Kufikiri kwetu vibaya na mustakabali wa afya zetu………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kufikiri kwetu vibaya na mustakabali wa afya zetu………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 12, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Leo nina kisa nataka kuwasimulia.

  Bwana mmoja alikuwa amekwenda kazini kama ilivyo kawaida yake, akiwa ndio anafika kazini akapigiwa simu kujulishwa kwamba nyumba yake inaungua. Bwana yule akarudi nyumabni haraka huku akijaribu kuwasiliana na watu wa zima moto. Alipofika nyumbani akaikuta nyumba yake ndio inazidi kuteketea kwa moto na hakuna kilichosalimishwa hata kitu kimoja na askari wa zima moto walikuwa hawajafika katika eneo la tukio.

  Basi yule bwana akawa amesimama akishuhudia nyumba yake ikiteketea asijue la kufanya. Ulikuwa ni msiba mkubwa sana kwake, kwani ile nyumba ilikuwa ni kubwa na ilimgharimu kiasi kikubwa cha fedha. Wakati akiwa bado amesimama pale nje akiwa anashuhudia lile tukio, mwanae mmoja wa kiume alimsogelea na kumshika bega, kisha akamwambia "usijali nilishaiuza tangu jana!, nilikusikia wewe na mama mkilalamika kuwa hii nyumba ni kubwa sana na mlikuwa hamuihitaji tena, nikakutana na tajiri mmoja mwekezaji toka nje ambaye alikubali kuinunua kwa gharama yoyote"

  Ghafla sura ya baba yake ikagubikwa na tabasamu la furaha na kumkumbatia mwanae na kumpongeza kwa kwa uamuzi mzuri alioufanya. Mpaka hapo hakuna kilichobadilika: Nyumba ilikuwa bado inaungua lakini hakuwa mmiliki wa nyumba ile tena. Kwa nini ajali, wakati haimuhusu? Wakati baba akiendelea kumpongeza mwanaye huyo, mwanaye mwingine mdogo wa kiume aliwasogelea uso wake ukiwa umegubikwa na huzuni, Baba alimwangalia mwanaye kwa mshtuko, "nini tena?" Baba aliuliza kwa wasiwasi.

  "Ni kweli mwekezaji mmoja alikuwa anataka kuinunua hii nyumba"
  yule kijana alisema, akimwambia baba yake. "Lakini mkataba wa mauzo ulikuwa bado kusainiwa na pande mbili, kwa hiyo hatuna cha kuuza."
  Yule baba aliishiwa na nguvu kabisa, na kukaa chini, mwili wote ulikufa ganzi na hakuwa na la kusema, akabaki kuwaangalia wale wanaye asiamini masikio yake. Bado hakuna kilichobadilika: Nyumba bado ilikuwa inaungua. Kilichobadilika ni taarifa tu. Wakati nyumba yake inaungua aligubikwa na huzuni. Alipopata taarifa kuwa nyumba ilishauzwa kwa mtu mwingine, ingawa bado ilikuwa inaungua alifurahi sana kwa sababu haikuwa yake tena.
  [​IMG]
  Zilipokuja taarifa nyingine toka kwa mwanae mdogo kuwa mkataba wa mauzo ulikuwa bado haujasainiwa, baba akataharuki na kurudi kwenye majonzi tena kwa sababu kumbe nyumba bado iko mikononi mwake. Akiwa bado amegubikwa na simanzi, aliyekuwa mnunuzi wa ile nyumba alifika, "najua hii ni bahati mbaya sana kwako, kwa nyumba yako kuungua, hata hivyo nilikuwa nahitaji hii ardhi tu, kwa hiyo nitalipa kiasi kile kile cha fedha tulichopatana"

  Kusikia hivyo, uso wa yule baba, ukabadilika tena na kugubikwa na furaha kubwa isiyo kifani, kwani nyumba haikuwa mikononi mwake tena, hakuna haja kusikitika. Naamini mpaka hapo mmeona mwili unavyopata mabadiliko kulingana na jinsi tunavyotafsiri matukio tunatoyapata. Ikiwa tutatafsiri tukio vibaya kwa kuangalia upande mmoja wa hasi, ni wazi tutapata maumivu ya kihisia. Kwa mfano wa tukio hili la nyumba kuungua, awali yule mzee alikuwa analalamika kuwa ile nyumba haihitaji tena, kwa kuwa ni kubwa na labda ilikuwa ina muundo wa kizamani, kwa hiyo hakuipenda. Alikuwa anatamani kujenga nyumba mpya ambayo ndiyo aliyokuwa akiihitaji.

