Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,558
- 41,078
Kwa bahati mbaya sana nchi yetu imekuwa nchi bandia. Kila kitu ni bandia.
Serikali inaundwa kutokana na uchaguzi bandia, hivyo na yenyewe inakuwa serikali bandia.
Bunge linaundwa na wabunge bandia na wa mchongo. Wabunge ambao wengine wametokana na kura za wizi, wengine wametangazwa tu kuwa wabunge bila ya kupigiwa kura na mtu yeyote. Kwa hiyo bunge letu nalo ni bunge magumashi.
Mahakama zetu zinaundwa na majaji wanaoteuliwa na watawala bandia, waliotokana kupitia uchaguzi bandia, na kukifanya kitu kinachoitwa mahakama, kuwa ni idara tu ya Serikali bandia. Kwa kuwa ni idara tu ya Serikali bandia, utendaji wake siku zote hufuata tu maelekezo ya Serikali bandia.
Ndiyo maana, kwa Tanzania, siyo ajabu, mtawala akaagiza fulani akamatwe,awekwe na asipewe dhamana, na ikawa hivyo. Atakamatwa na kuwekwa ndani, kosa atatafutiwa akiwa ndani. Mtawala akitaka, wakati wowote, anaweza kuagiza fulani aachwe huru, na ikawa hivyo.
Ndiyo maana kuna watu walipewa kesi za uhujumu uchumi, wakawekwa ndani bila dhamana. Na kisha, mtawala alipopenda, wakaondolewa mashtaka dhidi yao. Baadaye tena, miongoni mwao, waliojaribu kuwakosoa watawala, wakarudishiwa tena kesi za uhujumu uchumi.
Hii nchi ni lini tutakuwa na kila kitu halisia, yaani Serikali halisia iliyotokana na matakawa halisia ya umma, Bunge lililohalisia lililotokana na mapenzi na maamuzi halisi ya umma, na Mahakama halisia iliyopatikana kwa matakwa ya umma?
Tutaendelea kuwa na mihimili bandia mpaka lini? Wapi pa kuanzia?
Mihimili bandia haina haki ya kuheshimiwa.