ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,552
Nakumbuka nilipokua na ufahamu Wa kutosha mwaka 1978 nikiishi kwa uncle wangu Urafiki flats ubungo,kiwanda kilikua na hali nzuri na bora kabisakikiwa na wafanyakazi zaidi ya alfu tano waliokua wamejigawa katika shift tatu,SAA 1 asubuhi mpaka SAA 9 mchana,Shift ya pili SAA 9 mpaka SAA 5 usiku na shifi ya SAA 5 usiku mpaka SAA 1 asubuhi
Kiwanda kilimiliki mabasi takribani 10 kwa usafiri Wa wafanyakazi
Kiwanda kilimiliki Duka, LA nguo mjini
Pia walikua na maduka palepale Urafiki flats yaliokua complex kwa maana duka kubwa LA nguo,Duka LA chakula,
Kiwanda kilikua na flats hizo za gorofa NNE ambazo zilikaliwa na familia zaidi ya 300
Urafiki palikua na Kikosi cha Zimamoto na gari zake
Urafiki flats palikua na Urafiki police
Urafiki flats palikua na hospital
Urafiki flats palikua na tawi LA posts
Urafiki ilimiliki Band mahiri ya Dance
Urafiki ilimiliki Time nzuri ya Football
Urafiki ilimiliki timu nzuri ya netball
Urafiki ilimiliki kundi LA Sana'a
Ngoma,sarakasi,kwaya..nk
Urafiki walikua na timu ya boxing
Na vyote hivi vilikua ktk level nzuri tu kitaifa
Urafiki walikua na Shule Kubwa ya chekechea
Urafiki ilikua na ukumbi mkubwa Wa mikutano,sherehe wenyewe wakiuita Jumba LA maendeleo Urafiki
Kumbuka wote hawa wasanii mbali ya kushiriki sanaa/michezo pia walikua ni waajiriwa Wa kiwanda cha nguo urafiki
Cha kufurahisha Kiwanda kiliweza kuzalisha zaidi na mpaka kufikia kuvuka malengo na hiyo kupelekea wafanyakazi wote kupewa bonasi!
Mishahara pia walilipwa vizuri ,huduma za likizo na matibabu zilitolewa
Cha kusikitisha Urafiki ya Leo
Kiwanda kinaendeshwa na wachina
Ajira imepungua wafanyakazi hawazidi 100 hakuna shift
Flats sasa zinapangishwa kwa watu Wa nje wasio wafanyakazi
Wanapangaji wanazigeuza apartment wanavyopenda ikiwa ni pamoja na kutoa madirisha original na kuweka aluminium
Hospital imepangishwa na sasa kimekua chuo cha uandishi
Fire imekufa
Timu zimekufa
Band imekufa
Uzalishaji umeshuka sana
Ukumbi umekodishwa
Maeneo ya kiwanda yanavamiwa/kupangishwa mfano sasa kuna mpaka stendi za mabasi
Ni Mengi ya kuhuzunisha pale
Tumuenzi baba Nyerere.
Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app