Kuhami nchi isiwe mateka wa wafanyabiashara, Suma JKT iimarishwe

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
8,407
4,076
Kufuatia juhudi za serekali ya awamu ya 5 ya kupambana na wafanya Biashara waliozoea kukwepa kodi , ambao hivi sasa baadhi Yao , wameanza vitimbi vya kuhujumu serikali kwa kutofikisha bidhaa kwa walaji katika muda unaofaa na bei iliyo ya haki.

Ipo haja kwa serikali kupitia Suma JKT kufanya Biashara ya bidhaa hizo kwa angalau 50% ya hizo Biashara , ili kuweka nidhamu kwa pande zote.

Lakini ili Suma JKT iweze kufanya hivyo Lazima iimarishwe kwa kupewa competent staff walio committed to the course mpaka hapo mifumo yake ya usafiri, ukusanyaji wa kodi na utendaji kwa jumla utapokuwa umekoma, wa regulatory authorities Kama TBS , EWURA , TFDA nk
 
Ni vizuri suma jkt iliyo imarishwa kwa lengo la kufanya Biashara ikawa na supermarkets na pia kuwa na fuel outlets zake
 
Walishazoea kukwepa kodi. Ukiwabana walipe kodi inavyotakiwa Wanaona kama wanaonewa. Ajabu sana hii. Nimeamini mazoea hujenga tabia
 
Suma si wanajeshi hao? Ni vizuri kuwa na mipaka ya kibiashara kwa hawa jamaa. Si kila biashara wafanye wao. Supermarket na mafuta mmh! Wasije tu wakafikia kufanya na siasa.
 
Uadilifu wao ukoje?
Nakumbuka mwaka jana tu palikua na bosi mmoja wa SUMA JKT alifikishwa mahakamani kwa ufisadi wa mabilioni ya pesa.Japo alishinda kesi lakini ni jambo la kawaida sana hapa Tanzania kwa mtu aliyekwapua mabilioni ya pesa kushinda kesi.

Pia endapo serikali itawapa SUMA JKT hiyo kazi ya kufanya biashara halafu ukafanyika ufisadi basi itakua ni hatari sana kwani ufisadi unaofanywa na waandamizi ndani ya serikali utakua ni kuiba pesa ilikwisha kukusanywa na kuingizwa serikalini. Itakua ni hasara kwa serikali.

Kuliko pesa ya serikali iliyotoka hazina iibiwe au itumike vibaya ni bora ile inayobakia kwa mkwepa kodi mana anaongeza faida yake kutokana na mtaji wake mwenyewe hivyo kuongeza uwezo wake wa kuajiri watanzania wengine.
Huyu wa serikali atakua ameingiza serikali hasara mara mbili ,ya kuiba na mshahara wa serikali.

Cha msingi ni Kodi iweke kidogo kwa wafanyabiashara ili walipe. Kodi imekua kubwa sana na ushuru kila mahali.
Mfano mtu ananunua basi lake milioni 400 halafu anaajiri dereva na kondakta. Anapangisha ofisi kila mkoa linapopita basi ili aweke maajenti wa kukata tiketi.
Halafua akianza safari kila siku anatoa ushuru wa sh. 3000 kwa kila Halmashauri ya wilaya anyopita na analazimishwa kuingia stand.Akipita wilaya kumi ni 30,000 kila siku . Kwa mwezi ni zaidi ya laki 7 . Kwa mwaka ni milioni 84. Hilo ni basi moja na ni ushuru tu wa halmashauri bado kodi na pesa anazochangia za Tanroad na ewura kila anaponunua mafuta kwa kila lita. Hapo bado kodi ya mapato, Sumatra n.k.

Ukijiuliza serikali inamsaidiaje huyu mfanyabiashara kupata hata huo mtaji ili imwekee kodi nyingi hivi hupati jibu.

Hakuna mfumo wowote mzuri wa kuwasaidia wafanya biashara wa ndani ili wapate faida halali zaidi ya kupandisha kodi tu.
Kuna wawekezaji kule Loliondo wanatumia mabilioni ya serikali kwa kuomba kila siku kupatiwa ulinzi wa polisi kutokana na migogoro waliyoisababisha. Ukiangalia kodi wanayotoa kwa asilimia kubwa bado inawanufaisha wao na kuwaacha wananchi wakiteseka bila Ardhi na kuzidisha umaskini kwa watanzania na migogoro kila mkoa kutokana na watu kuhamishwa kupisha wawekezaji wakubwa wa nje.

