Kufikiri kwetu vibaya na mustakabali wa afya zetu………..!

Napajua hapo mahali wanapolima maharage katika eneo hilo la KIA, hata sisi tuliwahi kukodisha shamba katika eneo hilo, nadhani panaitwa MATIBA au MAKIBA, kama sikosei............

Je sasa unadhani kilichimuua huyo mzee ni mazao kukauka au mkopo wa benki?

wakati mwingine ukijifunza si lazima uchangie mimi nipo kupokea elimu zaidi hapa yakinikaa nitakuja kivingine na kuchangia once again thanks niko kielimu zaidi pata mengi kwako karibu kwa mengine zaidi
 
Kwa tulivyoumbwa binadamu mioyo yetu imekaa na alwayz huwa inajiandaa kupokea habari nzuri na zile ambazo tunazipenda. Ni vigumu sana kiakili na kimwili kubaki in normal situation pale ambapo unapata habari usiyoipenda.

Any wayz kitu ninachoweza kujifunza hapa ni kwamba kila jambo lina pande nyingi..every problem has opportunities in it!!

And thats whassup!
 
Kila penye shari kuna heri ndani yake. Thanx sana mtambuzi, mi pia namshukuru mungu si mtu wa kuyafikiri sana matukio mabaya kiasi cha kunifanya niumie. Naamini unapokuwa katika wakati mgumu sana ujue neema imekaribia. Najipa moyo kinamna hiyo na maisha yanasonga.
 
[
ukiwa kijana hizi theory zina maana ila kadiri unavyozeeka hizi theory huziwezi.

Kwa mtu wa miaka 45+ kupoteza nyumba ni msiba kabisa kuliko kijana wa miaka 26 kupoteza nyumba hiyo hiyo.

Maumivu huwa makubwa kulingana na nguvu uliyotumia kupata nyumba hiyo, imagine at my age nipotze nyumba sasa si nitarukwa akili?? Ila nilipokuwa kijana ningeweza vumilia au kuchukulia positively.

Mtambuzi, nashukuru tunaamini kwenye kitu kimoja mshua. Nimefiwa na watu wa karibu sana watatu. Wa kwanza 20 years ago, so u can imagine umri ulikuwa mdogo. Lakini hata the last one (few weeks ago) still nahisi I behaved the same. Wakati wa kuuguza huwa nalia na kuchanganyikiwa. Lakini akishafariki ni wakati wa ku-focus kwenye mambo ya msingi. To be composed is possible bwana!
 
Last edited by a moderator:
Kongosho bana.............
Awali uli-comment vizuri, lakini sasa unaharibu..........................
Ni vyema tukajifunzxa kwamba kamwe hatuwezi kushindana na hali halisi, kama nyumba inaungua hatuwezi kubadili hali hiyo, kikubwa ni usalama wa afya zetu na afya za wale waliotuzunguka, kuumia kihisia au kulia sana kamwe hakuwezi kubadili hali hiyo. Jambo muhimu hapo ni kuangalia maisha yatakuwaje baada ya hapo na si kuendelea kujuta na kujilaumu au hata kumtafuta mchawi. Hatuwezi kubadili jambo ambalo limekwishatokea ni sawa na kufanya juhudi kubwa kujaribu kufufua mzoga..........................

Kiongozi, hapa naunga mkono hoja!
 
King'asti, Mtambuzi na HorsePower

Nachojaribu kusema ni kuwa, ukipotelewa na kitu huwezi chukulia positive from initial point
Lazima taharuki itakuwepo tu, but at time t=x ndio utaanza kuona reasons na kukubali matokeo.

Labda tunachopishana ni t gani.

Kila mtu anapenda t=x, but x-->0 not x-->infinity

Ndio maana King'asti umesema wazi wakati wa kuuguliwa huwa unalia, that means hiyo ni taharuki hadi kufikia msiba time yako ya kuheal na kukubali matokeo inakuwa ishafika.

Lakini kusema utabasamu kwa tatizo from t = 0???
 
