Kufuatia matokeo ripoti ya makinikia

SUMUYANGE

Member
Apr 5, 2017
31
125
*SIASA CHAFU, UCHWARA, MAJITAKA NA WASOMI WENYE DEGREE FAKE NA FIKRA MGANDO KAMWE HAZITALIKOMBOA TAIFA*

BABA WA TAIFA ALISHASEMA, ILI TAIFA LIWEZE KUENDELEA LINAHITAJI MAMBO MANNE.

1.SIASA SAFI, msisitizo mkuu hapa ni siasa shirikishi yenye kujali na kuheshimu mawazo mbadala kutoka kwa wengine no michango mbalimbali juu ya mudtakhabali wa taifa.

2. WATU, msisitizo hapa ni kuwepo na watu wenye uchungu na ari ya maendeleo kwa taifa hili. Watu wazalendo wasio wabinafsi wanaowaza juu ya maslahi ya taifa, wasomi wenye fikra chanya wenye uwezo wa kuhoji na kushauri kwa kutoa mawazo mbadala juu ya mambo mbalimbali yahusio maendeleo ya taifa hili.

3. ARDHI kwa ajili shughuli mbalimbali za uchumi.

4. UTAWALA BORA. utawala unaozingatia utawala wa sheria, unaoheshimu utu, haki za binadamu, mawazo ya watu wengine, uhuru wa kujieleza na kufuatwa kwa katiba na sheria mbalimbali zilizotungwa juu ya mambo mbalimbali yahusiyo taifa letu.

Baada ya kueleza kidogo hayo hapo juu, naomba nijikite kwenye mjadala unaoendelea mtaani,kwenye vijiwe na kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii juu suala la makinikia.
KWANINI TUMEFIKA HAPA?????

Ukipitia mijadala mbalimbali kuna ukinzani wa mawazo, wengine wakiisifu serikali hasa jamaa wa ccm, ambao wamesahau kuwa chanzo cha haya yote ni serikali hii hii ambayo wanayoisifia, hili naweza kusema ni kukengeuka kwa makada hawa ambao hawaoni aibu kutokana na fikra dhaifu na uchama unaowasumbua kiasi cha kuwapinga wapinzani kwa zaidi ya miaka 20 sasa juu ya wizi huu wa madini ya watanzania.

Makada hawahawa waliojitoa ufahamu na kuishia kushangilia jambo kitu kilichopelekea kusainiwa kwa mikataba hewa ya kilaghai kwenye rasilimali zetu, kupitishwa kwa sheria kandamizi kwa lengo la kuwakomoa wapinzani, aibu yenu

Kwa tamaa zenu mmetuaibisha watz, mmewapuuza wapinzani na kupinga mawazo yao mchana kweupe kwa kujitoa ufahamu ili kukilinda chama chenu badala ya maslahi ya taifa.

Upande wa pili ambao kwa miaka zaidi ya 20 tulipiga kelele dhidi ya wizi huu uliobarikiwa na ccm tunasema ni too late.

Hivyo basi lawama zote juu ya wizi huu ccm mtaendelea kulaumiwa sasa na kizazi kijacho kwani tumefika hapa kwa sababu ya watu wenu mlioweka mbele maslahi binafsi ya matumbo yenu, kukandamiza na kuminya utawala wa kisheria, kuficha mikataba ya rasilimali zetu.

Ni dhahiri kabisa ccm ndio chanzo cha wizi huu na mnapaswa kuwaomba radhi watanzania.

Nini kifanyike???
----------------------------------
Kuwepo na utawala bora unaozingatia utawala wa sheria, unaoheshimu utu, haki za binadamu na uhuru wa kujieleza, unaoheshimu mawazo na maoni ya wengine, kuwepo uwazi ktk masuala mbalimbali ya kitaifa ili kuondoa figisu na ujanjaujanja wa kundi dogo lililojitwalia mamlaka ya kuendelea kunufaika na rasilimali zetu.

Wasomi wetu kuepuka kuwa madodoki ya wanasiasa, mnapaswa kutumia taaluma zenu kuhoji na kushauri, pamoja na kupinga kwa nguvu zote jambo lolote lile lisilokuwa na maslahi kwa walalahoi wa nchi hii, kujitokeza hadharani kukemea kila aina ya ukandamizaji na unyonyaji unaotekelezwa na kundi dogo lililojitwalia mamlaka ya kufaidi rasilimali zetu.

Kuepuka fikra dhaifu na mgando ya kujipendekeza kwa wakubwa kwa tamaa ya vyeo, laana hii itakutafuna wewe na kizazi chako.
Tuache siasa chafu zisizojenga taifa letu, tuendelee kujenga umoja na kuheshimiana sisi kwa sisi.

Vijana na makada wa lumumba mwache kujitoa ufahamu na kutumika vibaya kwa minajili ya kusaka vyeo, kwani vyeo vitapita, tuweke maslahi ya taifa mbele, wanyonge na walalahoi waliotuzaa na kutusomesha kwa tabu huko vijijini wanateseka kwa kukosa huduma bora za kijamii na hii imetokana na kasumba mbaya ya kushangilia na kuitikia ndiyoooo kwa kila kitu ili kumfurahisha fulani tutahukumiwa kwa hili

Mungu ibariki afrika
Mungu ibariki tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom