Kuhesabu vifaranga kabla havijaenguliwa....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhesabu vifaranga kabla havijaenguliwa....!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 3, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280

  [​IMG]

  Inawezekana hata wewe umeshawahi kuambiwa kwamba usihesabu vifaranga kabla havijatotolewa. Mara nyingi msemo huo hutumiwa katika jamii yetu ikiwa ni njia ya kumwonya mtu kwamba asiwe na matarajio makubwa na jambo ambalo halijafanyika kwa ukamilifu.

  Kila mtu, labda ukiwemo na wewe, unajua kuhusu jambo hili na unaliogopa pia. Unaliogopa kwa sababu umeambiwa kwa muda mrefu sana kiasi kwamba limekuwa ni kweli akilini mwako.
  Nikisema limekuwa ni kweli nina maana kwamba unaliamini kuwa ndivyo lilivyo. Hili ni tahadharisho kwamba mtu ukiwa na matarajio makubwa, utavunjika sana nguvu iwapo matarajio hayo hayatazaa matunda yanayotarajiwa.

  Bila shaka, waliotuambia hivyo walikuwa wanasema kwa nia njema kabisa. Lakini je lilifikishwa kichwani mwako kwa njia nzuri, ambayo isingeweza kuzalisha maana tofauti kabisa? Kila mmoja wetu wakati anakua aliwekwa kwenye tahadhari, ambapo alitakiwa bila kujua, kujiweka kwenye mazingira ambayo yatamfanya awe salama kihisia muda wote.

  Kwa mfano kutokujenga matarajio makubwa ni ili mtu asije akaumia sana kihisia pale matarajio hayo yakishindwa kufikiwa. Lakini leo ukubwani jambo hilo limekuwa ni sehemu muhimu ya tabia zetu. Hatuko tayari kuwa na matarajio makubwa kwa sababu tunaogopa kwamba kufanya hivyo ni kuingia mahali ambapo tutaumiza sana hisia zetu, pale ambapo jambo tunalotarajia likishindwa kuwa.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Tunaishi kwenye dunia ambayo saikolojia ya binaadamu imeegemezwa kwenye hofu. Hofu ya kupoteza inatusukuma na kutuendesha katika kufanya maamuzi yetu, na katika tabia zetu kwa ujumla.

  Kwa sababu ya hofu na mashaka jamii imejitengenezea njia ya kujihami na maneno kama 'usihesabu vifaranga kabla ya kuanguliwa' ni moja ya njia hizo ambazo, hutufanya wanajamii kufikiria karibu, kutokuwa na matarajio na kuogopa kutazama mbali.

  Kuamini katika msemo kama huo, kuna maana sawa kabisa na kuamini kwamba, mtu anatakiwa kufanya kidogo na kwa karibu ili asije akaumia, endapo atafikiria kufanya kikubwa na kwa mbali halafu kikakwama. Kila mmoja amefundishwa kujilinda kihisia, kukataa maumivu ya kihisia, pale mambo yatakapoenda mrama.

  Kuna baadhi ya maeneo hapa nchini ambapo mtu hatakiwi kusema kwamba atafanikiwa au kupata sana. Kwa mfano kusema atapata mavuno mazuri ni jambo lisilokubalika sana. Anapokosea na kufanya hivyo, anatakiwa kutema mate chini ili kuvunja balaa ambalo linaweza kutokea. Anachotakiwa mtu kusema ni kwamba hana uhakika, hajui, ‘ndio hivyo hivyo',
  ‘Mungu mwenyewe akipenda nitafanikiwa'.

  Kusema kwa uhakika ni jambo linalotisha, lakini pia ambalo linachukuliwa na jamii kama kuringa au kujiona, Kwa hiyo jamii inaona kufikiria mbali, kuamini kwamba inawezekana ni kuringa. Unakuta kutokana na mawazo haya, unapoteza kabisa nguvu ya kufanya na kumudu, tunapoteza uwezo wetu kama binadamu ambao tuna vipaji na uwezo mkubwa sana wa kiakili. Hapa ndipo ambapo imani nyingi tulizopewa zinapoonesha udhaifu wake kwetu. Bila shaka hujui kwamba matarajio ni moja ya rasilimali za nguvu sana ulizonazo.


   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,111
  Likes Received: 3,031
  Trophy Points: 280
  sasa bila kuhesabu.....nitawezaje kukadiria bajeti na matumizi ya baadae...?..kuku nimempa mayai 6...? kwa nini nitarajie vifaranga 2 na sio 6...think Mtambuzi....think....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,478
  Trophy Points: 280
  Leo mzee mwenzangu naona umeingia kimafumbo mafumbo.

  Nimekumbuka kale kamsemo "Usimnunulie mtoto nguo kabla hajazaliwa"
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hali ya matarajio ya jambo ambalo limetiwa shime linaweza kugeuza kile kilichoonekana kuwa hakiwezekani kikawezekana. Kama una ndoto, una lengo ambalo unataka kutimiza ni lazima uwe na matarajio makubwa, ndipo utakapoweza kulitimiza hasa pale inapotokea kwamba unakutana na vikwazo vikubwa.

