OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,035
- 114,472
Inashangaza sana kuona mapambano ya vihiyo aliyoanzisha Rais Magufuli punde alipoingia madarakani yamekosa maana eti kwa sababu ya kumkingia kifua mtu mmoja.
Leo hii unaposikia kwamba mamlaka zinawajibisha watumishi kwenye vyeti feki inaonekana ni kitu cha ajabu kabisa. Lile tamko kali la Rais Magufuli kuhusu kujisalimisha kwa viongozi wenye vyeti feki limeonekana sio kitu tena
Leo hii Rais hana tena sauti ya kuzungumzia vyeti. Ikumbukwe wakati Rais amefanya uteuzi wa wakurugenzi mteule wake mmoja alishutumiwa kutokuwa na elimu inayokidhi. Rais akafanya kitendo cha kujasiri kuwataka wateule kuja na vyeti.......
Makonda nakushauri,unamshushia Rais wetu heshima. Kejeli dhidi yake zinazoendelea mitandaoni ni pamoja na kukulinda wewe.
Tafadhali onyesha cheti