Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Kufilisika kisiasa kwingine kunatisha!

Nape Nnauye

MP Mtama
Joined
Dec 26, 2012
Posts
99
Reaction score
408
Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la CHADEMA la Tanzania Daima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu.

Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya Tanzania Daima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la CHADEMA limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la CHADEMA leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda.

WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.

================================
Habari kamili toka Tanzania Daima
================================

Kinana amkacha Dr. Slaa

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amemkacha Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Wawili hao walitarajiwa kukutana kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uzalendo', kinachotarajiwa kuanza kurushwa wakati wowote kuanzia mwezi ujao katika kituo cha televisheni cha ITV.

Taarifa za Kinana kumkimbia Dk. Slaa katika mdahalo huo zilisambazwa jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Taarifa hiyo na vyanzo vyetu vingine vya habari, vilieleza kuwa viongozi hao walialikwa na ITV kwa ajili ya mdahalo ambao ungerekodiwa na baadaye kurushwa na kituo hicho.

Kwa mujibu wa habari hizo, viongozi hao walipewa mwaliko wa kuhudhuria kipindi hicho siku kumi zilizopita na wote kuthibitisha ushiriki wao, lakini Dk. Slaa jana alifika katika studio za kituo hicho na kukutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, badala ya Kinana.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Dk. Slaa alisema: "Ni kweli tulikuwa tumealikwa kwenye mdahalo pale ITV (leo) jana saa 3, nilipofika nilikutana na Nape, nikamsalimu nikajua kuwa alikuwa amemsindikiza Kinana, lakini nilipomuuliza mwendesha kipindi kwamba Kinana yuko wapi, alisema amepata udhuru hivyo hajafika.

"Nilimwambia Nape wewe si saizi yangu, sitaweza kuongea katika kipindi hiki kama Kinana hayupo, hivyo kipindi hiki kiahirishwe hadi Kinana atakapokuwa na nafasi ya kuja," alisema Dk. Slaa.

"Haiwezekani mwenzangu akaahirisha ghafla kuja kwenye kipindui halafu nisipewe taarifa na badala yake nikatumiwa Nape, Nape si saizi yangu," alisisitiza Dk. Slaa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa baada ya kuahirishwa kipindi hicho, Nape na Dk. Slaa walisalimiana na kuagana. "Naamini siasa si uadui, niliongea na Nape nikamuuliza Kinana yuko wapi, alisema alikuwa amepata udhuru, akanipigia simu nije," alisema.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, Nape alisema alikwenda ITV badala ya Kinana, kuangalia maudhui ya kipindi hicho ili aweze kushauriana na Kinana na kuamua kuja au la.

"Mimi ndiyo msemaji wa chama, katibu mkuu hawezi kualikwa mimi nisiwe na taarifa, mimi ndiyo napaswa kwenda na nilikwenda nilipokutana na Dk. Slaa tukaelezwa, Dk. Slaa alishauri kuwa inafaa kualika watu wenye hadhi zinazofanana, yaani makatibu, hivyo mimi niliondoka nikamwacha Dk. Slaa, nadhani alirekodiwa kwa kuwa walisema wanaweza kurekodi mtu mmoja mmoja na katibu mkuu wetu anaweza kwenda siku nyingine kurekodi," alisema Nape.

Kinana mwenyewe alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo, hakuweza kupatikana kwani simu yake iliita bila kupokewa.
 
Hamocha😛amoja na sintofahamu ya historia yako,bado mm naamini wewe ni "mnyampaa".Viti yule mla fisi(mnyiramba,mtani) yupo au kapeleka ushahidi mbinguni? msalimie
 
KWANI WEWE NI KATIBU MKUU WA CCM??ILIKUWAJE UKAENDA ITV???ULITAKA KUTENGENEZA STORY JANA KUWA UMEKIMBIWA NA DR.W.P.SLAA KWA BAHATI MBAYA WATU WAKASHITUKIA HATA VUTA N KUVUTE KASEMA JANA ULIPIGA SIMU LUMUMBA KUWA HII STORY NDIO IUZE FRONT PAGES WAKAKUKATALIA SASA USIBWEKE NANI KAFILISIKA KISIASA NCHI HII KAMA CCM????HALA CHADEMA GOD BLESS CHADEMA ILE PROPAGANDA YAKO YAKO YA CHADEMA CHAMA CHA KIGAIDI ILIISHIA WAPI Nape Nnauye,???
 
Nape ameshindwa kurithi busara za baba yake......Ungekuwa kama baba yako ungeheshimiwa sana ila kwa sasa naona unapuliza tu vuvuzela kila kukicha....ama kweli moto huzaa majivu
 
Sioni mantiki kwenye hii story. Sasa aliyefilisika kisiasa ni nani? Dr. Slaa au gazeti la Tanzania Daima? Maana unaonekana unalishangaa gazeti la Tanzania daima, kwa kuipa uzito hiyo story na unalifananisha na Uhuru. Lakini title unaongelea kufilisika kisiasa! Hivi gazeti nalo lina nguvu za kisiasa?

Umesema Tandaleone (ambaye ni wewe mwenyewe) alikuwa anafanya propaganda, unataka kusema kwamba hiyo story haina ukweli? Hapa unataka kukanusha hiyo story au nia yako ni nini? Jitahidi kuwa na clear focus, unapoandika story zako.

Kwa level ya katibu mwenezi tungependa ufanye vizuri kuliko hivi. Kama unashindwa kutengeneza column nzuri yenye maelezo mazuri ya kukijenga na kukilinda chama chako, unawezaje kujivuna kwamba ungeweza kusimama na Dr. Slaa kwenye mdahalo?
 