  Bila matarajio makubwa, utasimama na kuacha, utakata tamaa. Wengi tunakata tamaa kwa sababu hatuna matarajio makubwa. Tulishaogopeshwa kujenga matarajio makubwa. Unapohesabu vifaranga kabla havijaenguliwa unapata nguvu kubwa ya ajabu kwa sababu unaona mafanikio, unajua inawezekana na unajua imekuwa tayari.

  Bila kuhesabu au kuogopa kuhesabu kunaweza kukuvunja nguvu na kukufanya uhisi kwamba hakuna la maana, hakuna kitakachozalishwa. Usije ukachanganya kati ya matarajio na matumaini.
  Kutumaini ndiko ambako hakuna maana kwenye maisha. Kutumaini ni kuhisi kwamba kuna siku bahati itatokea na jambo fulani litafanyika na kutakuwa na matokeo fulani siku zijazo.

  Kutumaini si lolote bali ni sala dhaifu, kutumaini siku zote huhusisha mafanikio na maanguko. Wakati matarajio yamefungwa kwenye tokeo moja tu-kufanikiwa. Kuhesabu vifaranga kabla kuna maana kujitilia nguvu matarajio yetu.

  Kwa kutengeneza matarajio, sio tu kwamba unajipa nguvu ya kusonga mbele, bali pia unapata nguvu mpya, unaona jambo likiwa kama limekamilika, hatua ambayo ni muhimu sana katika kukamilisha malengo yetu. Kile ambacho mtu anakitaka kwa uhakika na kuamini kwamba atakipata, huo ndio utabiri anaojifanyia , kwani siku zote huwa kweli.

  Wengine ili kuwa na uhakika ni lazima kwanza waone na kupata uzoefu wa jambo ndipo waamini. Watu hawa ni wale ambao kila siku wanachozungusha kwenye mawazo yao ni vile vitu ambavyo waliviona vikiwezekana na kupata uzoefu wake, nje ya vitu hivyo, vingine haviwezekani. Kwa nini sasa usianze kuamini kwamba jambo litakuwa, na litakuwa kweli ili uanze kujenga picha ambayo utaiamini ili ufanye kwa mafanikio?

  Kwa kuwa na matarajio mtu anajua kwamba jambo litakuwa, litafanyika, anakuwa na matumaini kuhusu uwezekano wa jambo kufanyika. Kwa hiyo kuhesabu vifaranga kabla havijaenguliwa ni jambo zuri sana tofauti na ulivyoambiwa kwamba ni nuksi na halina mwisho mwema.
   
 6. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Vipi kuhusu nguvu ya kunenea na huu msemo wa usihesabu vifaranga Mtambuzi?
   
 7. c

  christmas JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,603
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  very true mtambuzi tena fundisho lako linaingia zaid kwa watu kama sisi ambao ndio kwanza tunatoka kwa wazazi tunaanza kujitegemea bila hata kua na hakika kama maisha tutayamudu, ila mtu ukiwa na matarajio chanya juu ya kitu basi hata nguvu ya kujitahidi kukifanikisha kile kitu utakua nayo japo ni ngumu kiukweli
   
 8. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kwa kiasi kikubwa nakubaiana na wewe Mtambuzi, jamii kwa muda mrefu imejikita kata hofu ya kufanya au kuwa na matarajio makubwa kuepuka kuishia kuumia zaidi mara mipango ya matarajio makubwa inapokwama. Kuna tungo nyingi za zamani zilizotutia hofu kama unapotaka kuvuka mto usitumbukize miguu yote miwili au wenzetu hutumia higher expectations is like building castles in the air, misemo yote ikilenga kuzuia kujikita kufanya jambo kubwa ili kukwepa kuumia zaidi mara jambo hilo linaposhindikana.

  Lakini sijui kwa nini tunasahau kuwa wenye matarajio makubwa wakiweka na bidii na kuwa risk takers ndio hao ambao hufanikiwa kwa kiwango kikubwa na sisi tuliobebeshwa na kukaririshwa misemo hii tunajikuta tunatembea mwendo wa kobe kwenye suala zima la maendeleo, Loh!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. YETOOO

  YETOOO Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtambuzi umenikumbusha nilishawahi kuhesabu vifaranga kabla havijaenguliwa....kuna wakati nilifanya interview moja hivi nikawa na uhakika kabisa kazi nimeipata na waliniita kwenda kwenye salary negotiation,baada ya hapo nikawa nimeshaupangia ule mshahara wa kwanza kwa kusema laki tano nitatoa kama sadaka ya shukrani kanisani,laki nne kwa wazazi na laki nne kwa wakwe zitakazobaki matumizi binafsi,...weee mayai yakabaki viza sikuona kifaranga hata kimoja!!!!!
   
