Kufungwa kwa shule na vyuo: Waajiriwa wa taasisi binafsi watalipwa fao la kukosa ajira?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,005
Kutokana na shule na vyuo vingi vya binafsi kutegemea ada za wanafunzi kujiendesha ikiwa ni pamoja na kulipa mishahara.Na ukweli kwamba sasa hawataweza kulipa tena mishahara kwa wafanyakazi wao kwani haijulikani iwapo corona itaisha hivi karibuni.

Kwa vile watumishi hawa wamekuwa wakikatwa pesa zao katika mifuko ya hifadhi ya jamii;Je!Mifuko hii hususan NSSF watalipa fao la kukosa ajira iwapo waajiri watashindwa kulipa mishahara?

Maana kuna wengine wameshaanza kutoa likizo za bila malipo hadi corona itakapomaluzika.Na hali inavyoelekea,hii sio ya leo ama kesho.Kwa ujumla hali ni tete.Naomba viongozi wa kisiasa kwa hili nalo watoe mwongozo.Maana hizi pesa kwenye hii mifuko kazi yake itakuwa imefika.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo mnaanza kunielewa ile thread yangu ya Silent lockdown,si hao tu kuna wanamuzik kibao hali zao mbaya,wanamichezo na waamuz wa michezo ya mchangan n.k hii inawahusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom