Kufosi kuishi kizungu kwa shotcut za kibongo, Nina rundo la muvi/miziki/pdf za kudownload, kuna usalama wa online backup au nitunze kwenye external ?

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
258
745
Wabongo wengi tunapenda sana vya bure kwenye ulimwengu wa kidijitali, ni mwendo wa kudownload muvi / games / series / miziki / vitabu / software / window , n.k. nakumbuka hata nikiwa chuoni maktaba ilituandalia vipeperushi vya tovuti za kudownload vitabu bure, pia mwalimu wetu wa somo la computer alitufundisha kudownload muvi bure.

Ila kwa kupenda kuishi kizungu nako hatupo nyuma, wabongo wengi hasa wadau wa tech ukiwaomba ushauri kwenye mambo ya kidijitali watakushauri kimbele mbele yani.

kwenye suala la backups hata humu nimekutana na baadhi ya wadau wakishauri tutumie online backups kama wenzetu wa mbele, wakikazia mambo ya external yamepitwa.

Je kuna usalama wa kufanya backups online ?

Yes, nina unlimited internet
 
Usalama upo ndio.. kama unavyodownload movie bure sema unapata storage kdgo..
Usalama upo wapi wakati nchi za marekani na ulaya ukikutwa na muvi / mziki / kitabu / game ya kudownload ni kosa la jinai ?

Makampuni ya online backups ya huko wataruhusu vp utunze vitu vya kudownload ?
 
Usalama upo wapi wakati nchi za marekani na ulaya ukikutwa na muvi / mziki / kitabu / game ya kudownload ni kosa la jinai ?

Makampuni ya online backups ya huko wataruhusu vp utunze vitu vya kudownload ?
Kushare vitu ndio illegal, ila uki upload kitu chako personal hakuna mwenye muda na wewe.

Huko Ulaya kuna watu wananunua CD wana rip na ku upload online kama backup ya movie zao bila tatizo lolote kisheria.
 
Usalama sio tatizo tatizo ni gharama ya kuhifadhi online na bandwidth, online nakushauri hifadhi vitu ambavyo ni muhimu sana na sio rahisi kuvipata ukipoteza, documents zako, picha, video zako etc.


Hakuna haja ya kufanya online backup ya movie ni kupoteza hiyo storage na data, hata kama una unlimited inachukua muda sana ukishaanza kuingia kwenye TB za data, weka kwenye HD ikifa download upya, kama vipi weka hata copy kwenye HD mbili yofauti.
 
Nimesahau pia unaweza kuchoma kwenye DVD au hata blueray ila kumbuka disk nazo zinaoza baada ya muda fulani. HD pia zina kikomo cha maisha hasa isipotumika.
 
Tatizo la cloud storage ni gharama juu ya gharama.
Kupakia unahitaji gharama za internet.
Kupakua unahitaji gharama za internet.
Storage capacity Kubwa unahitaji gharama.

Lol! Mi naoma Hard drive ni affordable Kuliko cloud storage, japokuwa kila kitu kina faida na hasara.
 
Back
Top Bottom