Kuficha Ugonjwa: Utamaduni sahihi kwa Wanasiasa wa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuficha Ugonjwa: Utamaduni sahihi kwa Wanasiasa wa Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mhabarishaji, Oct 30, 2011.

 1. M

  Mhabarishaji JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,001
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Katika mila na desturi za Watanzania; ni ajabu kwa wanasiasa maarufu kuugua; na hata wakiugua, basi siyo magonjwa sugu kama UKIMWI. Ndiyo maana wakiugua, basi tunawaza haraka kwamba, huenda "wamepewa sumu".


  Ingawa Watanzania wengi hatutaki kukubali hadharani, lakini ni dhahiri kwamba, wanasiasa wengi maarufu, wanaumwa magonjwa sugu; hususan UKIMWI. Jambo hili lilidhihirika, kutokana na jinsi wanasiasa hawa, kwa wingi wao; walivyomiminika kwenda Loliondo kwa Babu. Asikudanganye mtu! Watu wengi waliokwenda kwa Babu, kilichowavutia kwenda huko, ilikuwa tiba ya UKIMWI; na magonjwa yale mengine yaliyokuwa yanatajwa, yalikuwa ni danganya toto tu. Sasa tujiulize, kwa nini tunashindwa kuwa wazi kuhusu magonjwa ya wanasiasa maarufu?


  Kama tunalipenda taifa letu, hatuna budi kuuacha utamaduni wetu huu. Tabia hii ya wanasiasa maarufu, kushindwa kuwa wazi kuhusu magonjwa yao, siyo tabia njema; itakuja kuliangamiza Taifa letu lote. Wanasiasa hawa, ni kioo cha jamii. Wakishindwa kuonesha mfano, ni vigumu kutarajia kwamba watu wengine, watamudu kuwa wazi kuhusu magonjwa yao.


  Tujifunze kwa wenzetu, katika nchi ya Zimbabwe. Mwezi wa Juni, mwaka huu wa 2011; Makamu wa Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Thokozani Khupe, alitangaza hadharani kwamba, ingawa bado ana nguvu ya kufanya kazi; hata hivyo anaumwa Saratani (Kansa) ya Matiti. Baada ya kauli hii, Spika wa Bunge la Zimbabwe, Lovemore Moyo; alimpongeza hadharani mwanamke huyu, na kumtaja kuwa ni mwanasiasa wa kuigwa; kwa jinsi alivyokuwa wazi, kuhusiana na ugonjwa unaomsibu.


  Gazeti la Zimbabwe Standard la Oktoba 2 mwaka huu wa 2011; pia lilimnukuu Spika wa Bunge Moyo, akisema jana yake hadharani kwamba, wabunge wengi wa Bunge la Zimbabwe, wana UKIMWI, na baadhi yao wamefiwa na wenzi wao (waume/wake zao); kutokana na UKIMWI.


  Kabla ya hapo, mwezi wa Septemba, mwaka huu wa 2011; Rais Robert Mugabe, yeye naye; alisema kwamba anawajua Viongozi wengi wa juu wa Serikali, wenye virusi vya HIV, ambao wanatumia ARV's (dawa za kurefusha maisha). Akasema kwamba, pamoja na kwamba viongozi hawa wameathirika, bado wanawaambukiza UKIMWI, watu wengine; bila kujali. Akawaonya wasifanye hivyo, ili kulinusuru taifa hilo lenye waathirika wengi wa UKIMWI.


  Katika hatua nyingine, mwezi wa Juni, mwaka huu wa 2011; Mwandishi wa kike wa Gazeti la B-Metro, Simiso Mlevu; alimpeleka mahakamani, Mbunge wa Bulawayo-Insiza, Siyabonga Ncube (MDC-N); kwa kumwambukiza UKIMWI, huku akijua kwamba anao. Simiso alidai kwamba, amekuwa ni rafiki yake Ncube, kwa miaka miwili; baada ya mkewe kufariki. Aliendelea kusema kwamba ingawa Ncube alimficha, hata hivyo, alikuja kuthibitisha baadaye kwamba; mkewe Ncube alifariki kutokana na UKIMWI.