  Niliwahi kuandika kuhusu jinsi mawazo yalivyo na nguvu, kwamba kile tunachofikiri ndicho kinachofanyiwa kazi na akili ya kina (unconscious mind), kwa hiyo, tukio lile ilikuwa ni matokeo ya kile alichokuwa anafikiri. Lakini kwa bahati mbaya matokeo ya fikra zetu hayaji kwa namna tunavyotaka, yanakuja kwa njia ya ajabu mno ambayo mwenye werevu wa kihisia pekee ndiye atakayeweza kung'amua. Akili ya kina huwa haileti majibu yakiwa yamevaa suti, mara nyingi yanakuwa na sura isiyovutia na yenye kutia kinyaa, usipoigundua, umekwisha.

  Maswali ya kujiuliza:

  Hivi kama yule mzee angekuwa na ugonjwa wa moyo, hudhani kama angekufa kutokana na mshtuko wa kuunguliwa na nyumba?

  Je ni mara ngapi tunapiga teke yale mambo yanayofanyiwa kazi na akili ya kina na kuja mbele yetu yakiwa na sura kama hii?

  Je hofu na maumivu ya kihisia tunayopata ni kutokana na tukio au tafsiri inayokwenda akilini kwetu?

  Je umejifunza nini juu ya kisa hiki?
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  nimejifunza nifurahie nyumba ikiungua ili nisiumie kihisia.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Nilijifunza kitambo kuchagua vita vya kupigana. Namaanisha prioritisation. Material things (kazi, fedha, nyumba na magari) ni vitu vya kupita. Vinaweza kuja kwa wingi maishani ukajikuta unasahau vya msingi, just to come back to your senses when it is too late nyakati zingine.

  Afya (ya mwili, akili na roho) ndio priority. Kwenye nyumba inayoungua cha kuulizia ni kama wanaoishi wote wametoka salama, that is all that matters! Ofcoz unarudishwa nyuma lakini sio sawa na kuvurugikwa kwa kufiwa say, na wanao wote. Na huwezi kujua Mungu atakuinuaje.

  Positivism theorem ndo mpango mzima.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  ukiwa kijana hizi theory zina maana ila kadiri unavyozeeka hizi theory huziwezi.

  Kwa mtu wa miaka 45+ kupoteza nyumba ni msiba kabisa kuliko kijana wa miaka 26 kupoteza nyumba hiyo hiyo.

  Maumivu huwa makubwa kulingana na nguvu uliyotumia kupata nyumba hiyo, imagine at my age nipotze nyumba sasa si nitarukwa akili?? Ila nilipokuwa kijana ningeweza vumilia au kuchukulia positively.

   
 5. CRISTA

  CRISTA Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Si kila kitu ufikilicho au uwazacho ni cha kweli u need to be carefully;
   
 6. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kwa tulivyoumbwa binadamu mioyo yetu imekaa na alwayz huwa inajiandaa kupokea habari nzuri na zile ambazo tunazipenda. Ni vigumu sana kiakili na kimwili kubaki in normal situation pale ambapo unapata habari usiyoipenda.

  Any wayz kitu ninachoweza kujifunza hapa ni kwamba kila jambo lina pande nyingi..every problem has opportunities in it!!
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ulichoandika na hasa hapo kwenye bold kinanifanya hata nisipoteze muda kubishana na wewe............ kwanza inadhihirisha kiwango chako cha maarifa ni kidogo, pili uwezo wako wa kusoma jambo na kutafakari ni mdogo, lakini pia hata uwezo wa akili yako katika kupambanua mambo ni wa kutiliwa shaka..................!

  Ahsante kwa kunifundisha neno jipya la kiswahili ..................... "ufikiliacho" LOL
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kongosho bana.............
  Awali uli-comment vizuri, lakini sasa unaharibu..........................
  Ni vyema tukajifunzxa kwamba kamwe hatuwezi kushindana na hali halisi, kama nyumba inaungua hatuwezi kubadili hali hiyo, kikubwa ni usalama wa afya zetu na afya za wale waliotuzunguka, kuumia kihisia au kulia sana kamwe hakuwezi kubadili hali hiyo. Jambo muhimu hapo ni kuangalia maisha yatakuwaje baada ya hapo na si kuendelea kujuta na kujilaumu au hata kumtafuta mchawi. Hatuwezi kubadili jambo ambalo limekwishatokea ni sawa na kufanya juhudi kubwa kujaribu kufufua mzoga..........................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  Mzee Mtambuzi wewe ni mwanasaikolojia nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Mtambuzi, nyumba yako ikiungua kuumia ni lazima.
  Sema muhimu ni kuangalia unaumia kwa muda na kiwango gani?

