Kuhusu China, Correct Me If Am Wrong

Kuhusu China, Correct Me If Am Wrong

Bandari hii ni muhimu kwa mstakali wa nchi yetu.Cha msingi mikataba isimamiwe vizuri ili vizazi vijavyo visije kutulaumu.Bandari zingine ndogo ndogo nazo ziendelezwe kuweza kusaidiaana na bandari kubwa katika kuleta ufanisi.
Nasisitiza watanzania wasomeshwe kwenye fani zinazohusiana na uwekezaji mkubwa tusije kuishia kuwa vibarua na kutoa mwanya kwa wageni kukamata ajira nyingi.
Kwa kuanzia Serikali ianze kutoa mikopo ya elimu kwa baadhi ya vyuo vya nje kwa vijana wa Kitanzania ili wajiandae kukamata ajira na kuwa wakufunzi kwa vyuo vya hapa nchini ili elimu hiyo ipatikane hapa nchini kwa urahisi na vijana wengi wapate taaluma muhimu kwa ajira zitakazo kuwepo.
 
Nime uona mtazamo wako na nadhani ni mtazamo wa wengi ambao unaweza kuwa na ukweli kwa kiasi flani. nina uheshimu. However, nadhani inahitaji experience ya kufanya kazi na multinational cooperations au kufanya negotiations at a national level kuelewa hasa haya ninayo ya eleza hapa., nivigumu sana kufananisha moja kwa moja transaction ya taifa na transaction ya kampuni au shirika dogo., ninafahamu wengi huangalia miaka hamsini kwa upande mmoja, kwamba itakua chini yao kwa miaka 50! na hivyo ni rahisi kwetu kupanic na kucomment negatively zaidi kuliko positively lakini swala situ kama tungeweza kuijenga bandari hiyo kwa kutumia resources zetu baada ya miaka hamsini swala ni je? kusubiri hadi baada ya miaka hamsini ndo tuweze kujenga hiyo bandari ni faida kwetu au hasara kwetu? hata kama tukifika hiyo miaka hamsini tukijikusanya ili tuijenge kwa resouses zetu., economist talk about "the time value of a project" project inayo simama leo nakuanza ku trigger economy positively ni far more profitable kuliko itakayo kuja kuanza baada ya miaka hamsini hatakama hiyo itaja anza kwa nguvu zetu wenyewe



Mkuu hapa ndipo ninapopingana na wewe.. Tunayo bandari ambazo zipo ambazo kuziboresha ilihitaji mtaji kidogo [ labda 40% ] ya investment ya kwenda kujenga mpya pamoja na miundo mbinu ili iweze kutumika. Hapo kama priority ilikuwa ni bandari ya kisasa kuboresha zilizopo ingekuwa ni busara zaidi.
Kwanza tungetumia mtaji kidogo iwe ni kwa resources za ndani ama kukopa kwa riba nafuu na hata pay back period ingekuwa ya muda mfupi. Suala la kuanzisha bandari mpya na kuzibana zingine ili zisilete mapato kwa taifa ... ni utaahila uliopitiliza....

Pili je tumejaribu kuuza idea hiyo kwa wawekezaki wengine kuwashindanisha na wachina... no body knows kwa sababu nci inaendeshwa kwa siri kubwa pasipo sababu...


halafu kama hiyo haitoshi hapa lazima tuwe realistic., katika taifa kama Tanzania hakuna maswala ambayo yanachukuliwa kua items of national interest kwamba hata uongozi huu ukipita atakaye fuata atayaendeleza hadi kufika mwisho wake bila kujali anatoka chama kilekile alicho toka wakwanza ama lah, wamarekani na mataifa mengine kama wa china na waingereza wana kitu kama hicho, yapo mambo yanayo cut across parties, yako mambo ambayo hata aingie nani ikulu yana fanyika kwa muendelezo wake., hichi hatuna tanzania, ndo maana yale aliyo yaacha mwl. nyerere alipo kuja mwinyi aliachana nayo akaanza yake, kaja mkapa naye na yakwake, kikwete vilevile., je ikija ingia tlp madarakani yataachwa mangapi?

HAPA nakubaliana nawe 100%.. KUNA haja ya kuwa na National Interest and priorities ambazo Rais yeyote ajae ataziendeleza

kwaio utagundua sirahisi sana kusema tujikusanye kwa miaka hamsini halafu tuje kujenga bandari hii kwa resources zetu wenyewe., kumbuka hapa pia iko mikataba kama kumi na saba iliyo tiwa sign pale hapa tuna zungumzia mmoja tu., sasa project kubwa kama hizi hazifanyikagi kwa mwaka moja alafu imekamilika badala yake huchukua muda mrefu wakati mwingine hukamilika katika uongozi tafauti na ule uliyo zianzisha.

