kugombana na kushindwa kupatana

kugombana na kushindwa kupatana

iron.heart

Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
59
Reaction score
15
Hivi unajua kwanini wanaume na wanawake wengi hugombana na kushindwa kupatana katika uhusiano
wao? Hebu soma hapa ufaidike.

ILI nisichoshe na maneno mengi,
nitachanganya pamoja baina ya vyanzo, namna ya kuepusha, kusuluhisha na lipi tucompromise na lipi tusicompromise.

Kwanza
Ni kusomana tabia na kujuana ili tujue
kosa lipi ni la kitabia na lipi ni la kibahati mbaya, lile la kitabiya liwekewe malengo ya kurekebishwa kidogo kidogo na lile la bahati mbaya
litathminiwe na kujengewa mazingira ya kutokurejea tena kisha lisamehewe.

la pili,
Ni kuhakikisha sisi binafsi hatuwi sababu ya wenzetu kuleta hizo conflicts, tujitathmini ili mazingira yawe yanamfanya mke/mume wetu asiwe na sababu ya kuleta malumbano, tujitahidi kutimiza majukumu yetu na kuwajali wenzetu.

La tatu:
Ni kuamini kwamba hakuna mkamilifu
katika binadamu

La nne:
mafahali wawili hawakai zizi moja, ni
kukubali kujishusha mmoja pale joto la
wawili la hasira linapokuwa juu

La tano
ni uchaguzi bora wa lugha, inaweza
ikawa umekosewa wewe kosa dogo
lakini ukatumia lugha kali ambayo ikazaa kosa kubwa zaidi ya lililokuwepo

La sita ,
kuwa na tabia ya kukubali makosa yetu pale tunapokosea, na tumaanishe
kuomba radhi kwa kujirekebisha, isiwe
tunaomba radhi leo kesho kutwa kosa
linarejea.

La saba:
Kuchagua mazingira mazuri ya
kuanzisha malumbano au mjadala
unaohusu tatizo lililojitokeza. Hata
ikibidi kugharamika kulipia sehemu
ambayo italeta utulivu wa akili

La nane:
kuepuka kutumia kisasi kama ni njia ya kusuluhisha

La tisa:
kuacha ubinafsi ikawa wewe siku zote
upo sahihi au una mamlaka kuliko
mwenzako katika suala la migogoro,
ubinafsi ambao unakupa kiburi kwamba unalofanya wewe halina kosa hata kama ni kosa.

La kumi:
Epuka kuwashirikisha watu wa nje
katika migogoro ya ndani ya ndoa.
Wapishi wengi huuharibu mchuzi.

La kumi na moja:
Usishutumu kwa kudhania, moyo ni
mwepesi kuvunjika kwa shutuma zisizo za kweli

La kumi na mbili:
Makosa madogo madogo ya
kibinadamu yapuuzwe (mfano, chumvi
imetiwa nyingi kwenye mchuzi). Hapa
iingie na kuvumiliana pia.

Mwisho
nimalizie na suala liliopo juu, lipi
tucompromise na lipi tusicompromise?
(samahani nimetumia kiswanglish
kwakuwa nieleweke zaidi lol)

Jibu:
mgogoro wowote tunaweza
kucompromise (kuafikiana) hata uwe na ukubwa wa jabali kama kuna MAPENZI ndani ya ndoa baina ya wawili , na mgogoro wowote hatuwezi kuafikiana (kucompromise) hata uwe mdogo kama chembe ya mchanga kama hakuna MAPENZI kwa mmoja kati ya wanamgogoro au wote wawili.

Kwahiyo nadiriki kusema
unapocompromise() kwanza angalia
kama mapenzi yapo? kama hayapo basi nadiriki kusema unasubiri meli uwanja wa ndege.

NIMEMALIZA, na hayo ni maoni yangu tu inaweza nikawa sipo sahihi!
 
Back
Top Bottom