Kufungwa kwa flow meter, game changer!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hiyo flow meter ndiyo inayoliza watu, mayowe yote yako hapo, fikiria hili kwa miaka zaidi ya mitano flow meter iliyonunulia kwa mamilioni ilikuwa haitumiki, ina maana mafuta yalikuwa yanaingia nchini kwa zaidi ya miaka 5 bila kukatwa kodi, sasa hiyo ni fedha kiasi gani? Na nani alikuwa anachukuwa ? Yaani wanufaika wa huwo Ufisadi ni akina nani? Kwa maana Mwarabu hawezi kuondoa flow meter na muondoaji hawezi kuondoa bila bosi wake kujua sasa hiyo cheni inapanda mpaka wapi?

Na siyo hapo tu, fikiria msululu wa watu waliokuwa kwenye payroll ya huu ufisadi, kwa maana sijawahi kusikia hata siku moja Bungeni kwa miaka 5 iliyopita watu wakiigeuza hii kuwa ishu waliichukulia kana kwamba ni ishu ndogo tu, kwa hali ya kawaida ukizingatia fedha iliyokuwa inaibiwa hii ilipaswa hata kubomoa Baraza la Mawaziri, lkn wapi!

Je Kamati za Bunge zilizopita ambazo ziliundwa na Upinzani +CCM hawakuliona hili? Na kwa nini walikaa kimya? Iweje hoja ya Wanafunzi Udom ambao hawakuwa na sifa itake kusimamisha Bunge lkn hii ya flow meter ambayo tumepoteza mabilioni ya fedha sijawahi kusikia Bunge likisimama?

Dokezo tu, rejea hoja ya Zito Kabwe kuhusu upungufu wa mafuta aliyoitoa Bungeni kwamba kulikuwa na mafuta ya kutosha siku kadhaa tu, na ndege zisingetua TZ, kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiria kidogo utajua kabisa kwamba Zito Kabwe ana ukaribu na ishu ya mafuta hapa Tanzania hivyo sichelei kusema kwamba hata yeye yuko kwenye payroll ya wizi huu, kumbuka hata ktk urafiki wa kawada tu kama girlfriend wako akikushika unachepuka halafu akaamua kukusamehe lkn ukweli ni kwamba hatosahau kamwe na siku zote kitu au jambo litakalo wagombanisha ni lile lenye uhusiano na kuchepuka kwako, ugomvi wenu wote maisha yenu yote utazungukia hapo hapo tu kwenye hiyo ishu, sasa ugomvi na malalamiko ya Zito Kabwe & Co. yanazunguka hapo hapo tu kwenye mafuta, atatuhumu kila kitu lkn mwisho wa siku anazungukia hapo tu kwenye mafuta, na anatumiwa na wale ambao pia wameshikwa lkn hawana uwezo wa kutoka na kusema hadharani, lkn ukweli ni kwamba hii flow meter ni game changer na mengi yanakuja, kuanzia sabotage mpaka vitisho ambavyo tayari tumevisikia Zito Kabwe Kiongozi wa Chama chenye Mbunge mmoja ambaye ni yeye anamwambia Raisi aliyetokana na Chama chenye Wabunge 200 na aliyeshinda kwa tofauti ya kura Milioni 2 au ~20% ya kura zilizopigwa kwamba ni one term president, angalau ukawa wangesema hivyo labda kidogo ingeleta maana kwa maana walipata 39% ya kura na wana Wabunge 70 na ushehe lkn Zito Kabwe mwenye Mbunge mmoja yaani amepata 0.00...% ya kura zote anampiga Raisi wa JMTZ mkwara kwamba ni one term president na kwamba CCM wamuonye Raisi wao, Duh hapo ndipo nilipochoka ...
Mtambo unaoliza watu, karibia unakamilka!

FLO3.jpg
 
Safi sana kwa maelezo mazuri,hii nchi wachache wameila na kuimaliza.Wapinzani nawaunga mkono kwa harakati zao za kufichua huozo ila Nina mashaka sana na mheshimiwa Zito naona mala hii amekomaa kwelikweli kama mpinzani wa kweli kinacho nishangaza Siku za nyuma alikuwa wapi?madudu yote yaliyofanyika alikuwa wapi? Sasa hivi Raisi mzalendo wa kweli kivitendo amejitoa muhanga kupambana na huovu kwa nguvu zote lakini MTU kama zito anaibuka kuzuia juhudi za raisi,bila shaka kuna kitu Zito kakikosa hawamu hii hapa lazima tujiulize!.Watanzania wote tumuunge mkono raisi madamu tunaona wenyewe kazi anayoifanya ya kutumbua majipu bila kujali urafiki na MTU.Mimi naona Mungu ana mpango wa kuinusuru Tanzania kupitia kwa JPM.
 
Barbarosa sis maadui ila kwa hili nakuunga mkono pia rais apongezwe pamoja na majaliwa. Mim ni muumin mzur wa kulipa kod kubana matumiz na kuweka akiba.

Serekal iliyopita should be accountable for messing up peoples lives. Yan mijitu kama michwa ni kutafuna tuu. Yan licha ya kuikomba hii nch miaka yote iyo aina hata aib na kias kwa sasa hiv kuzibiwa mirija had inamtuma zitto. They should be grateful really katika nch zingine za waelewa sasa hiv wangekuwa nyuma ya nondo.

Ngoja niendelee kupiga hapa mzigo nitarud kwa ajil ya Hidaya
 
Jamani Watanzania tuwe tunajenga utamadumi wa kitambua kazi za watu.