NDIO maana nimesema hapo juu kweli tulikuwa tunahitaji Bandari mpya? au ilikuwa rahisi kuboresha zilizopo? kuna ubembuzi ykinifu wowote umefanya na kubaini pros and cons za kujenga bandari mpya vs kuimarisha zilizopo? kumbuka tunabebeshwa mkopo mkubwa bure pasipo na sababu wakati tungeweza kuuepuka.
 
Simply namuunga JK mkono kwa hili la kushirikiana na wachina! Tulipotoka hapo nyuma, hasa Mkapa aliamua kuegemea upande wa magharibi! uchafu mwingi unaomtesa JK uliasisiwa na Mkapa... Kenya wamepiga hatua ya haraka baada ya Kibaki kuwatamkia "no more west! we are turning east now!" ndo maana wanahaha kuhakikisha Raila anaingia madarakani...Wazungu ni wanyonyaji in the name of Demokracy...Bora wachina ambao siku zote wako kwenye win win ...
 
Jamani Mbona tunadanganywa na misaada ya US/UK na UE yenye kudharirisha utu wetu na masharti ya mashoga! leo hii tunajiuliza kwanini CHINA waisimamie mradi huu kwa kuleta menejiment yao ebu tujiulize menejiment za MIGODINI ni wazungu wa TZ ndo wanaoongoza au? Hivi tujiulize mikataba ya madini tena yanayochimbwa na kuisha ni ya miaka mingap 99 au 100? Bandari its a big deal huwezi compare na mikataba ya madini hata chembe! Tusidanganywe na US/Uk/UE the new world order is coming soon
 
Jamani, hivi baada ya hiyo miaka hamsini bandari itakuwa bado iko imara kwa maana ya miundo mbinu yake (majengo na magati)?
Naamini kwa umuhimu kwa nchi saba zinazoitegemea na ukubwa wa hiyo bandari, miaka 20 inatosha kabisa kwa Wachina kurejesha mtaji na faida ili tupate angalau miaka 20 ya sisi kupata faida ya moja kwa moja kabla span life ya majengo na magati haijaisha.
 
1) Naona wachina wanapigwa madongo juu ya hii mikataba, kwani ni Tanzania au China ndio wameinitiate ujenzi wa hiyo bandari?
2) Wachina wanajua udhaifu wetu katika kusimamia miradi, wametupa TAZARA- imetushinda, Kiwira-imetushinda, Urafiki-imetushinda, Mang'ula machine tools-imetushinda, magari ya nyumbu-imetushinda, Uwanja wa taifa-SIJUI...sasa bado unataka mtu akujengee port kwa mabilioni then alale mbele, ili umlete TASCAN na mikataba yake. Kwanza akiwapa tu after 2yrs utasikia tu matatizo harafu hiyo hela yake mturudisha vipi?....also know that, there is no free lunch nowadays.....kama unamashaka na mtu jenga mwenyewe.
 
Ndibalema hakuna mahala popote imeongelewa Mkataba wa ujenzi wa bandari na EPZ Bgamoyo utakuwa ni wa miaka 50. Hizo ni speculations za watu wanaotaka kujenga hoja za kuupinga mradi. Kilichosainiwa ni framework agreement, wala haina details zozote za gharama au muda wa kurudisha uwekezaji uliofanyika. Ile framework agreement ndio imetengeneza njia ya kuanza mazungumzo ya kina kuhusu namna ya kutekeleza mradi wenyewe.

Lakini for the sake of argument hata ingekuwa kweli kuna mkataba wa miaka 50, sio lazima iwe ni jambo baya,kitakacho determine miaka ni uwekezaji uliofanyika ni wa kiasi gani (thamani gani) na return of investment itachukua muda gani. Hizo ndio factors zinazo determine muda wa mtu kuendesha mradi chni ya utaratibu wa Build Operate Transfer (BOT).

Ipo mifano ya mradi kama wa Eurostar- reli ya kutoka Uingereza kwenda Ufaransa ambayo ujenzi wake uligharimu Pauni za Kiingereza Bilioni 5 (takriba dola za kimarekani Bilioni 10). Makisio ya awali ya mwekezaji kuendesha reli ile na kurejesha faida ilikuwa ni miaka 50. Lakini baada ya kuanza kazi, reli ile ilikumbwa na misukosuko kadhaa ikiwemo na abiria kutoitumia sababu ya uwepo wa other cheaper options kama low cost airlines (Easyjet, Ryan Air), ongezeko la gharama za uendeshaji kutokana na bei ya mafua kupata, mtikisiko wa uchumi barani ulaya n.k mwisho wake wale wawekezaji walirudi mezani na Serikali za Uingereza na Ufaransa wakakubaliana kwamba miaka 50 haitoshi kurejesha kiasi cha fedha kilichowekezwa...ikaamuliwa waongezewe miaka 40 mingine which means jumla miaka 90. (Ukitaka kusoma kwa undani kuhusu mradi huu nenda kwenye link hii:Illustrative Examples of PPP in the EU

Nimelazimika kukusimulia ya Uingereza ili tupate picha kwamba suala la muda wa mwekezaji kuendesha mradi unakuwa determned na factors nyingi........ni vrma kuzielewa badala ya kukurupuka kushambulia hoja bila kuwa na facts za kutosha kuhusu mradi wenyewe.

