Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,719
- 215,830
Habari za Jumanne wapendwa,
Jana usiku niliongea na shost, huyu shost alifiwa na mama yake January mwaka huu, kwakweli ulikuwa msimba mkubwa sana, ulimsumbua na alishindwa kwenda kazini miezi michace baada ya mazishi. Ni baada ya counselling sessions kadhaa ndiyo alirudi katika hali ya kawaida. Mama kwao ndiyo alikuwa mzaliwa wa kwanza, kwakua wazazi walikufa mapema, baada ya kuolewa yeye na mume wake walichukua jukumu la kusomesha wadogo wa mama, walihakikisha wote wamepata mafunzo yaliyowawezesha kupata ajira.
Mdingi ni wale wazee waliosoma wakati ukoloni, hakuipenda sana elimu ya Tanzania Enzi zile, hivyo ilimgharimu kutafuta kazi nje ya nchi ambako alihakikisha kuna elimu bora ya watoto wake.
Bahati nzuri watoto wote wamefanikiwa vizuri kimaisha lakini baba hakuwa amewekeza sana Tanzania kwakua muda mwingi alikuwa nje.
Bahati nzuri alinunua kiwanja ambacho kwasasa hivi mji ulivyopanuka kipo maeneo yaliyochangamka sana. Kwa ushirikiano watoto waliwajengea wazazi nyumba nzuri sana. Kwa exposure mama aliyopata huko kote alikokaa alijua kuteneza bites na juice na kufanya packaging mwenyewe, hivyo alifungua kiosk pembeni ya nyumba. Iiianza kama kiosk baadae lilikuja kuwa duka kubwa, mtaani pale watu wengi walitegemea kupata mahitaji madogo madogo kutoka dukani.
Kwa kuwaonea huruma watoto wake, mara nyingi mama aliwaambia wasitume pesa nyumbani, pesa ya kula yeye na mzee inatoka dukani. Watoto walizidi kumjazia mama stock kwani hakutaka mengi kutoka kwao.
Ghafla tu, maradhi ya moyo yalimwondoa mama duniani. Shost aliumia, aliniambia "Sky, huu ndiyo muda nina pesa ya ziada ya kumfurahisha mama, leo anaondoka". Ni mapenzi ya Mungu.
Kisa kinakuja, wakati wa msiba mama mdogo, mdogo wa mwisho wa mama alikuja na masanduku yake mawili msibani. Baada ya mazishi, watu wote wameondoka watoto wanamuuliza kulikoni, anasema yeye atabadi amtunze mzee. Walimwambia mfanya kazi anatosha kumtunza mzee.
Sasa shost jana ananipigia simu, mama mdogo amerudi, amemwambia shemeji yake kuwa anataka kuendeleza duka aliloacha dada yake. Shost amekasirika, amechukua likizo hivyo Jumapili anaondoka kwenda kumtoa mama mdogo, anajua hana lingine anamwinda msure.
Hivi inaruhusiwa kuoa mdogo wa mkeo mke wako akifariki?