  Haiwezi nyumba iko inateketea mbele yako afu uwe na tabasamu usoni?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Labda niwape kisa kingine ambacho ni maarufu sana. Kuna bwana mmoja ambaye anajulikana kama ni bingwa wa kutokata tamaa naye si mwingine bali ni mgunduzi wa balbu hii ya umeme, bwana Thomas Edison. Labda kwa kifupi kwa wale wasiomjua Thomas Edison, huyu jamaa alifanya majaribio 1000, wakati akiwa katika mchakato wa kugundua Balbu. Ingawa wakati mwingine watu wanatofautiana ki takwimu katika kuelezea habari zake, lakini mimi kitabu nilichosoma kinasema alifanya majaribio 1000 ya kutengeneza balbu ndipo akafanikiwa kuwasha hii balbu ya umeme tunayotumia,

  Hebu fikiria majaribio 1000 ndio ufanikiwe, ajabu ee!!

  Lakini pia katika majaribio hayo alikuwa anapata vikwazo kadhaa, mojawapo ya tukio kubwa ni lile la maabara yake kuungua na hivyo kupoteza mafaili yake yote ya kumbukumbu za ugunduzi wake. Cha kushangaza wakati anaangalia yale majivu ya makabrasha yake aliwaambia wasaidizi wake kuwa imekuwa vyema yale mafaili yaliyohifadhi kumbukumbu za majaribio yake yaliyoshindwa yameungua kwa hiyo hakuna haja ya kuhangaika na majaribio yaliyoshindwa na badala yake waanze upya.

  Si hivyo tu bali alikiri kwamba katika majaribio hayo pia amejifunza kushindwa!
  Baadae ndipo wakafanikiwa kuwasha balbu.

  Je umeona jinsi mtu huyu alivyo na akili za ajabu?

  Hivi ni mara ngapi sisi tunakwama katika shughuli zetu na kujipongeza japo kwa kushindwa kwetu?

  Rafiki yangu SnowBall amezungumzia kitu kinachoitwa Dialectic Thinking. Amesema kila jambo lina pande mbili, kwa mfano kama kuna kushinda basi kuna kushindwa, na kama kuna kupata, kuna kukosa pia.
  Mifano iko mingi sana.

  Lakini swali la msingi hapa ni, je tumefundishwa nini kuhusiana na hizi pande mbili?

  Je ni kweli kuna upande mbaya na mzuri?

  Ni nani aliyekufundsha hivyo?

  Ukweli ni kwamba hakuna upande mbaya katika kila jambo, bali tafsiri zetu ndizo zinazotupotosha. Kufanikiwa na kutokufanikiwa kwa jambo lolote ni mojawapo ya changamoto za kujifunza. Tunaweza kujifunza kutokana na kufanikiwa na pia tunaweza kujifunza kutokana na kutofanikiwa.................

   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kongosho katika mambo ambayo nimejifunza na ninashukuru nimemudu, ni kutoumizwa na tukio lolote linaloitwa baya. kwanza mimi siamini kama kuna tukio baya, ninachofanya ni kuyapokea matukio yote yawe mabaya au mazuri na kuangalia namna gani nitajifunza kutokana na tukio hilo.........
  kama umesoma vizuri posti yangu utagundua kwmaba kinachotuumiza wengi ni namna tunavyotafsiri matukio yanayotutokea na ndio sababu yanatuumiza.

  Kama tukiyapokea matukio kwa namna ya kujifunza, mara nyingi huwa washindi, lakini tukibaki kujuta, na kuomboleza maisha yetu yatakuwa ya ajabu sana na afya zetu zitakuwa nyondenyonde na kuna uwezekano wa kupoteza maisha....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu Young Master mimi sio mwanasaikolojia, bali nimejifunza kuondokana na kuishi kimazoea...................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Cathode Rays

  Cathode Rays JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,736
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mtambuzi

  umenikumbusha jambo moja lililonisaidia kubaldilika hisia zangu mara baada ya kuumizwa na jambo....

  Niliwahi kumpenda binti sana then katika hatua ambazo najiandaa kumuoa alinizunguka na kuanguka katika uhusiano na mtu mwingine kiasi cha kwua mja mzito. Nilimpenda sana na kwa sababu hii niliumia sana huku nikihisi mengi sana jambo ambalo lilizidisha kuumia zaidi ya kusaidika...

  Wakati fulani nilijiuliza, hivi kuumia huku kunaweza kubadilisha scenario nzima? Je yule ambae ananifanya mimi niumie yuko kwenye hali gani? Nae anaumia kama mimi au anakula raha wakati mimi naumia?

