Kuhusu Bomu Arusha - Sit Back and Relax Polisi Watafanya Kazi yao

Mtumbatu

JF-Expert Member
Apr 27, 2012
362
170
KAULIYAPOLISIKUHUSUBOMULAARUSHA.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa taarifa za shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Arusha jioni ya leo, Jumamosi, Juni 15, 2013, tukio ambalo
limesababisha vifo vya watu wawili na majeruhi ya Watanzania kadhaa.

Aidha, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa na ndugu wa wafiwa wote na pia ametuma pole nyingi kwa majeruhi ambao wameumizwa na kujeruhiwa katika tukio hilo ovu na katili.

Vile vile, Rais Kikwete amewatumia salamu za pole viongozi wa CHADEMA kufuatia tukio hilo la woga mkubwa na pia kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki za kuchunguza kwa haraka, kubaini,
kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria wote waliohusika na tukio hilo, wawe watu wa ndani ya nchi ama nje ya nchi.

Katika salamu zake za rambirambi na za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Magesa Mulongo, Rais Kikwete amesema: “Nimepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa CHADEMA mjini Arusha jioni ya leo, tukio ambalo limesababisha vifo na
 
Kwa olasit tuliambiwa alikatisha ziara kume jamaa alisha maliza. Je hili la Bomu kwenye Mkutano wa CHADEMA ziara kwanza msiba wa wananchi baadaye. Tumepokea salam na rambirambi za mkuu wa kaya. Safari njema ukishamaliza ziara na kurudi home. Tuombe wasije piga bomu wakati wa ujio wa Obama maana ni kama wiki moja na nusu tu imebaki Mkuu.


 
Polisi watafanya kazi yao siyo! Bado tunasubili majibu ya haya
- Wako wapi walimuua Padre Zanzibar
- Wako wapi waliomteka na kumpiga Ulimboka
- Wako wapi waliorusha bomu Kanisani Arusha

Tanzania ni vichekesho tu
 
Back
Top Bottom