Kufanya mapenzi kabla ama baada ya Ndoa, kipi bora?

Kufanya mapenzi kabla ama baada ya Ndoa, kipi bora?

Waliosema shake well before use hawakukosea.
Shake before use,inasaidia kujua stamina ya mwenzi wako,na ukijia utajua nini cha kufanya.
 
Mungu anaxema tuoane wote mabikira ukioa mwanamke aliye bikiriwa sio mmeo mke wa mtu kwani demu anavyo bikirwa damu inavyo Mara uume unavyo ingie ile damu mungu ndo anaichukua nakubariki name atakuwa ameorewa tayari mwanaume anaye mubikiri demu tayari akuwa ameowa kwahiyo kama umeoa used hujawai kumubikiri mwanamke yyote wewe bado hujaoa
 
Nauliza hivi sababu najua jukwaa hili tutapata muafaka wa hili jambo tukiweka kwa pamoja mawazo yetu katika jambo hili ambalo hua lina mkanganyiko katika mahusiano mengi.

Lakini je nauliza mapenzi ya dhati lazima yapimwe kwa zinaa? Naomba nitumie neno hilo kali mana ndilo linavyoitwa hivo katika Biblia kwa wanaokutana kimwili kabla ya ndoa. Au ngoja tu nipunguze ukal wa neno..je sex ndo kipimo cha mapenzi ya kweli?

Unakuta watu wawili mmekubaliana kabisa ..mwanaume amekubaliana na mwanamke kwamba wasubiriane.hadi ndoa ndipo watakapofanya sex ama tendo la ndoa mana wapo ndoani sasa,
lakini katika kusubiriana huko mmoja kati ya wapenzi hao anatembea na mtu mwingine, anakua na mahusiano na mtu mwingine na haichukui mda wana sex, lakini yule mpenz wako anaekupenda kwa dhati aliekuvumilia na ambae mlikubaliana kwa dhati kwamba msubiriane mana hio sex mtaenda kuifanya kwa nafas mkiwa kwenye ndoa, lakini wapi huyo unamuona sjui mshamba ama vipi ama hukumpenda ulikua unamtumia for your own selfish reasons ama sabab tu nyingine ambayo hazina mashiko, then huyo mwingine unamvulia nguo free kabisa mnafanya sex bila shida yoyote.

Badae matokeo yake mhusika ananogewa na mimba anashika anaamua kukuacha kabisa. Cases hizi zipo sana kwa wanawake na pia wanaume, na kwakwel inauma sana mana utafikiria kwamba through all that time alikufikiriaje ama alikuchukuliaje?

Kuna mdada mmoja mpenz wake alikua wamekubaliana kwamba April hii aje nyumban kujitambulisha, na situation ilikua kama hii nayoilezea kua walikubaliana wajitunze hadi ndoa ndio sex, lakin ghafla bin vuu jamaa kapita alipopita kampa.msichana mwingine mimba.

Mdada kachanganyikiwa na nyumban walikua wamejiandaa na ugeni mzito wa wakwe. Hamna kilichoendelea. Badae jamaa anasema alizidiwa, sasa najiuliza kama mtu uko na mpenz wako umezidiwa na unataka kwanini msiambizane tu, jamaa si angempa mimba tu mpenz wake?

Je kwani sex before marriage inakubalika kweli, na kwan ni kipimo cha upendo kweli? wanadai lazima upime sijui, kwamba mwenzangu yuko vipi, kwani amekua mchele? Na je vitabu vitakatifu vinasemaje?


Biblia inasema...Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe.

Sijui kwa wenzangu waislamu sijui katika kitabu chenu kitakatifu cha Quran kinasemaje kuhusu hili...mana lazima twende na maandiko sasa

Kama mfano mwingine mada flan imeletwa jukwaa hili, jamaa wamekubaliana na mpenz wake wa kike vizuri kwamba sex hadi ndoa, mwanamke akatambulishwa kwao, means mahusiano yalikua na muelekeo, kumbe mwanamke anafanya yake huku na kumvulia nguo mwanaume mwingine na mimba juu, na mipango ya ndoa iko katika hatua za mwisho, yule mpenz wake anaempenda kwa dhati akamuona mjinga, ndio jamaa anaambiwa akaanza kulia hadharani.

Msondo ngoma walisema ukiona mtu mzima analia mbele za watu ujue kuna jambo.

Tujadiliane hili kua nini hasa kinatokea ?? Ni mapepo ama nini?.ama kulogwa..!! Hivi upendo ama mapenzi ya kweli kabla ya ndoa yanaweza kupimwa kwa zinaa kweli???
Mapenzi kabla ya ndoa muhimu, yanakusaidia kujua mwenzako yukoje? Unamhimili vizuri? Je ukiwa naye utafurahia maisha yote? Je anajua mambo? Sio unaoa halafu mwisho wa cku unakutana na kitu ambacho hakikuwa matarajio yako. We ni teksi umepita njia ya trekta. Utajuta nakwambia
 
Mkuu hapa kuna vitu viwili kama sio vitatu...kwanza kwa maoni yako unaona kipi bora, kufanya sex kabla ya ndoa ama baada ya kufunga ndoa

Halafu pili, unakuta mmepanga na mwenzio na kukubaliana kwa dhati kwamba hakuna kukutana kimwili hadi mtakapofunga ndoa, lakini mwenzako huyo anakugeuka anakucheat kwa mwingine, na huyo mwingine anaeku cheat nae ashamvulia nguo,
ndo nauliza hua ni kitu gani hiki?