Kwa kifupi hii hali ya inasababisha hawa wawekezaji wasiwe na faida kubwa kwa taifa letu zaidi ya kutumia gharama kubwa za kuwalinda mpaka wakati mwingine kupoteza maisha ya watu wetu.

Serikali inakimbizana na kodi za wafanyabiashara ambao kimsingi hawakwepi kodi ila ni uzembe tu wa Serikali kutotaka kuwasikiliza na kuona umuhimu wa kuwawekea mazingira mazuri ya kupata faidi.
Bidhaa iliyopita bandarini imekwepaje kodi bila idhini ya serikali?

Na serikali inategemea kupandisha kodi tu kila siku kwa wafanyabiashara badala ya kuangalia vyanzo vingine vipya vya kodi. Mikataba mibovu ya madini na gesi inawanufaisha wachache tu.
Hivi ikitokea hao wanaonunua vitu toka nje siku wakaamua kuachana na hiyo biashara serikali itajiendeshaje?
Kwa sababu hata wakiingiza hawaiathiri serikali kwa kuwa hawaingizi bidhaa kwa pesa ya serikali.

Mfanyabiashara ndiye anayeinufaisha serikali na sio serikali inayomnufaisha mfanyabiashara kwa kuwa siku akiamua kuacha serikali inakosa mapata hata yale kidogo.

Leo hii tunadanganyana kuwa hawa wafanyabiashara wanaiibia serikali!!
Wanaiibia kwa mtaji upi walioweka ubia na serikali????

Serikali inaibiwa na mashirika makubwa kama UDA na Madini, gesi na Mabenki ambapo ina ubia huko lakini mtu anauza genge lake kwa kamtaji kake alikokapata kwa biashara ya kuokota chupa za maji halafu unamwambia anaiibia serikali kisa anajificha kutokana na iuwekewa kodi kubwa kwa mtaji alioutafuta mwenyewe.

Serikali inaibiwa na wale waliokua wanakopa pesa za mabilioni ya JK halafu wametokomea bila kurejesha na sio wafanyabiashara wanaonyimwa mikopo kutokana na kukosa rasilimali zisizohamishika.

Tunaiomba Serikali ipunguze mlolongo wa kodi kwa wafanyabiashara na pia iweke mazingira bora kwa watu kupata mikopo yenye riba nafuu.
Riba kubwa kwenye mabenki ,kodi kubwa kwenye biashara. Halafu serikali inawapangia mishahara ya kuwalipa mpaka vibarua kwa hao wafanyabiashara.
 
Ni vizuri suma jkt iliyo imarishwa kwa lengo la kufanya Biashara ikawa na supermarkets na pia kuwa na fuel outlets zake
Mukialike na chama cha kikomunisti cha china nacho kije kufungua supermarkets.
 
Nakuunga mkono kwa 100% na asielewa hata elewa kamwe, tatizo kodi ni nyingi na kubwa mno , pili mfumo wa kodi unamlazimisha mfanyabiashara yeyote aidha kufunga biashara au akwepe, watu hawajiulizi ni kwa wakwepe wooote ? makampuni , wakubwa kwa wadogo woote wanakwepa hayupo hata mmoja mlipaji mzr, hongera sana kwa kuielewa vema nchi yako
 
Kufuatia juhudi za serekali ya awamu ya 5 ya kupambana na wafanya Biashara waliozoea kukwepa kodi , ambao hivi sasa baadhi Yao , wameanza vitimbi vya kuhujumu serikali kwa kutofikisha bidhaa kwa walaji katika muda unaofaa na bei iliyo ya haki.

Ipo haja kwa serikali kupitia Suma JKT kufanya Biashara ya bidhaa hizo kwa angalau 50% ya hizo Biashara , ili kuweka nidhamu kwa pande zote.

Lakini ili Suma JKT iweze kufanya hivyo Lazima iimarishwe kwa kupewa competent staff walio committed to the course mpaka hapo mifumo yake ya usafiri, ukusanyaji wa kodi na utendaji kwa jumla utapokuwa umekoma, wa regulatory authorities Kama TBS , EWURA , TFDA nk
ndoto za alinacha ,sio kila unachofikiri kinawezekana,kwanza serikali haiwezi kuwa na fedha za namna hiyo,dunia ya leo hamna serikali inayofanya fikra kama za kwako,uchumi unapangwa na mabepari
 
Back
Top Bottom