Hili la Flow Meter kila tunapolizungumza tusione aibu kutaja wazi kuwa liliibuliwa na Uchunguzi wa Gazeti la Uchunguzi la JAMHURI hadi Rais Magufuli akalisifia.

Nawatakia mjadala Mwema.

Balile
 
Ni Zito Kabwe ambaye tangu mwanzo alikataa kupokea posho za vikao vya bunge. Lazima mtu wa kawaida ajiulize anaishi kwa kutegemea nini lazima ipo namna. Sasa mrija huu unazibwa kelele amezianzisha. Viva Mheshiwa Rais ziba mirija yote ndio watu tutafanya kazi na tuishi kwa vipato halali.
 
Jamani Watanzania tuwe tunajenga utamadumi wa kitambua kazi za watu.

Hili la Flow Meter kila tunapolizungumza tusione aibu kutaja wazi kuwa liliibuliwa na Uchunguzi wa Gazeti la Uchunguzi la JAMHURI hadi Rais Magufuli akalisifia.

Nawatakia mjadala Mwema.

Balile
Kwa hiyo usalama wa taifa,management ya bandari na top officials walikua hawalijui hili ?
 
Safi sana tumepata Raisi wa kuigwa nchi hii lazima iende Mungu yuko pamoja na JPM la msingi Raisi aangalie mapolisi wasiwaonee vyama pinzani maana bila wao mambo hayaendi maana wale maadui wa nchi hii watakosa MTU wa kuwasema na juhudi zs raisi zitagota sehemu maana jamaa watalindana ns kumkwamisha.
 
Kweli kabisa. Hivi vyama vya upinzani bwana, viliachia ufisadi kwenye mafuta kwa miaka yote hii..... na sasa serikali mpya imekuja na mwarobaini, wanailalamikia. This is what you seem to be saying. Moron.
 
Tulipoandika hiyo Habari, Waziri mmoja akatuma SMS kwa mmoja wa wakurugenzi akihoji imekuwaje zifungwe kwa miaka mitano na kwa nini zisifunguliwe.

Huyo Mkurugenzi akaituma SMS hiyo kwa mama wa Vipimo na mama wa Vipimo akaziwasha Siku hiyo hiyo.

Waziri Mkuu naye mchana akaenda kuangalia nini kinaendelea akamtaka mama wa vipimo ajieleze kufikia saa 11 jioni.

Baada ya hapo mama wa Vipimo akasimamishwa kazi kupisha Uchunguzi.

Baadaye tukachapisha Barua ya Mgawe akimuonya mama Chuwa kuwa uamuzi wa kuzima Mita aliuchukua bila kushauriana na wengine na akamuonya kuwa ungemgharimu.

Yaliyobaki ni historia
 
umeongea vizuri sana na inawezekana ukawa na uelewa mzuri sana wa haya mambo..ila tatizo langu lipo sehemu moja tu..vijana wa ccm sijui niwaweke kundi gani..walipoambiwa raisi wao na serikali ni DHAIFU walikua kama mbogo..walitoa mapovu sana na kumtetea kwa kila hali..kaja Magu anafumua uozo mnaanza tena kumshangilia na kumponda aliyepita...ndo mnaona udhaifu wake sasa hivi..nashindwa niwaweke kundi gani..tuachane na hayo
kuna kipindi mlikua mnasema zitto ndo mpinzani wa ukweli na ana akili kuliko wapinzani wote..alipogoma kuandamana na kutoka nje ya bunge mulimsifia kweli kweli sasahivi kaanza kuisema serikali mnamponda...mnafichua tusiyoyajua..bado nawaza niwaweke kwenye kundi gani nyie vijana wa ccm...
 
Jamani Watanzania tuwe tunajenga utamadumi wa kitambua kazi za watu.

Hili la Flow Meter kila tunapolizungumza tusione aibu kutaja wazi kuwa liliibuliwa na Uchunguzi wa Gazeti la Uchunguzi la JAMHURI hadi Rais Magufuli akalisifia.

Nawatakia mjadala Mwema.

Balile
Hapa goli linahamishwa!?.
 
Tulipoandika hiyo Habari, Waziri mmoja akatuma SMS kwa mmoja wa wakurugenzi akihoji imekuwaje zifungwe kwa miaka mitano na kwa nini zisifunguliwe.

Huyo Mkurugenzi akaituma SMS hiyo kwa mama wa Vipimo na mama wa Vipimo akaziwasha Siku hiyo hiyo.

Waziri Mkuu naye mchana akaenda kuangalia nini kinaendelea akamtaka mama wa vipimo ajieleze kufikia saa 11 jioni.

Baada ya hapo mama wa Vipimo akasimamishwa kazi kupisha Uchunguzi.

Baadaye tukachapisha Barua ya Mgawe akimuonya mama Chuwa kuwa uamuzi wa kuzima Mita aliuchukua bila kushauriana na wengine na akamuonya kuwa ungemgharimu.

Yaliyobaki ni historia
sifa ni hulka ya kila mwanadam. Haya bana hongereni na msirud nyuma. Vp la UDA jikiten pia hapo had Kwa babu seya na mwanae walau mumlipizie kisas mzee wetu Ngoyai
 
Sasa mbona wapinzani waliposema Mkwere dhaifu mliwapinga? Wapinzani wasingeweza kusema kila kitu Mkwere alikuwa na madhaifu mengi hivyo hili la mita lilijumuishwa kwenye kauli moja ya mnyika "Rais Dhaifu" ambayo mliipinga
 
Back
Top Bottom