Kufungwa kwa flow meter, game changer!

Kufungwa kwa flow meter, game changer!

TRUVADA IQ yako ni zero kama huwezi kuutambua mchango wa wapinzani basi wewe bila shaka una mtindio wa akili.
 
Kwa hiyo usalama wa taifa,management ya bandari na top officials walikua hawalijui hili ?

Wanajua ila kwa kuwa ni wanufaika hawakuona umuhimu! Walichosahau ni kwamba, kila lenye mwanzo lina mwisho! Walizani wataendelea na mizaha yao kama desturi! Nami nashauri wote wawajibishwe hadi mkuu wa nchi aliekuwepo wakati husika!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hiyo flow meter ndiyo inayoliza watu, mayowe yote yako hapo, fikiria hili kwa miaka zaidi ya mitano flow meter iliyonunulia kwa mamilioni ilikuwa haitumiki, ina maana mafuta yalikuwa yanaingia nchini kwa zaidi ya miaka 5 bila kukatwa kodi, sasa hiyo ni fedha kiasi gani? Na nani alikuwa anachukuwa ? Yaani wanufaika wa huwo Ufisadi ni akina nani? Kwa maana Mwarabu hawezi kuondoa flow meter na muondoaji hawezi kuondoa bila bosi wake kujua sasa hiyo cheni inapanda mpaka wapi?

Na siyo hapo tu, fikiria msululu wa watu waliokuwa kwenye payroll ya huu ufisadi, kwa maana sijawahi kusikia hata siku moja Bungeni kwa miaka 5 iliyopita watu wakiigeuza hii kuwa ishu waliichukulia kana kwamba ni ishu ndogo tu, kwa hali ya kawaida ukizingatia fedha iliyokuwa inaibiwa hii ilipaswa hata kubomoa Baraza la Mawaziri, lkn wapi!

Je Kamati za Bunge zilizopita ambazo ziliundwa na Upinzani +CCM hawakuliona hili? Na kwa nini walikaa kimya? Iweje hoja ya Wanafunzi Udom ambao hawakuwa na sifa itake kusimamisha Bunge lkn hii ya flow meter ambayo tumepoteza mabilioni ya fedha sijawahi kusikia Bunge likisimama?

Dokezo tu, rejea hoja ya Zito Kabwe kuhusu upungufu wa mafuta aliyoitoa Bungeni kwamba kulikuwa na mafuta ya kutosha siku kadhaa tu, na ndege zisingetua TZ, kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiria kidogo utajua kabisa kwamba Zito Kabwe ana ukaribu na ishu ya mafuta hapa Tanzania hivyo sichelei kusema kwamba hata yeye yuko kwenye payroll ya wizi huu, kumbuka hata ktk urafiki wa kawada tu kama girlfriend wako akikushika unachepuka halafu akaamua kukusamehe lkn ukweli ni kwamba hatosahau kamwe na siku zote kitu au jambo litakalo wagombanisha ni lile lenye uhusiano na kuchepuka kwako, ugomvi wenu wote maisha yenu yote utazungukia hapo hapo tu kwenye hiyo ishu, sasa ugomvi na malalamiko ya Zito Kabwe & Co. yanazunguka hapo hapo tu kwenye mafuta, atatuhumu kila kitu lkn mwisho wa siku anazungukia hapo tu kwenye mafuta, na anatumiwa na wale ambao pia wameshikwa lkn hawana uwezo wa kutoka na kusema hadharani, lkn ukweli ni kwamba hii flow meter ni game changer na mengi yanakuja, kuanzia sabotage mpaka vitisho ambavyo tayari tumevisikia Zito Kabwe Kiongozi wa Chama chenye Mbunge mmoja ambaye ni yeye anamwambia Raisi aliyetokana na Chama chenye Wabunge 200 na aliyeshinda kwa tofauti ya kura Milioni 2 au ~20% ya kura zilizopigwa kwamba ni one term president, angalau ukawa wangesema hivyo labda kidogo ingeleta maana kwa maana walipata 39% ya kura na wana Wabunge 70 na ushehe lkn Zito Kabwe mwenye Mbunge mmoja yaani amepata 0.00...% ya kura zote anampiga Raisi wa JMTZ mkwara kwamba ni one term president na kwamba CCM wamuonye Raisi wao, Duh hapo ndipo nilipochoka ...
Mtambo unaoliza watu, karibia unakamilka!​

