Shule za serikali enzi zetu zilikuwa best
enzi hizo shule za umma zilikua poa kulinganisha na za binafsi kwasababu
1. uwekezaji ktk shule za binafsi ulikua ni mdogo
2. kipindi hicho shule za umma zilikua chache na serikali ulikua inaajiri walimu waliokua wanamaliza vyuo.
3. kwa kiasi kikubwa, wanafunzi waliokua wanachaguliwa na kuripoti kt shule za umma walikua wenye uwezo mkubwa kutokana na mchujo wa kupenya ktk kuchaguliwa ktk shule chache zilizokuwepo. pia wanafunzi hao walikua hawahamii ktk shule za binafsi kwani shule za umma ndizo zilizokua zinafanya vizuri.
4. shule za binafsi walikua wanapata wanafunzi vilaza waliokosa nafasi za kuchaguliwa ktk shule za umma. vipanga wote walikua hawahamii shule binafsi kutokana shule za binafsi kuwa na ada kubwa na ufaulu mdogo.
5. ...
kwasasa shule za umma ziko nyumba ya shule za binafsi kwasababu
1. kuongezeka kwa shule a umma (hasa za kata). japo serikali zilizopita zilijitahidi kwa kiasi chao ktk kuboresha elimu kwa kuajiri walimu, ila changamoto ktk shule hizo ni nyingi na hazijaisha. hii imepelekea kuyumba kwa shule za umma.
2.
kutoajiri walimu ktk shule za umma kwasasa. huu uongozi wa bana matumizi, tukajenge uwanja wa ndege wa kimataifa kule chato unaathiri elimu yetu.
3. uwekezaji mkubwa ktk shule za binafsi. shule za binafsi zinazofanya vizuri zimewekeza sana ktk elimu. changamoto almost zote za kielimu hazipo ktk shule hizo. mazingira mzuri ya kufundisha na kujifunzia, walimu wa kutosha wanaolipwa vizuri, n.k.
4. shule za binafsi zinapata wanafunzi vipanga tena kwa mchujo wa kitaalamu. sio kama huku kwetu tunajisifu kua 98% ya waliomaliza la saba, wamechaguliwa kujiunga form one. huku walio wengi hawajui hata kusoma wala kuandika. vipanga wanavutiwa ktk shule za binafsi hasa ktk mambo ya mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia, na uwepo wa walimu wa kutosha wanaofanya kazi kwa moyo kutokana na kulipwa vizuri.
5. ...