Kufeli kwa shule za serikali

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,113
4,655
Matokeo mabaya kwa shule za serikali angalieni wakuu wa shule wengi ni wabovu na sio wabunifu wanashindwa kuwasimamia walimu wao hivyo serikali m-deal na hawa wakuu pia ikiwezekana muwachague walimu wa sayansi wawe wakuu wa shule.
 
Matokeo mabaya kwa shule za serikali angalieni wakuu wa shule wengi ni wabovu na sio wabunifu wanashindwa kuwasimamia walimu waho ivyo serikali mu deal na hawa wakuu pia ikiwezekana muwachague walimu wa sayansi wawe wakuu wa shule
Uchambuzi wako mbona finyu sana!
 
Matokeo mabaya kwa shule za serikali angalieni wakuu wa shule wengi ni wabovu na sio wabunifu wanashindwa kuwasimamia walimu waho ivyo serikali mu deal na hawa wakuu pia ikiwezekana muwachague walimu wa sayansi wawe wakuu wa shule
Mkuu tuliza akili na uache kutoa povu, hili andiko halina mashiko na pili haya uliyoyaandika yanatokana na utafiti ganiiiiii? Mbona serikali ilishakataza uuzaji na unywaji Wa VIROBA???????.........
 
Hivi unajua mwalimu wa Serikali wanavyonyanyaswa kupata haki zake,? Hivi unategemea darasani atafundisha akiwa na saikolojikale nzuri? Nyumbani kuko hivyo,Anaidai serikali haitaki kumlipa, Madaraja haimpandishi kwa wakati na wakati mwingine yanapandishwa kwa upendeleo, Mfano ninao ushahidi wa waalimu watatu shule ya kijijini waliajiliwa 2011 Hadi sasa hawajawahi kupanda daraja, Hawana kesi yoyote na wanafanya kazi izuri lakini hawathaminiwi,Sasa unamtaka Mkuu wa shule awasimamie nini? Waliopo halmashauri kutwa nzima wapo kwenye vikao visivyoisha tena vyenye kulipana posho, Je ni lini waalimu wamefanya vikao shuleni kwao wakajilipa posho? Polisi kila tarehe 15 Anapewa Ration ya chakula, 400000, Mwalimu kila tar 15 Anapewa nini? Acha kuropoka, Funga mdomo kama hujui chanzo cha tatizo
 
Mimi natofautiana na mleta mada. Unavyojaribu kulinganisha matokeo ya sasa na ya hapo nyuma jaribu pia kuzingatia mabadiliko katika udahili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza. Zamani walidahiliwa wachache na wenye uwezo mkubwa kutokana na ushindani uliochangiwa na uchache wa shule za sekondari wakati huo. Leo kila kata ina sekondari, tena baaadhi ya kata kuna sekondari zaidi ya moja. Chanzo cha wanafunzi ni shule za msingi zilizo ndani ya kata. Wanasiasa wanataka madarasa yajae wanafunzi wa kidato cha kwanza. Hivyo ufaulu wa darasa la saba inabidi ushushwe ili kukidhi haja. Matokeo yake darasa la saba zima katika shule husika linahamia sekondari. Halafu wasipofaulu sekondari lawama abebeshwe mwalimu. Hii sio sawa. Hata zifanyike jitihada gani, kama mtindo ndio huu wa kuhamisha standard seven karibia wote kwenda kidato cha kwanza, usitegemee mabadiliko katika ufaulu. Hivyo mtoa mada unakosea sana kuwashambulia wakuu wa shule. Hapo sijaongelea sababu nyingine ambazo ni nyingi tu zikihusisha maslahi ya walimu.
 
Matokeo mabaya kwa shule za serikali angalieni wakuu wa shule wengi ni wabovu na sio wabunifu wanashindwa kuwasimamia walimu waho ivyo serikali mu deal na hawa wakuu pia ikiwezekana muwachague walimu wa sayansi wawe wakuu wa shule
hoja yko haina mashiko.ufaulu wa mwanafunzi ni swala pana.
 
Matokeo mabaya kwa shule za serikali angalieni wakuu wa shule wengi ni wabovu na sio wabunifu wanashindwa kuwasimamia walimu waho ivyo serikali mu deal na hawa wakuu pia ikiwezekana muwachague walimu wa sayansi wawe wakuu wa shule
Ko walimu wa sayansi wa na nn cha ajabu katika kuongoza shule kuliko walimu wengine?
 
Mkuu tuliza akili na uache kutoa povu, hili andiko halina mashiko na pili haya uliyoyaandika yanatokana na utafiti ganiiiiii? Mbona serikali ilishakataza uuzaji na unywaji Wa VIROBA???????.........
Haya yoote ni madhara ya Shisha,, makonda kajitahidi kupigania matumizi Shisha ,, sasa madhara yke ndo haya post hazieleweki.
 
