Wakuu, kwa wale wenye ufahamu kuhusu ukweli wa bei harisi wa haya magari tunayoona yanatangazwa humu jf. Mfano kuna subaru moja ya mwaka 2004 bei yake imewekwa $160 yaani kama laki tatu na nusu hivi za kitanzani sasa nini maana yake? Inamaana nikiwa na milioni tano za TZ nawezakuwa na uhakika wa kulitia mikononi mwangu? Au nikutamanishana tu?
Kwenye Ukokotozi wa Gharama halisi za Gari iko hivi
1) FOB (Bei ya Kunulia gari ikiwa kule kule Japan) = $160
2) Inspection Kwa niaba ya TBS = $ 300
3) Usafiri Japan to Tanzania = Makadirio $1,000 - $1,500 inategemea na Ujazo wa Gari kwa vipimo vya CBM (hapa usipokua makini waweza kuongezewa zaidi ili muuzaji akajazie ile $160 kijanja)
4) Bima ya Majini ili ikitokea meli imezama ulipwe ingine = $ 70 (Makadirio)
Jumla (CIF + Inspection) = $ 2,030 (estimate)
Uje TRA sasa, hapo itahitajika Kujua vifuatavyo,
1) Jina ya gari, (Toyota, Suzuki, Subaru, Daihatsu, Nissan etc), kwa kesi yako hapa ni Subaru
2) Muundo wake (Subaru Impreza, Subaru Legacy, Subaru Forester, Subaru Lexiga, etc,
3) Imetengenezwa mwaka gani
4) Ina Ukubwa gani wa Injini (CC)
5) Inatokea Nchi gani (Zaidi hua ni either Japan au UK), yaweza kua pia yatokea Kenya, Zanzibar, etc but hizi ni exceptional cases
6) Inatumia aina gani ya Mafuta, Diesel au Petrol