Kuhusu Benjamin Mkapa kugombea tena urais wa JMT

Kuhusu Benjamin Mkapa kugombea tena urais wa JMT

Hapa ndo wanasiasa waelewe umuhimu wa kuwa wasafi wanapokuwa madarakani, ni kweli mkapa isingekuwa mambo ya rada na epa tungefikiria kama angeweza kurudi madarakani.
 
Yani we ni maamuma kabisa ndo kingereza gani sasa hiki Umeandika.?givi hizi shule za sikuhizi zinamatatizo gani.?

Alitakiwa aandikeje?? Hebu tuambie wewe Mtaalam wa lugha ya Kingereza ambaye hata neno la Kiswahili "hivi" limekushinda kuliandika na badala yake umeandika "givi"
 
mimi Mrisho Kanichekesha Sana Yani Anakopa Fedha Za Wahisani Ili Azunguke Kuwaaga Wahisani
 
Ndg. wa JF, nadhani kiukweli tunakumbuka sana mambo makubwa aliyoyafanya rais mstaafu Benjamin Mkapa kipindi cha uongozi wake. Miongoni mwa hayo ni kudhibiti sana mfumko wa bei pamoja na kuongezeka thamani shillingi ya Tz, ambapo US$1 ~ 1500 Tshs. tofauti na sasa ambapo $1=2200 Tshs.

Ningependa kuuliza kwa wataalamu wa sheria, baada ya kupita miaka 10 tangu amalize muda wake, JE KIKATIBA MH. MKAPA ANAWEZA RUHUSIWA KUGOMBEA TENA URAIS?

Kama anaruhusiwa, akachukue fomu arudi kutusaidia watanzania. Binafsi namkubali sana mzee.


Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana!! Wakati wa utawala wa Mkapa tulikuwa tunalalamika kuwa hali ya uchumi ni mbaya, pesa hakuna na maisha ni magumu mpaka tukatengeneza misamiati kama UKATA, UKAPA nk yote ikimaanisha wkt ule hali ilikuwa mbaya!!!!!!

Amekuja Kikwete naye tunalaumu na kusema hali ya uchumi ni mbaya bora arudi Mkapa madarakani !!! Inamaana tulitaka thamani ya dola moja tangu enzi za Mkapa mpaka leo ibaki ile ile sh 1500??? Kwani enzi za Nyerere na Mwinyi thamani ya dola ilikuwa ni sh 1500 kama awamu ya mkapa??? Kama enzi za nyerere na mwinyi dola haikuzidi sh 1000 unonaje tukisema mzee Mwinyi arudi madarakani???

Pambana kufanya kazi kwa bidii ndugu!!wakati ww unalalamika na kutamani Mkapa arudi, wenzako wanazidi kuporomosha majumba ya kifahari Mithali ya makasri huku wakiagiza magari mapya toka Japan na kusababisha magari kuwa mengi mpaka barabara hazitoshi na Hatimaye foleni haziishi mijini!!!!!

Hayo ndiyo maisha mkuu!!!!!!!
 
Ndg. wa JF, nadhani kiukweli tunakumbuka sana mambo makubwa aliyoyafanya rais mstaafu Benjamin Mkapa kipindi cha uongozi wake. Miongoni mwa hayo ni kudhibiti sana mfumko wa bei pamoja na kuongezeka thamani shillingi ya Tz, ambapo US$1 ~ 1500 Tshs. tofauti na sasa ambapo $1=2200 Tshs.

Ningependa kuuliza kwa wataalamu wa sheria, baada ya kupita miaka 10 tangu amalize muda wake, JE KIKATIBA MH. MKAPA ANAWEZA RUHUSIWA KUGOMBEA TENA URAIS?

Kama anaruhusiwa, akachukue fomu arudi kutusaidia watanzania. Binafsi namkubali sana mzee.

Ya kwako ni "single track mind"!! haya yote umeyazika kwa makusudi au tuseme hukuyasikia wala kuyasoma popote!!; Mikataba mibovu/michafu, TAN RESOURCES/KIWIRA; NET GROUP (PROBLEMS) SOLUTIONS, NBC, NYUMBA ZA SERIKALI; majaji, ma-RPC; ma-RC, watumishi wa umma waandamizi wanaishi Uswazi; hata gari la zima moto na maji taka haliwezi kufika; wee weee weeeee!!
Maisha yanakwenda mbele bro hayarudi nyuma! the brightest; Patriotic, honest; focused and committed Tanzanians are not yet born; muache Chinga One apumzike; he has played his part and that is it; BWM; enjoy your retirement in peace. Thank you for your long service to this country.
 
Ndg. wa JF, nadhani kiukweli tunakumbuka sana mambo makubwa aliyoyafanya rais mstaafu Benjamin Mkapa kipindi cha uongozi wake. Miongoni mwa hayo ni kudhibiti sana mfumko wa bei pamoja na kuongezeka thamani shillingi ya Tz, ambapo US$1 ~ 1500 Tshs. tofauti na sasa ambapo $1=2200 Tshs.

Ningependa kuuliza kwa wataalamu wa sheria, baada ya kupita miaka 10 tangu amalize muda wake, JE KIKATIBA MH. MKAPA ANAWEZA RUHUSIWA KUGOMBEA TENA URAIS?

Kama anaruhusiwa, akachukue fomu arudi kutusaidia watanzania. Binafsi namkubali sana mzee.

Ikulu sio ya babako.
 
Wagombea uraisi wote 39 hakuna mwenye sifa za kugombea uraisi mpaka mamvi?
VOTE FOR UKAWA.

Usiangalie Chama..tizama Mtu..just imagine Ukawa Wako ready kumpokea Huyo Huyo mamvi akitoka CCM..huoni Kuna kitu Apo?
 
Nawashauri wenzetu wa CCM kweli wamwombe Mhe. Rais wa awamu ya tatu agombee Urais kupitia CCM. Mkapa alitufanyia mengi mpaka fedha zilikuwa zinabaki kwenye Halmashauri mwisho wa mwaka. Kwa kweli Mkapa alinyoosha nchi.
 
Kweli watanzania ni nyumbuuuuuuu........ No memory ... Wamezoea kutawaliwaaa, kudanganywaaa, kuibiwaaa
 
Kweli watanzania ni nyumbuuuuuuu........ No memory ... Wamezoea kutawaliwaaa, kudanganywaaa, kuibiwaaa
 
Back
Top Bottom