Jambo la muhimu la kuzingatia ni kwamba mradi wa Bandari ya Bagamoyo na Eneo la viwanda utakuwa na manufaa mengi from day one utakapoanza. Wananchi wapatao 3000 watapata ajira za muda za moja kwa moja katika ujenzi wa bandari na EPZ, wananchi wengine wapatao 2000 na zaidi watapata ajira zisizo za moja kwa moja kama vile Mama Ntilie watakaouza chakula, wenye nyumba zao watakaowapangisha wajenzi, wauza vinywaji, watoa huduma za usafiri-daladala, taxi, maroli ya kusafirisha mizigo n.k

Faida nyinginezo za mradi huo ni kwamba mara utakapokamilika, thamani ya properties zilizopo eneo la mradi na maeneo ya jirani kama vile Bunju,Boko, Mbezi, Tegeta n.k yatapanda thamani na kuwafaidisha wamiliki endapo watahitaji kukodisha property zao au kuzitumia kuwekea rehani kupata mikopo benki n.k

Faida nyingine ni za moja kwa moja kwa Serikali......ukubwa wa bandari maana yake volume ya mizigo itakayopitia hapo itaongezeka ambapo Serikali itaongeza mapato kupitia IMPORT DUTY, customs Duty......bandari itakapokamilika itaajiri wafanyakazi wasiopungua 1000, eneo la viwanda litakapomilika-litawezesha viwanda vingi kujengwa (by the way Mwekezaji ndio atavutia viwanda kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kuweka viwanda vyao kwenye eneo hilo na tayari ameshapata wawekezaji walio tayari kuwekeza provided kuna efficient port) na viwanda hivyo vitatoa ajira kwa wananchi wasiopungua 50,000 na zaidi.

Kwa faida ya wasiojua kwanini viwanda vingi vitakuja kuwekeza katika eneo hilo:
1) bidhaa zitakazozalishwa hapa Tanzania katika eneo hilo la viwanda zitaweza kufaidi misamaha ya kodi inayotolewa kwa Nchi masikini huko Marekani (Chini ya AGOA); Ulaya (Everything but Arms EBA), Japan (TICAD consession), na China yenyewe iliyotoa msamaha wa kodi kwa asilimia 95 ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania

2) Cheap labour- ukweli ni kwamba toka China uchumi wake umekua, factors of production zilizokuwa zinawa favour zimetoweka....Afrika ndio ina fursa ya kuziba pengo hilo la China

3) Kwakuwa viwanda vingi lengo lao ni kuzalisha bidhaa za kupeleka nje ya nchi- uwepo wa bandari kubwa yenye mtandao mkubwa duniani inakuwa ni kivutio kikubwa kwao.....mwekezaji wa Bandari ya Bagamoyo anao mtandao wa bandari kadhaaa ulimwenguni....wao ndio wanamiliki bandari tano kati ya bandari kubwa kumi duniani....ikiwemo bandari ya Hongkong, Schenzen n.k

Ukiachilia ajira etc.....serikali inaweza kufaidika pia kwa kupata mrahaba (royalty) katika kipindi chote ambacho mwekezaji ataendesha bandari ili kurejesha uwekezaji aliofanya.

La muhimu hapa ni wataalam wetu watakao negotiate mkataba huo kuwa makini na kuhakikisha serikali inapata WIN-WIN deal na hao wawekezaji. Kwenye nchi nyingine kama Singapore, India, Ulaya, Marekani...zipo specialised firms zinazotoa huduma ya kuguide serikali zinazo negotiate na wawekezaji complex transactions za aina hii. Ipo haja ya Serikali kuangalia uwezekano wa ku procure services za firm za aina hiyo.

mimi si mjuzi wa mambo ya mikataba ila hapo penye red kidogo pamenitia moyo, ila maelezo yaliyofuatia yananikumbusha machungu ya mkataba wa Buzwagi, baada ya kusaini walikuja na mlolongo wa faida zitakazopatikana na loyalty etc lakini mpaka leo ni maumivu tu.
 
Haya na mikataba mingine iliyosainiwa ni ipi? maana wengine tunasikia tu mikaba mingi imesainiwa...
nchi hii!!!!
 
Serikali ingeiweka mikataba hii wazi ingekua vyema sana kuisoma.
 
Ingawa sijafika mwisho wa uzi wako hapa kwa mkataba huu wa miaka 50 sijui kuendesha bandari itakuwa kama migodi wanachimba masaa 24 ila mwisho wa siku wanasema hakuna faida hii bandar kwa upande wa china kuiendesha mwisho wa siku wataichukua yote kabisa mana lazima deni wanalo dai litakuwa lipo juu tushindwe kulipa waombe bandar tuwaachie
 
Back
Top Bottom