajenzi, wauza vinywaji, watoa huduma za usafiri-daladala, taxi, maroli ya kusafirisha mizigo n.k

Faida nyinginezo za mradi huo ni kwamba mara utakapokamilika, thamani ya properties zilizopo eneo la mradi na maeneo ya jirani kama vile Bunju,Boko, Mbezi, Tegeta n.k yatapanda thamani na kuwafaidisha wamiliki endapo watahitaji kukodisha property zao au kuzitumia kuwekea rehani kupata mikopo benki n.k

Faida nyingine ni za moja kwa moja kwa Serikali......ukubwa wa bandari maana yake volume ya mizigo itakayopitia hapo itaongezeka ambapo Serikali itaongeza mapato kupitia IMPORT DUTY, customs Duty......bandari itakapokamilika itaajiri wafanyakazi wasiopungua 1000, eneo la viwanda litakapomilika-litawezesha viwanda vingi kujengwa (by the way Mwekezaji ndio atavutia viwanda kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuweka viwanda vyao kwenye eneo hilo na tayari ameshapata wawekezaji walio tayari kuwekeza provided kuna efficient port) na viwanda hivyo vitatoa ajira kwa wananchi wasiopungua 50,000 na zaidi.

Kwa faida ya wasiojua kwanini viwanda vingi vitakuja kuwekeza katika eneo hilo:
1) bidhaa zitakazozalishwa hapa Tanzania katika eneo hilo la viwanda zitaweza kufaidi misamaha ya kodi inayotolewa kwa Nchi masikini huko Marekani (Chini ya AGOA); Ulaya (Everything but Arms EBA), Japan (TICAD consession), na China yenyewe iliyotoa msamaha wa kodi kwa asilimia 95 ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania

2) Cheap labour- ukweli ni kwamba toka China uchumi wake umekua, factors of production zilizokuwa zinawa favour zimetoweka....Afrika ndio ina fursa ya kuziba pengo hilo la China

3) Kwakuwa viwanda vingi lengo lao ni kuzalisha bidhaa za kupeleka nje ya nchi- uwepo wa bandari kubwa yenye mtandao mkubwa duniani inakuwa ni kivutio kikubwa kwao.....mwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo anao mtandao wa bandari kadhaaa ulimwenguni....wao ndio wanamiliki bandari tano kati ya bandari kubwa kumi duniani....ikiwemo bandari ya Hongkong, Schenzen n.k

Ukiachilia ajira etc.....serikali inaweza kufaidika pia kwa kupata mrahaba (royalty) katika kipindi chote ambacho mwekezaji ataendesha bandari ili kurejesha uwekezaji aliofanya.

La muhimu hapa ni wataalam wetu watakao negotiate mkataba huo kuwa makini na kuhakikisha serikali inapata WIN-WIN deal na hao wawekezaji. Kwenye nchi nyingine kama Singapore, India, Ulaya, Marekani...zipo specialised firms zinazotoa huduma ya kuguide serikali zinazo negotiate na wawekezaji complex transactions za aina hii. Ipo haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa ku procure services za firm za aina hiyo.

Asante kwa elimu uliyotoa, paliponigusa sana ni hapo mwisho. Ni ukweli usiopingika kuwa serikali ianze kuingia gharama ya kuyatafuta hayo makampuni yatakayotusaidia kwenye negotiations za mikataba ya jinsi hii (ikiwezekana mikataba yote). Manake wataalam wetu, mmmmh...sina uhakika kama utaalam ni mdogo au kuna factors nyingine unknown zinazowaangusha...
 
Oh Nadhani nime kupata sasa., na inapokuja kwenye swala la priorities sijui kama Sisi wa tanzania ni wazuri sana., sijui. ila ukiniuliza mimi hata kama kwenye scale of preference Bandari kubwa yakisasa inaweza isiwe namba moja in the line lazima niseme kwamba itakuwepo in the line.,

huku ndo kusema kwamba japo yako mengi ambayo tuna yahitaji sana huenda kuliko bandari lakini bandari pia tuna ihitaji., nina sema hivi kwa sababu ziko tafiti nyingi zilizo fanyika hapa nchini na kuonyesha namna ambavyo tanzania inapoteza fedha nyingi kutokana na kutokua na uwezo wa kuhudumia nchi zote zisizo kua na bahari ambazo inazibidi kwenda hadi mombasa ilihali ingekua raisi zaidi kwazo kufanya biashara na bandari ya dar ila udog wa bandari hii na volume ya trade inayo zungumziwa hapa ndiyo kimekua kikwazo miaka yote., mimi nadhani bandari bado inahitajika hata kama haihitajiki kama vile ambavyo tuna hitaji shule bora, huduma za afya na maji safi lakini ukweli ni kwamba bado bandari ni kitu kinacho weza kutufaa.,

lakini pia tujikumbushe tu kwamba bandari ni jambo moja kati ya mengi sana yaliyo wekewa sahihi siku ile sasa tusije tuka sahau huenda hayo tunayo ya waza kua ya muhimu zaidi kuliko bandari katika uhitaji wetu huenda ya meguswa tayari na mikataba hiyo mingine kwa namna moja au nyingine.

lastly naomba tu niseme hapa pia., A Nation is a very big Organisation! uongozi wake sio mrahisi kivile

Nakubaliana na wewe, basi wafanye kwa hela yao na sio sisi tukope kwa ajili yao, nadhani unaielewa nachomaanisha, waje wajenge kuazia bandari, Reli, EPZ sisi tukusanye KODI yetu na hiwe hivyo kwenye KODI hakuna haja ya Negotiontion ila kwenye Mapato sawa tunaweza kupigiana hesabu ya hata miaka 200, Ila KODI walipe zote bila msamaha.
 
Kataka swala hili kuna mambo mengi ya kujiuliza ila me nitajikita katika life cycle ya hiyo bandari. wachina wahitaji miaka 50 waendeshe bandaria ambayo life cycle yake hatujui ni miaka mingapi. kama life cycle yake ni miaka 100 hapo sawa ila ninaiman kwamba hapo baada ya miaka 50 mashine na kila kitu hakitakua katika hali nzuri coz ya depliciation. kwahiyo baada ya miaka hamsini itakuwa ubora na ufanisi wake ni mdogo mno.
 
Back
Top Bottom