Matokeo mabaya kwa shule za serikali angalieni wakuu wa shule wengi ni wabovu na sio wabunifu wanashindwa kuwasimamia walimu wao hivyo serikali m-deal na hawa wakuu pia ikiwezekana muwachague walimu wa sayansi wawe wakuu wa shule.
Mawazo haya bila shaka yanatoka kwenye SIMtank
 
3e835b3bca40ee0c80eda89a2a578ed3.jpg
 
Mimi natofautiana na mleta mada. Unavyojaribu kulinganisha matokeo ya sasa na ya hapo nyuma jaribu pia kuzingatia mabadiliko katika udahili wa wanafunzi wa kidato cha kwanza. Zamani walidahiliwa wachache na wenye uwezo mkubwa kutokana na ushindani uliochangiwa na uchache wa shule za sekondari wakati huo. Leo kila kata ina sekondari, tena baaadhi ya kata kuna sekondari zaidi ya moja. Chanzo cha wanafunzi ni shule za msingi zilizo ndani ya kata. Wanasiasa wanataka madarasa yajae wanafunzi wa kidato cha kwanza. Hivyo ufaulu wa darasa la saba inabidi ushushwe ili kukidhi haja. Matokeo yake darasa la saba zima katika shule husika linahamia sekondari. Halafu wasipofaulu sekondari lawama abebeshwe mwalimu. Hii sio sawa. Hata zifanyike jitihada gani, kama mtindo ndio huu wa kuhamisha standard seven karibia wote kwenda kidato cha kwanza, usitegemee mabadiliko katika ufaulu. Hivyo mtoa mada unakosea sana kuwashambulia wakuu wa shule. Hapo sijaongelea sababu nyingine ambazo ni nyingi tu zikihusisha maslahi ya walimu.

Mkuu;
Natofautiana nawe kwa mengi tu. Huwezi niambia kuwa kwa sababu wanafunzi wengi huingia kidato cha kwanza kwa kufaulu kwao wengi ndio kunawafanya wafeli. Unataka kusema hakuna hata mmoja tu mwenye kuelewa?? Nadhani sema kuwa waalim wengi hawana wito. Wengi wamekuja kufanya kazi zao na wale wenye wito wa hiyo kazi ndo hao hukimbilia private kwa sababu wanasikika sifa zao hivyo hutwaliwa private chap chap.
Waalim ni wito sio kazi. Mwenye wito anacho kipaji cha kufundisha. Kama umeenda kufanya kazi hutakaa ueleweke. Kwa sababu unaangalia saa ukutani 45 min zako ziishe utoke. Unakopi skim ili kuwafurahisha wakaguzi.
Mkaguzi mwenyewe hana usafiri wa kufika huko uliko mara kwa mara.
Serekali; Badala ya kuwatumbua waalim wakuu, tafuteni waalim wenye wito sio wasaka ajira. Haiwezekani mwalim ufundishe mwaka mzima halaf wasikuelewe na mwakani uendelee. Huna wito.
 
Mmmmmh, ndugu. Unaongelea wito dunia ya leo? Yaani mtu apoteze miaka akisaka elimu, atumie resources za wazazi, alipie mkopo wa heslb indefinitely halafu unasema akafundishe kwa wito? Hapana ndugu hizo zama zimepita. Hawa hawa waalimu wasaka ajira(kama unavyowaita) wapewe incentives za kutosha , na mazingira ya elimu yaboreshwe kwa ujumla wake utaona matokea.

Umeongelea pia kuhusu suala la angalau hata wachache wangeonekana wamefaulu katika darasa husika. Ndugu yangu kama umesoma unajua hali inakuwaje unapokuwa kwenye darasa lenye ushindani wa watu wengi wenye uwezo. Automatically hautazembea, ni wazi nawe utajitahidi tu. Lakini kama waliodahiliwa ni wa ufaulu wa chini kama ilivyo siku hizi , hata wakiwemo wawili wanojitahidi watafeli tu kwa kuwa wapo kwenye wingi wa wenzao wasio na uwezo, hivyo kukosa ushindani na kurelax. Mfano enzi zetu sisi kufaulu darasa la saba haikuwa mchezo. Unakuta kata nzima au tarafa anafaulu mmoja tu na mwenye uwezo kweli. Sasa huyo anaenda kukutana na wenye uwezo wenzake, sikilizia moto wake hapo. Wala walimu hawakuwa na kazi sana. Lakini kwa ufaulu wa leo wa darasa la saba kumlaumu mwalimu ni kumuonea. Na pia kulinganisha matokeo ya sasa na ya hapo nyuma ni statistically insignificant.
 
Back
Top Bottom