  Huo ndiyo uwazi uliopo kwa watu wa nchi ya Zimbabwe, wanajua kwamba hata wanasiasa maarufu wanaweza kuugua magonjwa sugu, na hata UKIMWI. Hivyo sivyo ilivyo kwetu Watanzania. Kwetu sisi, wanasiasa maarufu wakiugua, wanakuwa "wamepewa sumu". Tumefikia mahali pa kudanganyana kwamba, mwanasiasa fulani amepelekwa India, kwa sababu ya vijidudu 150 vya Malaria. Je, uongo huu ni kwa faida ya Taifa letu? Na je, wanasiasa wanaposhindwa kuwa wazi juu ya magonjwa yanayowasibu; TANZANIA ISIYO NA UKIMWI, KWELI INAWEZEKANA? Katika nchi yetu, eti UKIMWI ni maradhi ya walalahoi tu, lakini wanasiasa maarufu, wao, hawawezi kuwa nao. Tunamdanganya nani? TUTAFAKARI!
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  kaka hayo yote sisi hatuyataki ukizingatia swala la afya ni la mtu binafsi
  tunataka mchapakazi na ilivyo kawaida mtu mchapakazi,mpigania haki huwa acheleweshwi na mtandao wa mafisadi na ndio maana haraka watu tunaanza kuwaza habari za sumu

  ni ukweli usiopingika kwamba ya nini kujitangaza kuhusu afya yako hata wewe huwezi kufanya hivyo endapo unaumwa ni 1 katka 50.
  Kiongozi si lazima kwa kuzingatia hakuna sheria inayo wataka wafanye hivyo.
   
 3. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Huwezi kuchapa kazi kama unaumwa na tena unaficha maradhi.
  Kazi ni afya , ndio maana hata unapo kwenda kusoma ni lazima upime afya yako.
  Huwezi kujiunga na jwtz bila kupima ukimwi

  pia huwezi kupata ajira bot bila kupima ukimwi ,sasa watu wanapima ukimwi kwa mara ya kwanza lakini baada ya hapo wanageuka kuwa weruweru.


  Dhana ya kuchunguza afya lazima iambatane kwanza na kupima ukimwi. Siku hizi wajawazito wanapima kwanza ukimwi ili daktari aweze kuchukua tahadhari.

  Sasa kama wewe una ukimwi harafu unasema ni suala la afya ni la mtu binafsi kwa nini ufuatilie afrya za wabunge wanao kimbizwa kwenda india???

  Ubinafsi wa kuficha afya ni sawa na kutengeneza bomu litakaro lipuka baadaye baada ya ushahidi wa misululu ya loliondo!!!


  Siku hizi ni sera ya uwazi na ukweli katika afya!!!
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kaka maneno yako yametulia .Huu ni umbeya kabisa .Awaache waumwe hata yeye akiumwa hatangazi na ugonjwa ni siri ya mtu akiamua kusema poa akikataa poa .Sisi kazi na maendeleo mtu akishindwa ajiondoe mwenyewe .
   
 5. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii no kweli kabisa mbona alipougua gono hakutangaza au anafikiria sisi hatujui ???? viva la amistad
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kama afya ni swala la mtu binafsi kwa nini munafuatilia afya ya zitto kabwe???

  Kwa nani munahusisha ugonjwa wa mwakyembe na sumu???
  Kwa nini musimwache prof. Mwandosye mpaka mna hangaika kupika simu hadi india???

  Kwa nini watanzania wanalalmika mwakyembe na zitto walipo safiri kwa usiri mzito ???

  Je hizo ni afya zenu???
   
 7. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Rais kikwete alipo anguka jangwani kila mtu alikikua anafuatilia afya yake na hata alipokwenda kwa waganga wa kienyeji bagamoyo bado watu walifuatilia je, afya ya kikwete ni yenu???
   
