Mtumbatu
JF-Expert Member
- Apr 27, 2012
- 363
- 171
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa taarifa za shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Arusha jioni ya leo, Jumamosi, Juni 15, 2013, tukio ambalo
limesababisha vifo vya watu wawili na majeruhi ya Watanzania kadhaa.
Aidha, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa na ndugu wa wafiwa wote na pia ametuma pole nyingi kwa majeruhi ambao wameumizwa na kujeruhiwa katika tukio hilo ovu na katili.
Vile vile, Rais Kikwete amewatumia salamu za pole viongozi wa CHADEMA kufuatia tukio hilo la woga mkubwa na pia kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki za kuchunguza kwa haraka, kubaini,
kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria wote waliohusika na tukio hilo, wawe watu wa ndani ya nchi ama nje ya nchi.
Katika salamu zake za rambirambi na za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Magesa Mulongo, Rais Kikwete amesema: Nimepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa CHADEMA mjini Arusha jioni ya leo, tukio ambalo limesababisha vifo na