na tatu, mapenzi kabla ya ndoa ndo kipimo cha upendo wa kweli?
1)sex kabla ya ndoa ni good coz at mkiachan hutopata stress kwamba unalea kuku then huli nyama
 
Dunia ina mengi ndugu yangu. Yahitaji mkono wa Mungu kuvuka.
Ukisema unasubiri hadi ndoa utakuwa umeonekana muaminifu na watu watawapongeza. Lakini ukikuta umeingia kwenye ndoa na ukakuta kuna tatizo au upungufu fulani utaanza kujilaumu. Hii ndo husababisha mafarakano ya ndoa na uchepukaji. Fikiri mwanamke anakuja gundua mmewe hana nguvu za kiume na ameshaolewa inakuwaje??? Na watu waliowapongeza ndo wanaanza kulaumu kwa nn hukujaribu kabla ya kuingia ndoani??
Tumuombe Mungu sana wapendwa. Mfumo wa maisha waweza kufanya uyatende usiyokusudia.
 
No sex before marriage naona ipo vizuri zaidi. Inasaidia ndoa yenu kua ktk msingi mzuri ikiwa wote mnahofu ya Mungu..

Fata moyo wako vile unavokutuma ktk hilo na usimamie hapo bila kujali msukumo toka kwa mazingira ya kampani uliyonayo. Au jamii ilipoelemea,kama uko tayari kusubiri hadi ndoa we subiri bila kuyumbishwa na tamaa za mwili.

Uaminifu wako katika hilo usiathiriwe na mwenzako unaemtegemea. Mkiweza wote kujitunza mpaka ndoa ni heri kwenu zaidi....
 
Dah... Inategemea na imani yako.... Lakini kwa kutumia busara....kupiga gem kabla ni poa zaidi... unajua ubora wa mwenzio ambao utakusaidia kufanya maamuzi...siyo unaingia mkataba unakutana na kibamia au mfuko wa rambo...halafu unaanza kulialia.... Piga ua shibe ya gem ndiyo inabeba uhusiano kwa 99%...Vinginevyo ni sinema tu[emoji13] [emoji13]
 
Jamn zinaaa ni katika madhambi makubwa na yenye kurithika..ukizini na zinaa itaingia nyumbani kwako iwe kwa mama ako,dada zako,mtoto wako au hata mkeo..na msismeme zinaa inasaidia kujuana,kama mwanaume unajua huna nguvu kwa nn unaoa at first place?!!!..jitibu kwanza..bikra ni kitu kimethaminika sana katka uislam na mwenyezi Mungu amewatukuza sana mabikra katka Quran..na ndio maana wanaume watakaoipata pepo watapewa wanawake bikra kila wakiwaingilia bikra inarudi tena..mentality ya uzinzi ni mbaya sana na muandae majibu ya kumjibu Mungu kuhusu hao watoto wa nje ya ndoa au mimba zinazotolewa kukwepa aibu kwamba ulizini na hujaolewa.
 
Unajua ndoa nyingi zinaharibika kutokana na watu kutoridhika kwenye tendo msingi ni sex be4 mkiona kwamba hamkunani vzr bas unaacha mtu afunge ndoa na mtu atakaemtimizia haja zake
 
Ooh kumbe...
Kwaio mafundisho ya kiislam yanakataza kufanya hivyo.

ktk dini yetu ya uislam Kukutana baada ya ndoa ndio na sio kabla ya ndoa,ila tu ndo ivo dunia ya leo kusubiri mpk ndoa inaonekana mwiko lazma kuonjana,coz hata mtoto atakaezaliwa kabla ya ndoa yule atahesabika tu mtoto wa nje hata ikitokea mkafunga ndoa yule atahesabika mtoto wa nje ya ndoa.so kwa upande wetu haifai kusex kabla ya ndoa
 
....Inategemea na jinsi unavyotongoza mwanamke....kama utamfata kwa kigezo cha KUOA...basi ni lazima ukutane na kikwazo hicho cha KUSUBIRI HADI NDOA...yabidi uwe mjanja sana...na mbinu MUJARABU.. VINGINEVYO UTAISHIA KUNAWA TU...maana sisi wanaume ndy sehemu ya tatizo... wengi waliingia kwa LENGO LA KUOA akishapewa BUMUNDA anakuwa ANAKIMBIA now Madada wameshtukia hilo....NI bora yule anayefata kwa mapenzi tu....msichana anamuelewa haraka na atakula BUMUNDA wakati wewe ukisubiri KUOA....onja kwanza halafu tangaza NDOA utaeleweka....na so utangaze NDOA kabla hujala BUMUNDA....MWISHO utalia
Wadada wa humu jf embu mniambie kuna ukweli katika hili??
Kwamba mwanaume anaanza na wewe relationship haalaf anataka sex unampa then anatangaza ndoa ndo unamuelewa, lakin yule ambae mmependana mkaahdiana ndoa na pia sex had honeymoon unakua humuelewi,na hatimaye unamuacha, does it make any sense?
 
Adam hakuoa na alipiga gemu na Eva.

Ibrahim mpaka anapata mtoto hatukuoneshwa ndoa kafungia wapi.

Musa alilipa mahari lakini hatuoneshwi kama alifunga ndoa.

Leo mimi nisipige gemu kabla ya ndoa na jina langu hata kwenye biblia hakuna? Hapana.
[emoji16][emoji16]
naomba kwa wasomaji wazuri wa Biblia tunaomba msaada hapa kwenye hoja hizi hapa za ndugu yetu
 
Back
Top Bottom