 10. c

  christmas JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,603
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Ila nahisi hii kitu kwa wazungu haipo kabisa, correct me if am wrong
   
 11. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mmmh kweli lakini bila kuvihesabu maana yake unaishi bila mipango, mimi nahisi kuna umuhimu fulani kuvihisabu na pia ni muhimu kuweka plan B. Ni kama ikiwa kuku wangu hatataga basi nitampeleka kwa kuku wa jirani ili atagishwe.

  Mimi huwa navihisabu bwana, nikiwa najiamini na maamuzi yangu.
   
 12. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Siku zote nilikuwa mtu wa machale, nikajaribu kutake risk, nikapamia nimerudi kuwa na machale kwani nitapofanya vizuri zaidi!

  I don't count my chicks before they are hatched!
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  ila Asprin mimi hayo yalinishinda nilinunua nguo na nepi kabla sijakwenda kujifungua na uzuri Mungu ni mwema sana alinielekeza kununua nguo ambazo ni za jinsia zote hivyo nilipopata kadume kangu kalivaa pasi shida yyte ile. to me ilikuwa kama njia ya kumwambia ibilisi Mungu hashindwi and ilikuwa kweli. hofu ndio msingi wa hili asikwambie mtu hapa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. A

  AGNETH Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  mtambuzi hongela kwa messege zako zinafisha ujumbe asante sana .
  nakutakia neema na baraka katika kufanikisha kuelisha jamii poa mtambuzi tupo pamoja (JF)
  I VERY HAPPY MTAMBUZI:flypig:
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  MadameX hivi kweli umesoma nilichoandika au?
  naomba urudie kusoma between line then ndio utoe comment
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  Asante Bw.Mtambuzi somo lako nimelipenda nitakupa mfano wangu mzuri jinsi nilivyokuwa na matarajio makubwa ya kufaulu mtìhani wa kidato cha nne nilitarajia ningepata division 1 but nikaja nikbja kupata three ya 25 point moja pungufu ningekuwa nimefail unaweza kuona jinsi ya kuwa na matarajio makubwa kulivyoweza kunisadia kwa sababu matarajio yangu ilikuwa ni kupata division one ingawa niliumia sana kihisia....ebu fikiria kama ningepata zero ningeumia kiasi gani baada ya matokeo kutoka.....asante sana kwa somo lako Bw. mtambuzi...May God bless you.
   
 17. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  sio kuhisi,ni kweli kabisa.
   
 18. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hiyo inategemea zaidi na aina ya mazingira uliyokulia. Kuna watu hawana uhakika na chochote lakini pia hawana hofu, kwa kuwa tu wamekubaliana na hali halisi kuwa katika dunia yetu ni vigumu kuwa na uhakika wa aina yeyote kwa sababu nguvu na mambo yaliyo nje ya uwezo wetu yanayoweza kuathiri muenendo wa maamuzi na mipango yetu ni mengi sana.

  Hapa bwana mtambuzi nadhani hujaelewa kinachojaribu kufikishwa. Ni kuwa huo msemo unaonesha hali halisi. Maana kuna mengi yanayoweza kutokea kwenye mayai na huwa yanatokea saa nyingine, kwa hiyo kuhesabu vifaranga kabla ya mayai kuanguliwa sio uhalisia kabisa. Kwa hiyo basi kimisingi huo msemo haumkatazi mtu kuwa na matarajio bali unamtahadharisha kuwa kuna uwezekano matarajio yasifikiwe kutokana na sababu mbalimbali. Vilevile sijawahi kuona biashara au mradi wowote ambao hauna changamoto ("risk free") na ndiyo hakuna namna ambayo unaweza kuwa na uhakika wa 100% kuhusu jambo lolote.

  Katika kuendeleza hoja ileile, ni kuwa sio kweli kuamini msemo huo kuna maana ya kuamini hicho unachoeleza hapo juu, bali kuna maana ya kujiandaa kukabiliana na matokeo yeyote yanayoweza kutokea kutokana na mambo mengine yanayoweza kuathiri yale unayoyatarajia.

  Kuna baadhi ya maeneo hapa nchini ambapo mtu hatakiwi kusema kwamba atafanikiwa au kupata sana. Kwa mfano kusema atapata mavuno mazuri ni jambo lisilokubalika sana. Anapokosea na kufanya hivyo, anatakiwa kutema mate chini ili kuvunja balaa ambalo linaweza kutokea. Anachotakiwa mtu kusema ni kwamba hana uhakika, hajui, ‘ndio hivyo hivyo',
  ‘Mungu mwenyewe akipenda nitafanikiwa'.


  Si kweli ni jambo linalotisha bali ndiyo hali halisi. Mimi nakupa changamoto moja, hebu niambie kitu/mradi wa baadaye ambao unaweza kuwa na uhakika nao kwa 100%.
   
Loading...