Kufeli kwa DSM form 4: Nani alaumiwe Makonda, wazazi, wanafunzi au Jiji lililochini ya UKAWA

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
Kumekuwa na desturi ya kwanasiasa kuonekana wakati wa mazuri ila ikitokea mambo hayajaenda Sawa kila mmoja anakimbilia kiti cha nyuma.

Hivi haya matokeo ya dsm kwenye shule kumi zenye matokeo ya ovyo kabisa Nani anastahili kubeba lawama.

1: Mkuu wa mkoa Makonda, maana tuliona mama wa Mtwara akichukua Hatua kwa walimu wazembe ila wa dsm aliwasaidia kusafiri bure.

2: Jiji kwa sababu liko chini ya Ukawa, tulitegemea kuona taswira halisi ya elimu chini ya Ukawa.

3: Wazazi ambao hawana muda na watoto maana kila siku yuko barabarani anatafuta sent.

4: Wanafunzi wenyewe maana kama shule ya kata kijijini au mikoani anafaulu shule za kata dsm atajitetea kwa sababu gani.

Nani unadhani anastahili kubeba zigo hili na nini kifanyike kuepusha jiji kuwa jiji la vilaza.
 
Kama jiji likawa na population hii, kama hatua sisipochukuliwa miaka michache ijayo dsm itakuwa mahala hatari kwa usalama zaidi ya mwanza enzi zile za watoto wa wa kuleana. Ni kawaida kuchanjwa viwembe kama ukibisha kutoa pochi au saa au viatu.

Hii kitu ichukuliwe serious
 
Suala la kuporomoka kwa Elimu ni suala pana kuliko vile tunavyolichukulia,hatupaswi kumlaumu yeyote kati ya hao uliowaorodhesha,bali tunapaswa kurudi nyuma kama Taifa na kujitathimini upya ili tuje na suruhisho la kudumu juu ya Elimu ya watoto wetu.

Ziangalie zile zilizokuwa zikiitwa Shule za vipaji maalumu na Shule maalumu za serikali ambazo zina kila kitu kuanzia walimu wa kutosha,vifaa na mazingira bora ya kujifunzia,mbona nazo matokeo yake ni tia maji tia maji?

Chanzo cha anguko la Elimu yetu ni Sera ya Elimu na mafunzo pamoja na mifumo ya kutahini wanafunzi wetu wa Shule ya msingi.Tusidanganyane,tangu serikali ilipoanza kuhamisha watoto wote waliomaliza darasa la VII na kuwapeleka katika vyumba vya kata vilivyoitwa secondary,ndipo mdororo huu wa Elimu ulipoanza.

Haiwezekani darasa zima lilazimishwe kufauru na kujiunga kidato cha I kisha darasa hilo tulitegemee lije na matokeo mazuri ya kidato cha IV miaka minne baadae.Kumpeleka sekondari mwanafunzi asiye na uwezo kiakili huko sekondari hata wakimfanyia upasuaji wa Kichwa na kumuwekea material yote,bado hatoweza kufaulu.

Hadi pale tutakapoacha siasa kwenye mambo ya msingi,ndipo tutakapoanza kuishuhudia Elimu yetu ikichipua upya.Haiwezekani mtu mmoja apige marufuku jitihada zote zilizokuwa zinafanywa na Shule kwa makubaliano ya wazazi kwa kisingizio kuwa Elimu ni bure,kisha tutegemee matokeo mazuri,mtoto atafaulu vipi wakati majengo ya kata tunayoyaita sekondari yana upungufu mkubwa wa walimu?

Tunawaruhusu vipi watu wachache waliolewa madaraka wakatae kuajiri walimu wa kutosha kwa kisingizio kuwa walimu wanatosha wakati Ukweli ni kwamba Shule hazina walimu?Tamko la kutaka kuajiri walimu wa sayansi tu na kuwaacha walimu wa michepuo mingine lina maana gani ikiwa wanafunzi wanaendelea kupata "F" katika masomo ya Lugha na Biadhara?Tamko la kusitisha ajira za walimu wasiyo wa Sayansi lingekuwa na maana kama tungekuwa tunashuhudia "Vibanda" kwenye matokeo ya watoto wetu,lakini kama watoto wetu wanaendelea kupepea bendera za ccm(F),kwenye matokeo yao,kuzuia ajira za walimu wa arts ni upuuzi usiyovumilika.

Tuache siasa,hakuna Taifa lolote duniani lililoendelea kwa kuichezea Elimu ya watu wake,kupigia chapuo Elimu bure huku serikali ikishindwa kutoa fedha za kutosha kuendeshea Elimu,badala yake ikajikita majukwaani kuhimiza wananchi wake "wafyatuane" kwa sababu Elimu ni bure ni mbwembwe tu za kisiasa ambazo haziwezi kuwasaidia vijana wetu.
 
Sababu Ni Moja Tu! Mikoani Hakuna Maisha Kwahiyo Vijana Wanasoma Kwa Ajili Ya Kutafuta Maisha... Lakini Dar Maisha Yapo! Kwahiyo Vijana Hawana Muda Wa Kukesha Na Vitabu...
 
Makonda hajatoa tamko bado. Nasubiri kwa hamu.
Aongee nn cha maana kwa mfano..tangu aungie ulishawahi ona anatembelea shule ht moja kusikiliza changamoto au kuziona...yeye anatembelea clouds tu..na kupanda minazi iliyonyauka badala ya miti inayoeleweka...akajua akiwapa walimu ofa ya kupanda bure ataongeza ufanisi woooooooiiiiii
 
Back
Top Bottom