Kwa CBO (Community Based Organisation) unatakiwa kuandaa katiba ya Kikundi husika, Orodha ya wanachama waanzilishi ,Muhtasari wa kuazimia kuanzisha Asasi hiyo na barua ya maombi ya usajili (Barua ielekee Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri uliyopo).Kisha unapeleka Idara ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri uliyopo kwa ajili ya usajiri.
Kwa uzoefu wangu Ada ya usajili wa CBO ni 20,000/- hadi 50,000/- tu.
Kuanzisha NGO inatakiwa pia uwe na orodha ya wanachama waanzilishi, katiba ya asasi na muhtasari wa kikao kilichoazimia kuanzisha asasi hiyo .Kisha unaandika barua ya maombi ya kusajili asasi (NGO) kwa DAS wa Wilaya ambayo mnakusudia kuwepo Makao makuu ya Asasi yenu.
Baada ya hapo DAS atawahoji baadhi ya mambo Kisha ataandika barua ya kuomba usajili wa asasi yenu kwenda kwa Msajili.Barua hiyo atwapatia mtaiambatanisha pamoja na orodha ya nyaraka nilizozitaja hapo juu pamoja na barua yenu ya maombi kwa msajili.
Ada ya usajili wa NGO unatofautiana kulingana na wigo wa kijografia mnaouhitaji.Kwa mfano:NGO ya kufanya kazi katika Wilaya pekee,Mkoa ,Tanzania nzima au Kimataifa.
Nadhani nimejitahidi kukeleza kadri ya uzoefu wangu.
Kwa msaada zaidi ni-PM.