FLO3.jpg
Sijaelewa hapa, kwamba ulitaka wabunge wa upinzani ndo waseme kuhusu flow meter na si suala la Dodoma au?, tokea hilo suala limetokea na akatajwa Waziri kuhusika nini kimetokea baada ya hapo?, nani alihusika na kachukuliwa hatua gani?, umewezaje kumuingiza Zitto alafu ukawaacha mawaziri wenye dhamana na viongozi wengine?,Zitto kama kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo anasimamia pia msimamo wa chama, tunamuunga mkono Magufuli kwa juhudi zake za kupambana na ufisadi na ACT ndo chama pekee cha upinzani ambacho tokea awali kimekuwa kikimuunga mkono Magufuli kwa juhudi zake, lakini tunalaani hatua zake za kukandamiza Demokrasia, kumbuka kabla hujaenda huko kusema Zitto kuna jambo anakosa, kumbuka amefanya mkutano akaitwa Polisi hiyo kitu haikuwepo katika Utawala uliopita unataka Zitto aweje?, unataka atulie kuona Demokrasia inakanyagwa?, na hata katika hotuba yake, alisema anaona Magufuli atatawala kipindi kimoja kwa sababu Wananchi hawatakubali kunyimwa uhuru wa habari, narudia tena na yeye amekuwa akisema anaunga mkono juhudi za kupambana na ufisadi lakini kitendo chake cha kuminya Demokrasia tutakipinga daima
 
Uandishi Ndo huu tunaotaka nimeipenda bila masharti
 
Safi sana kwa maelezo mazuri,hii nchi wachache wameila na kuimaliza.Wapinzani nawaunga mkono kwa harakati zao za kufichua huozo ila Nina mashaka sana na mheshimiwa Zito naona mala hii amekomaa kwelikweli kama mpinzani wa kweli kinacho nishangaza Siku za nyuma alikuwa wapi?madudu yote yaliyofanyika alikuwa wapi? Sasa hivi Raisi mzalendo wa kweli kivitendo amejitoa muhanga kupambana na huovu kwa nguvu zote lakini MTU kama zito anaibuka kuzuia juhudi za raisi,bila shaka kuna kitu Zito kakikosa hawamu hii hapa lazima tujiulize!.Watanzania wote tumuunge mkono raisi madamu tunaona wenyewe kazi anayoifanya ya kutumbua majipu bila kujali urafiki na MTU.Mimi naona Mungu ana mpango wa kuinusuru Tanzania kupitia kwa JPM.

HAWAMU=AWAMU....punguza jazba,hata magufuli kuna vitu kavikosa awamu hii ndo mana kawa mtumbua majipu..tumia darubini utaona hasa ndani ya chama chake
 
Swali la msingi la kujiuliza hizo mita zilizofunguliwa zinafanya kazi au ziko katika hali gani. Mana usitake tu sifa ya kuwa umeibua swala la flow meter za bandari wakati. Story yako haijawa na uendelevu baada ya waziri mkuu kutoa maagizo nini kimefanyika na nini hakijafanyika mpaka sasa hivi. Wewe bwana Mwandishi wa Jamuhuri tuletee developing story ya baada sakata zima nini kinaendelea.Ili hizo sifa unazozilazimisha kupewa ziwe na msingi mzima wa habari iliyokamilika
 
Sasa mbona wapinzani waliposema Mkwere dhaifu mliwapinga? Wapinzani wasingeweza kusema kila kitu Mkwere alikuwa na madhaifu mengi hivyo hili la mita lilijumuishwa kwenye kauli moja ya mnyika "Rais Dhaifu" ambayo mliipinga

Mhe Rais mstaafu angekuwa dhaifu tusingefika hapa, kila mtu na zama zake, yeye alikuwa fair mkapiga kelele haya kaja mtendaji tena makelele, mnataka mtu wa namna gani, Zitto yupo vizuri kihoja ila kuna mda huwa simuelewi labda kuna ukweli wa hoja hapa , muda utatuambaa majibu sahihi
 
inaweza kuwa flow meter ndo ilichangia kuwepo kwa petrol stations nyingi kutoka Dar hadi Chalinze. hongera kwa gazeti la jamhuri kwa kuibua ishu hii. yule mama wa wakala wa vipimo namuonea huruma nadhani uhusika wake ni mdogo katika ishu hii ni kama alikuwa anapokea maelekezo tu lazima kutakuwa na mapapa wa ufisadi huu.
 
Back
Top Bottom