Kufuatia Madudu na Maroroso ya CHADEMA, Je, bado kuna imani na matumaini na CHADEMA kwa 2015?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,610
113,825
Wanabodi,

Kufuatia Chama cha Democrasia na Maendeleo, Chadema, kukumbwa na migogoro, mitafaruku na sintofamu kadhaa wa kadhaa za hapa na pale haswa kuhusiana na hatma ya timua timua kwa baadhi ya viongozi wake waandamizi na kuwafutia uanachama wao, katika hali iliyopelekea baadhi yao kushindwa kuvumilia dhulma, manyanyaso, na ukiukwaji mkubwa wa haki ndani ya Chadema na hivyo kuitafuta haki yao mahala stahiki pa kupatia hakiambao miongoni mwao, baadhi ya watu wameitafsiri hali hiyo kama ni madudu na maroroso, hivyo yameakatisha kabisa tamaa na matumaini na Chadema kuweza kutuletea ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania hapo 2015 na hivyo kuamua kuachana na rasmi na Chadema.

Inawezekana, miongoni mwao hawa waliokatishwa tamaa na Chadema ni yule Mfadhili Mkuu wa Wazi wa Chadema, Mzee Jaffer Sabodo, nae kuna uwezekano, amechoshwa na madudu na maroroso ya Chama cha Democrasia (jina ) na Maendeleo (ndoto), Chadema, sasa amehamishia majeshi yake chama cha NCCR Mageuzi kwa kuwadonolea kianzio cha Shilingi milioni 20?!.

Hayo yamethibitika asubuhi ya leo baada ya Mzee Sabodo, kuibukia NCCR Mageuzi, wakati wa mkutano wake mkuu.

Inawezekana, Mzee Sabodo ni just one-of, lakini Chadema ni ile ile, inapendwa vile vile, na hata baada ya kumtimua rasmi Zitto, hakutakuwa na any mass exodus ya washabiki na wafuasi wake kumfuata, bali watabakia loyal kwa Chadema as it is now!.

Au pia jee inawezekana Sabodo kawa muwazi tuu na mkweli mwenye guts, lakini kuna wengi waliopoteza imani na Chadema na wame/wata withdraw their support to Chadema, kimya kimya?!.

Vipi kwa upande wako, bado una imani na Chadema?!.


Wasaam

Pasco.
 
Chadema ndio msingiiiiii!!!!!! Peoples powerrrr.......


Najisikia kinyaa kujib post ya huyu mdini Pasco....
 
Kwani baada ya maroroso ya ccm sabodo akaenda kutoa msaada cdm je wanaccm walipoteza imani na ccm? Tuanzie hapo ndipo tuje kwa cdm.
 
Imani ndo imekuwa kubwa zaidi kwa sababu kimeonyesha ni chama serious kinachoweza kuchukua hatua hata kwa vigogo jambo ambalo CCM wanaishia kutishia tu na baadaye kubadili maneno. ...kinachoshangaza ni baadhi ya watu wanaimani na Lowasa pamoja na madudu na maroroso ya RICHMOND na DOWANS?
 
Pasco chadema hakuna hio kitu unayoita mgogoro..ni maamuzi rasmi ya kamati huo mgogoro labda unao wewe kichwani mwako...ukienda bank kukopa kwa masharti...ukaweka hati ya nyumba halafu ukashindwa ..bank watangaza kuuza nyumba wewe unakimbilia mahakamani ...jua ni usumbufu tu lazima mwisho wa siku nyumba itauzwa na wewe kupata hasara zaidi za kesi feki
 
Pasco,

Watakutukana tu hawa. Tutaelewana mwaka 2015 baada ya matokeo kutangazwa ndipo watagundua.

By the way kipimo cha karibu kabisa ni uchaguzi ujao wa madiwani katika Kata 27. Salama yetu ni kupata angalau madiwani 10. Chini ya hapo itakuwa aibu na dalili mbaya kwa mwaka 2015. Tayari huko Lushoto mgombea wa CCM amepita bila kupingwa kwa sababu ya kukosa umakini katika kuweka wagombea.

Kuna watu kibao wanajifanya CHADEMA kindakindaki kumbe CCM wakubwa, kama tulivyoona yule jamaa huko Lushoto alivyoingia mitini.

Na hapa JF kuna wapiga kelele kibao wakijifanya kushabikia CDM lakini mwakani baada ya matokeo utaona watakavyopotea. Ni swala la muda tu, tuombe uzima.
 
Last edited by a moderator:
ma ccm bwana mnajitahidi sana kuonyesha kuna mgogoro CHADEMA sasa wakati sabodo anakuwa tajiri wewe pasco na mafisadi wako wa Lumumba mlikuwepo?sasa iweje leo hii mmchagulie Sabodo nani wa kumpa pesa na nani asimpe,tunaludia teena ccm ni geenge la walaghai na nyinyi hilo mnalijua
 
Wanabodi,
...
Vipi kwa upande wako, bado una imani na Chadema?!.

Pasco.

Hii ni Kufuatia leo , Mzee Sabodo kuibukia kwenye Mkutano Mkuu wa NCCR Mageuzi.
Pasco,
Did they tell you that Mbowe also was in attendance?
 
hizi ndoto nyingine zinakera ingawa sijalazimishwa kusoma

jk anajuwa hilo ndio maana kawaambia msitegemee police....mjiandae kisaikologia upo.....au jk pia humuamini....au yule wapigwe tu sie tumechoka
 
Back
Top Bottom