Kuharibika kwa kiswahili fasaha

Mtanzatozo

JF-Expert Member
Mar 2, 2016
972
1,163
Habari wapendwa natumai wote ni wazima wa afya! nawsalimu kijamhuri ya muungano wa tanzania....!
kiukweli sidhani kma naongea jambo geni au lisilojulikana, ila napenda tu kugusia kwa kuona halipungui zaidi ya kuongezeka.
Llugha ya kiswahili inamchanganyiko wa lugha kubwa ya biashara ambayo ni KIINGEREZA, watanzania wengi walio wasomi sanasana ndio watumiaji wakubwa wa viunganishi vya maneno/sentensi za kiswahili na kiingereza. Mfano; nilipendezwa sana na yule mschana, she was beautiful kwa kweli..! hapa ni neno moja lenye lugha mbili.
Naomba wataalamu na wakuzaji wa lugha ya kiswahili waliangalie kwa jicho la pili, maana tusije kupoteza lugha yetu ttukawa na kizazi kitachoongea lugha nyngine
Note; Tujitahidi kama unatoa sentensi au ujumbe hakikisha una lugha moja ulopenda kutumia kwa wakati huo.
 
Kabisa kadri muda unavyozidi kwenda kuna baadhi ya maneno ya kiswahiki yanapotea. Achana na walisoma hata ambao hawajasoma kuna maneno ya kiingereza wanayatamka kwa kujua ama kutokujua kua hayo maneno si ya kiswahili bali ni kingereza na yana kiswahili chake pia.

Kuna hawa watoto wanaosoma izi private schools toka chekechea, na hawa nduo watakuja kuua kabisa kiswahili aisee. Mtoto akirudi nyumbani kama wazazi nao ni wasomi basi ngeli mwanzo mwisho. Huyu akikua na akawa na familia si ndo ivo ivo kiswahili kitakua kinafifishwa, japo si jambo la siku moja ila miaka hata 50 ijayo hali itakua mbaya.
 
Lugha huzaliwa, hukua na hufa. Kuna uwezekano namna hiyo ya kuongea iko miongoni mwa wafanyakazi au rika lako na kwenye bongo movie lakini katika maeneo makubwa hawaongei kama hivyo.

Badala yake ukiwa Swazi Inter pale karibu na Vegas mtu atasema "Nilimkubali kishenzi yule chura yaani kazi kazi" na bado anawakilisha huo ujumbe wa "Nilipendezwa sana na yule msichana, she was beautiful kwakweli"

Kwahiyo utagundua kua watu wawili wamefikisha ujumbe ule ule ila kutokana na maeneo waliyopo kila mmoja katumia lugha iliyozaliwa na kukulia pale.
 
mfano wako na wangu unatofautiana kwa kiasi kikubwa sana! nimezungumzia tu lugha ya kiingereza na kiswahili tukiachana na mabadiliko yatokanayo na lugha m
za mtaani au mahala husika kutokana na tamaduni zao
 
Nimetoa huo mfano kwakua ilivyo ni kwamba kuna namna ya kuongea inatokea miongoni mwa baadhi ya watu tu katika jamii.

Mfano wa sentensi uliyotoa ni zile za watu wanaojincosider 'elites' au wasomi kama wewe ulivyosema. Yaani hawa elites wanafanya sana code switching na code mixing kama namna ya kuonyesha hadhi yao. Na ni kweli mfano wangu haujabase kwenye code switching wala code mixing ndiyo maana umeona hauendani na ulichotaka kuwasilisha.

Code mixing na code switching zimekuepo kwa muda mkubwa haziwezi kuua lugha isipokua hizi husababisha kuzaliwa neno jipya lenye lugha ngeni na kiswahili au kuliazima neno zima kama lilivyo.
 
Back
Top Bottom