Kufunga ndoa kiurahisi kupitia nyota | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufunga ndoa kiurahisi kupitia nyota

Discussion in 'Love Connect' started by MziziMkavu, Sep 14, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  NYOTA YA PUNDA NA MIZANI


  Mpate mpenzi siku ya Ijumaa kwenye sherehe za ngoma saa 3 au saa 9, vaa nguo rangi mbili juu nyekundu chini njano. Mshike mkono mara kwa mara, hakikisha mnakula kabla ya mazungumzo
  NYOTA YA NGOMBE NA NGE  NgÂ’ombe: kutana nae saa nane na uwe peke yako, Vaa nguo ya rangi ya kijani iwe siku ya Jumanne saa 2 au saa 8. Mpe chakula cha mafuta mafuta na rojo rojo. Mkutanishe na jamaa zako wa nyumbani usimtazame usoni, mguse guse shingo na mapaja. Penda kuimba imba au vaa Walkman. Tendo la ndoa liwe refu na la kurudia rudia.


  NYOTA YA MAPACHA NA MSHALE  Penda sana kuzungumza kiingereza au kusoma soma na kushika gazeti unapotembea mbele yake. Kutana nae siku ya Jumatano saa 9 na mpende ndugu yake wa pili. Penda kutafuna tafuna Big G na zungumza utani kwa wingi huku ukizungumza upesi upesi. Vaa nguo za kitoto fupi na usikose mkanda.


  NYOTA YA KAA NA MBUZI


  Penda sana kununa, usicheke hovyo, mpe vitu baridi kama peremende, ice cream, na vitu vya kunyonya. Mvamie na umshike shike kitovu pia mfinye finye vidole. Tembea nae taratibu na uzungumze nae pole pole, penda sana mambo yake. Vaa nguo ya rangi ya bluu isiyoiva. Lazima muishi sehemu za bondeni na nyumba yenu iwe na choo cha ndani na sehemu ya kulia chakula. Kutana nae Jumamosi au Jumapili saa 4 au saa 10. Zungumza nae kwa kigugumizi.


  NYOTA YA SIMBA NA NDOO


  Mpenzi apende kukandwa na kutolewa ukali na mtembee kwa haraka, saa za mapumziko ziwe saa 1 na saa 5. Awe muhongaji na mkae karibu na nyumba ya kona. Mwanamke avae Kofia au Ushungi na kiuno akibane kwa Mshipi au kanga. Tendo la ndoa liwe fupi na la kurudia lakini pendelea kukandana. Kutana nae siku ya Jumapili ambayo ndio siku ya Mapenzi.


  NYOTA YA MASHUKE NA SAMAKI  Chagua mpenzi asiesoma zaidi kuliko aliyesoma, utampata mpenzi wa ndoa tarehe 30 na huenda mkakutan hospitali au hotelini au baada ya ajali. Kuwa maridadi, viatu virefu vya kisigino na mlio. Usikose senti ndogo na uoneshe kulia au kukata tamaa na kumuhudumia katika ugonjwa wake au jamaa wake wa kike. Kutaneni siku ya Alhamisi.
   
 2. salito

  salito JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Kaka hapa hata sielewi,hizi nyota unazijuaje??ni za watu au??na mtu unajuaje nyota yako?
   
 3. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ay see...........
   
 4. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  MziziMkavu, naona ushaanza kuwa mtaalam wa ramli sasa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Unajimu!

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. mwathu

  mwathu JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 406
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Duuuuh hii nouma kuliko hata ya shehe yahya
   
Loading...