 8. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wabung kapuya ngono.JPG e ni wagonjwa angalia
   
 9. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Afichae dhambi hatafanikiwa kabisa!!!!

  Mshahara wa dhambi ni mauti!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ... Swala la usiri wa Ugonjwa si kwa vinogozi peke yao!! I think it depends to whom do you hide your illness, your Dr ..? hili si sahihi .. Public...? Mhhh i don't think if they have any right to know!! ...Unless if you personally volunteers ...
   
 11. o

  onchoseciasis Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unamaanisha nini? ina maana wanasiasa maarufu waliopo India ni waathirika? acha hizo wewe; ugonjwa ni siri ya mtu na daktari wake, ana hiari kutangaza kwa watu wengine au laa!! sisi hatufuatilii afya yake kwamba anaumwa nini bali tunataka kujua maendeleo yake baada ya kupata matibabu
   
 12. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe hutaki kujua afya yake halafu wewe huyohuyo unataka kujua afya yake baada ya matibabu!!! Sasa nani atakujulisha kama si daktari??

  Mimi nakuona unajichanganya huwezi . Hata salamu za asubuhi tu watu huwa wanaulizia afya !!(vipi hali yako ya afya, umeamukaje?, watoto wanaendeleaje?) sasa mlolongo wote huo ni wa kutaka kujua afya ya mwenzako sasa leo wewe umekuwa kigeugeu na kujichanganya!!!!!
   
 13. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wamebinafsisha mashirika mengi ya serikali na sasa wanataka kubinafsisha afya!!!


  Huu ni ubinafsi mkubwa kusema afya ni suala na mtu binafsi!! Hapa lazima tujue!!!
  Ukiendelea hivyo hata afya ya watoto wako na ndugu zako utaacha liwe suala lao!!!
   
 14. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kuficha ugonjwa ni aibu kwa watanzania angalia ushoga unatunyemelea !!!


  Kama ukimwi umetufanya tufiche ugonjwa , je ushoga utatufikisha wapi?
   
 15. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Maneno yote uliyoyaandika nimeyapiga RED kwa sababu yamedhihirisha Utanzania Wako. Na kwa kweli Ndivyo Tulivyo baadi yawatanzania wengi, na Tusipobadilika sisi pamoja na akili zetu, dhana ya Ujinga itaendelea miongoni mwetu.
  Tumekuwa makini sana wa kutafuta makosa na madhaifu ya wengine, na tunaona raha kwelikweli endapo madhaifu ya mwenzetu yatawekwa hadharani ila Hatuongelei kabiiiiiisa madhaifu yetu Binafsi.
  Mhabarishaji wetu Ungefahamu kwamba pia wewe ni Mmojawapo wa Viongozi wa Taifa kwa namna moja au nyingine. Habari yako hii ni kama hotuba kwa Jamii tunayoisoma. Ungekuwa Mzalendo wa kweli Kwanza ungeangalia Kundule lako, kama liko OK ndipo ungehukumu kundule la mwingine. Ungeanza kwanza mwenyewe kwa kutujuza kuhusu afya Yako, Umepima au haujapima na matokeo yake yakoje. na kama umeshachukua CT scanning na majibu yake yakoje. kisha ukishatuambia hayo ndipo utugeukie na sisi na kututaka pia tuweke uwazi wa afya zetu na ndipo tuwageukie Viongozi wetu. Wewe mwenyewe mwooooga, hujapima na unakimbiakimbia ila unataka wengine waelezee afya zao. uwe mstaarabu.. Kabla ya Kuongelea personal za mwenzako kwanza Jicheki wewe mwenyewe. Mabadiliko yanaanza na wewe!
   
 16. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Asa ugonjwa na ushoga vinaingiliana kivipi? Unamaana ukificha ugonjwa utanyemelewa na ushoga? Na kama ni hivyo, je unamaana hao viongozi wengi wanaoficha ugonjwa karibu watakuwa mashoga?
   
Loading...