Kwa mazoea yako ya kumwita BABU DR Slaa ndio maana alisepa, naamini alifikiri ungeenda zaidi ya hapo. Bora Kinana huwa anaongea kwa staha na kwa heshima.
 
Unataka kumaanisha nini? Maelezo ni mengi lakini hayana mpangilio unaotiririka ili uweze kueleweka. Jipange sawasawa.
 

Huyu jamaa ni mkurupukaji sana......kama kipindi "kinadaiwa" kuandaliwa hapa alikuwa anafanya nini hiyo jana? Hukohuko ITV?

213767641.jpg
 
Mbona Nape anashindwa kujibu hoja.Mimi nasikitishwa na kauli za Nape lazima ziwe na kejeri, kwa sisi wasomi mtu hata kama humpendi vipi lazima uheshimu elimu yaka.Kama ni Dr utamuita Dr kama ni professor Utamuita ivyo.Kwa kauli kama hizo za Nape mimi napata mashaka na vyeo mnavyopewa.Nikiangalia naona ni siasa za chuki tu.
 
Tandale one ulivyoleta mada hapa ya jana ya kumshusha hadhi Dr slaa hukujua madhara yake sasa the whole naton knows your vindict attitude sorry Nape
 
Naomba hiyo single yenu ya ugaidi muachane nayo. Wachochezi wakubwa mnaogawa watanzania ili wasiungane kuwang'oa. Hamkawii kukataa kuwa nyie siyo waanzilishi wa choko choko. Hasara iliyopata nchi hii kuongozwa na ccm kamwe haiwezi kufidiwa. Acheni demokrasia istawi.
 
Toka jana nimekuwa nikisoma kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu hoja ya " NAPE, KINANA NA DR. SLAA" juu ya kipindi kilichodaiwa kuandaliwa na ITV. Leo kwa uzito mkubwa stori hiyo imebebwa na gazeti la Chadema la TanzaniaDaima. Kwa gazeti hili ni stori inayouza gazeti lao leo.

Niseme toka jana niliposoma propaganda ya Tandaleone nilishangaa lakini nikajipa muda kujua msingi wa propaganda ile. Baada ya muda nikaona majibu ya Babu Dr. Slaa nikayashangaa pia japo si sana, bado niajipa muda. Jioni nikapigiwa simu na mwandishi wa TanzaniaDaima kuulizwa juu ya hiyo stori, nikasema wameanza sasa kuja hadharani na makusudi yao naanza kuyafahamu. Pamoja na kujitahidi kueleza kilichotokea bado matokeo ni Lead Stori ya TanzaniaDaima leo inayodai eti Kinana kamkimbia kiaina Babu Dr.Slaa!!!! Raafiki yangu mmoja asub alipoona gazeti la Chadema limeandika vile akanitania akasema nilitegemea UHURU waandike "KINANA AMPUUZA BABU DR. SLAA" nikamwambia UHURU linafanya kazi ya nchi si ya Chama pekeake ndo maana limekuwepo hata kabla ya CCM kuwepo!!

Lakini ninachotaka kusema hapa ni propaganda kama za Gazeti la Chadema leo ni dalili za kufilisika sana kisiasa kiasi kwamba hhata jambo dogo sana linageuzwa kuwa jambo kubwa na linalodhaniwa linaweza kutumika kipropaganda. WASWAHILI WALISEMA kwa sisimizi hata kifuu cha nazi kwake ni sawa na bahari!Pengine tungemsaidia sana mwajiri kwa kumfanyia utafiti kwanini ofisi za wilayani na mikoani za taasisi anayoiongoza zinafungwa kwa kasi ya ajabu.

pole sana VUVUZELA NAPE.Kwa taarifa yako ungekuwa na maadili tu ungekula sana mema ya hii nchi...Lakini kwa kuwa heshima na adabu vimekupita pembeni bado una mlima wa kupanda si kwa sisi vijana wenzako na marika mengine yote....Heshima hainunuliwi baba.Wewe na ujana wako nakuuliza SLAA NI BABU YAKO?!!.jifunze kuwa na adabu...KWA WAKUBWA ZAKO.

mwana mwenye heshima na adabu ni mzigo wa babaye lakini kama hayo ni mzigo wa mamaye....

nakushauri.

1.mtafute mama yako akufundishe adabu.
2.Siasa ni siasa na utu ni utu ,mpe heshima SLAA na siyo kumuita babu.
3.Fuata maadili ya kazi yako.
4.Kuwa na mipakaya kazi yako au wewe ndo kinana?
5.Epuka cheap popularity.
6.Jitathimini kisiasa.
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...

Acha kubwatuka wee ZeMarcopolo kiongozi wa wajinga wa lumumba....mbona gaziti la uhuru liliwahi kunakili taarifa ya Lema iliyotolewa kwenye blog ya yule mwanamke mjinga wa UK anayemchafua Lema kila kukicha akiwa uingereza kwa kili lilichoda kuwa "CHADEMA yaumbuka Uingereza" na kuifanya kuwa stori ya kuuza gazeti?????hapa nani mdaku kati ya anayenakili habari kutoka kwenye blog bili kuifanyia utafiti na anayefanya utafiti???
 
Nape huna hadhi ya kufanya mjadala wowote na Dr Slaa hata Kinana mwenyewe pia hana hadhi hiyo kumbuka Slaa huyo unaemtukana kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya ccm NEC alipata kura million 2.8 wewe na Kinana mna kura ngapi japo za kuibiwa tu. IQ yako ina tatizo kubwa sana.
 
Back
Top Bottom