Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,275
- 18,352
Habari za majukumu wakuu.
Pole na pilika za kutafuta maisha sambamba na kupambana na janga la Covid-19. Mungu ni mwema atatuvusha, tuendelee kuchukuwa tahadhari kujikinga na kuwakinga wenzetu.
Niende kwenye kiini cha mada yangu.
Kuna tabia flani imezuka au nisema labda ilikuwepo hata kwa watangulizi wetu (babu na bibi enzi hizo), unakuwa na rafiki ama ndugu yako mnashibana sana, mnasikilizana sana. Inatokea anapata shida au dharura, anakujia umkopeshe fedha kiasi flani aweze kutatua shida yake.
Kutokana na mnavyoheshimiana roho inakwambia sio vema uache kumsaidia rafiki yako au ndugu yako, unaingia ndani unakomba akiba yako kiduchu uliyokuwa nayo unampa kwa ahadi ya kurejesha baada ya siku mbili tatu let say anakwambia baada ya siku 2 atarudisha.
Unampa anashukuru sana anaondoka, sasa unakaa wiki mbili au mwezi au miezi kadhaa baadae hujapata mrejesho hata wa kuambiwa labda amekwama au mambo yalikwenda tofauti na alivyotarajia, yaani anakaa kimya tu, unamuona mitandaoni akipost mavitu kwa furaha tele, anasahau wewe ulijibana ukamuazima fedha ashughulikie shida iliyomkabili wakati ule.
Hebu wakuu tuelezane kiutu uzima hii tabia ya kitoto namna hii huwa inalenga nini? Kwamba marafiki tusisaidiane mwenzetu anapopata shida? Tabia kama hii inajenga picha gani na wewe unayekopeshwa na hurejeshi wala kutoa taarifa kwamba umekwama somewhere hii ni nini? Mambo ya kijinga kabisa.
Mtu anakukopa unamheshimu sana kiasi kwamba hata kumdai unaona aibu, lakini yeye kwa ujasiri mkubwa anakupotezea as if wewe huna shida na fedha.
Vijana wenzangu, wazee, mabibi na mabwana hebu tuache mambo ya ajabu, mtu utakuja kupata shida watu wanakukwepa maana una tabia ya kudhurumu kirahisi rahisi.
Najua mnanielewa, wewe mwenye tabia kama hii iache maana haina siha njema, watu tunaishi kwa kutegemeana, usilazimishe tuishi kwa kubaguana tukashindwa kusaidiana.
Tuendelee kunawa mikono kwa maji tiririka na tutumie vitakasi mikono vyenye alcohol isiyopungua 60%
Asanteni kwa kunielewa.
Sent using Jamii Forums mobile app