Last edited by a moderator:
Foto-de-Thomas-Edson-LUZ-Loja-de-Consultoria.jpg

Labda niwape kisa kingine ambacho ni maarufu sana. Kuna bwana mmoja ambaye anajulikana kama ni bingwa wa kutokata tamaa naye si mwingine bali ni mgunduzi wa balbu hii ya umeme, bwana Thomas Edison. Labda kwa kifupi kwa wale wasiomjua Thomas Edison, huyu jamaa alifanya majaribio 1000, wakati akiwa katika mchakato wa kugundua Balbu. Ingawa wakati mwingine watu wanatofautiana ki takwimu katika kuelezea habari zake, lakini mimi kitabu nilichosoma kinasema alifanya majaribio 1000 ya kutengeneza balbu ndipo akafanikiwa kuwasha hii balbu ya umeme tunayotumia,

Hebu fikiria majaribio 1000 ndio ufanikiwe, ajabu ee!!

Lakini pia katika majaribio hayo alikuwa anapata vikwazo kadhaa, mojawapo ya tukio kubwa ni lile la maabara yake kuungua na hivyo kupoteza mafaili yake yote ya kumbukumbu za ugunduzi wake. Cha kushangaza wakati anaangalia yale majivu ya makabrasha yake aliwaambia wasaidizi wake kuwa imekuwa vyema yale mafaili yaliyohifadhi kumbukumbu za majaribio yake yaliyoshindwa yameungua kwa hiyo hakuna haja ya kuhangaika na majaribio yaliyoshindwa na badala yake waanze upya.

Si hivyo tu bali alikiri kwamba katika majaribio hayo pia amejifunza kushindwa!
Baadae ndipo wakafanikiwa kuwasha balbu.

Je umeona jinsi mtu huyu alivyo na akili za ajabu?

Hivi ni mara ngapi sisi tunakwama katika shughuli zetu na kujipongeza japo kwa kushindwa kwetu?

Rafiki yangu SnowBall amezungumzia kitu kinachoitwa Dialectic Thinking. Amesema kila jambo lina pande mbili, kwa mfano kama kuna kushinda basi kuna kushindwa, na kama kuna kupata, kuna kukosa pia.
Mifano iko mingi sana.

Lakini swali la msingi hapa ni, je tumefundishwa nini kuhusiana na hizi pande mbili?

Je ni kweli kuna upande mbaya na mzuri?

Ni nani aliyekufundsha hivyo?

Ukweli ni kwamba hakuna upande mbaya katika kila jambo, bali tafsiri zetu ndizo zinazotupotosha. Kufanikiwa na kutokufanikiwa kwa jambo lolote ni mojawapo ya changamoto za kujifunza. Tunaweza kujifunza kutokana na kufanikiwa na pia tunaweza kujifunza kutokana na kutofanikiwa.................


Mtambuzi check your facts, Huyu jamaa siyo kweli kwamba ndiye mgunduzi wa balbu ila ana mchango wake kiasi fulani.
 
Kongosho katika mambo ambayo nimejifunza na ninashukuru nimemudu, ni kutoumizwa na tukio lolote linaloitwa baya. kwanza mimi siamini kama kuna tukio baya, ninachofanya ni kuyapokea matukio yote yawe mabaya au mazuri na kuangalia namna gani nitajifunza kutokana na tukio hilo.........
kama umesoma vizuri posti yangu utagundua kwmaba kinachotuumiza wengi ni namna tunavyotafsiri matukio yanayotutokea na ndio sababu yanatuumiza.

Kama tukiyapokea matukio kwa namna ya kujifunza, mara nyingi huwa washindi, lakini tukibaki kujuta, na kuomboleza maisha yetu yatakuwa ya ajabu sana na afya zetu zitakuwa nyondenyonde na kuna uwezekano wa kupoteza maisha....

Kama hauumizwi na matukio mabaya ni kwa sababu tu threshold yako inaweza kuwa juu kiasi fulani kuliko watu wengine ambao tunaweza kuwaita ni wa kawaida. Kwa mfano watu wote walio katika hali ya kawaida wanaweza kupata maumivu ya mwili na kupiga makelele lakini kila mtu ana kiwango fulani cha maumivu anachoweza kuvumilia kabla ya kuanza kupiga kelele. Hata hivyo hakuna binadamu anayeweza kuvumilia maumivu ya viwango vyote bila kupiga kelele.

Kwa hiyo utaona kuwa hata kwa upande wake kama matukio hayakuumizi ni kwa kuwa bado hayajavuka threshold yako, otherwise trust me yakivuka hiyo pointi utaumia tu.
 
Back
Top Bottom