  From this moment I tried to collect up myself na toka wakati huo nilijifunza when a tragedy happen, if it is well beyond your control, kuziachia hisia zako kuumia wont control anything zaidi utakuwa unajiumiza mwenyewe....AND THAT IS WHERE THE SECRET OF "THE POWER OF LETTING IT GO" LIES, kwenye kila tragedy inayotutokea........Kuumia kwa huyu mzee in any way kusingeirudisha nyumba, better to accept and face the future
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kuandika hapa wakati fulani katika mfululizo wa topic zangu kwamba kamwe hatuwezi kubalidi jambo lolote lililo nje yetu, bali tuna uwezo mkubwa sana kubadili jambo lililo ndani yetu.... Hii ina maana gani, ni kwamba, sisi tuna uwezo wa kuamua ni namna gani tuyapokee matukio yanayotujia maishani mwetu, lakini hatuna uwezo wa kuwapangia wengine waishi namna gani au wayapokee vipi matutukio yanayowatokea....... Ninachofanya hapa ni kueleza uzoefu wangu na silazimishi kila mtu akubaliane na kile ninachokisema.
  Ukweli ni kwamba hatuna uwezo wa kumbadilisha mtu, labda aamue mwenyewe, lakini kama hataki, itakuwa ni kazi bure. Na hiyo iko hivyo kila mahali, kwa ndugu zetu wazazi wetu, wake zetu na hata jamii iliyotuzunuka, kamwe usipoteze muda wako kutaka kumbadilisha mtu.
  kwa mfano kwa kesi yako, ni kwamba bibie alikwisha fanya uamuzi na kama ungeendelea kulazimisha, lazima ungeingia kwenye fikra za uovu hususan kwenye kulipiza kisasi, na hilo lingekuwa ni kosa kubwa ambalo lingekuletea maumivu makubwa kihisia kuliko yale ya kuachwa.
   
 16. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  hii story imenikumbusha nikiwa darasa la tano kuna baba alichukua mkopo bank akakodisha shamba akalima maharagwe pale KIA. mwaka ule ukame ulikuwa mkubwa sana alienda shambani kukuta maharagwe yamekauka alianguka na kufariki palepale.Zamani nilikuwa nahudhunika sana na mambo madogo lakini siku hizi kikitokea kitu nasema already happen let me look the way forward
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Napajua hapo mahali wanapolima maharage katika eneo hilo la KIA, hata sisi tuliwahi kukodisha shamba katika eneo hilo, nadhani panaitwa MATIBA au MAKIBA, kama sikosei............

  Je sasa unadhani kilichimuua huyo mzee ni mazao kukauka au mkopo wa benki?
   
 18. mito

  mito JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,619
  Likes Received: 2,006
  Trophy Points: 280
  Tutasema yote, tutaleta theories zote lakini ukweli unabaki pale pale kama alivyosema kongosho kwamba kuumia utaumia tu ili hali umepoteza mali yako/zako. Muhimi ni how long you gonna be in that situation and to what extent

  Huo mfano wa balbu sijaupenda sana kwani tafiti karibia zote za nchi zilizoendelea zinagharamiwa na serikali au private companies zenye interest na utafiti huo, so utaona hapo researcher alipoteza tu muda wake na kazi ambayo alikuwa ameishafanya na ambayo ilikuwa haijaleta matokeo mazuri. Lakini kama lab na equipment vingekuwa vyake hasingesema maneno hayo. Isitoshe wanakuwaga na insurance cover ya majanga kama hayo
   
 19. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  mmm ya kweli hayo Mtambuzi?Me jina sikumbuki ila najua ni KIA.O.k nkilichomwua ni hayo mazao na mkopo wa benk vyote kwa pamoja coz kama hasingekuta mazao yamekauka obvious asingepata stroke palepale na kama asngekuwa amekopa benk ila mazao tu yamekauka obvious asingepata mshtuko mkubwa so vyote kwa pamoja vilipelekea kifo chake
   
 20. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  Bw.Mito naona umeshindwa kumuelewa Bw.Mtambuzi ni kweli mtu unaweza ukaumia kwa kupoteza mali au kitu chochote kile cha thamani.lakini kumbuka kuumia huko au kutokuumia kunatokana na wewe kutafsiri kile kilichotokea kwa mtazamo tofauti.Ni kama alivyosema Bw.Mtambuzi kwamba hakuna mtu anayeweza kumbadilisha tabia mwenzie kama yule anayebadilishwa tabia hataki....in short ni kwamba hata wewe huwezi kumbadili mwanao tabia kama hataki....kwa maana hiyo kuumia au kutoumia kwa mtu kutokana na kupata hasara au kupoteza mali inategemea na muhusika mwenyewe anavyoitafsiri ile hali....Nina miaka 18 nafurahi nimesoma na kulielewa hili somo inashangaza kuona watu wengi hawalielew hili somo na ndio maana Bw.Mtambuz anasema si lazma ukubaliane nae na wala hakulazimishi ukubaliane nae kwa sababu jukumu la kukubali au kukataa ni lako kutegemea na mtazamo/tafsiri yako.
   
Loading...