Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,865
- 730,439
Labda iwe ni kwasababu zisizozuilika kabisa kama kuthibitisha kuwa maiti ni yenu kweli baada ya kutokea makosa mochwari na hili ni la kibinadamu na kiupendo zaidi na si kwasababu nyingine yoyote ile kwakuwa roho ikishaachana na mwili kinachobaki ni kasha tu au jumba tupu.
Kuna hatari za kukutana na mambo ya ajabu huko kaburini , wengine hukuta maiti zimezikwa na mambo ya ajabu kabisa wengine wakikuta jeneza au kaburi liko tupu bila kuwepo dalili za mwili wowote.
Kuna pia kuhamisha makaburi ya muda mrefu ili kupisha shughuli nyingine,waliowahi kufanya hizi kazi wanajua fika walikutana na vituko gani
Maiti ambazo roho zake zilitoka kwa amani si kwa visasi si kwa vinyongo si kwa uchawi ushirikina wala mauaji au sababu nyingine yoyote ile mbaya hizi hazina neno kabisa...hii unaweza kulala nayo chumbani.
Tunapozungumzia vituko vya mochwari au makaburini kwa sehemu kubwa huletwa na maiti ambazo roho zake hazikutoka kwa amani na kabla ya muda (tumeambiwa umri wa mwanadamu ni miaka mingapi).
Kwahiyo ndugu zangu kuna baadhi ya mambo hayatakiwi kuchokonolewa kivile kwakuwa hata mkifanya nini marehemu hawezi kuwa hai tena.
Waliolala kuzimu wameshalala hakuna haja ya kwenda kuwasumbua tena kwakuwa kati yao hao roho zao huwa pembeni ya miili yao