Kuelimisha jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelimisha jamii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nahavache, Nov 16, 2011.

 1. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mara nyingi nimeona kile ambacho watu wengi walio na nafasi ya kufungua na kuangalia mitandao ya tovuti (internet) wanatoa maoni ambayo mara nyingi siyo hasa yale wananchi wanayoyaamini. Kwa mfano, leo nimefungua tovuti ya raia mwema nikaona kuwa asilimia 85 ya waliopigia kura swali kama ni sahihi au sio sahihi kwa wabunge wa chadema kutoka nje ya ukumbi wa mikutano wakati ule walisema ni sahihi kwa wabunge wa CHADEMA kutoka. Hata hivyo, jamii kubwa inaweza ikawa haiamini haya maneno. Tatizo kubwa ninaloliona ni kuwa watu wengi wanakuwa hawajaelewa hasa yanayoendelea katika ulimwengu wa siasa. Ni watu wachache tu ambao wanafikiwa na vyombo vya habari vinavyotoa habari sahihi. Kusema kweli, kuna vyombo ambavyo mara nyingi vinapotosha um asana. Hasa vyombo ambavyo vinamilikiwa na CCM na serekali. Mimi nadhani kuna haja ya mtu mmoja mmoja kuelimisha watu walioko vijijini ambao hawana nafasi ya kupata taarifa sahihi kutoka kwa vyombo vinavyotoa taarifa sahihi. Mimi kuanzia leo, kila siku nitatumia muda mchache wa simu yangu kuongea na wanavijiji angalau wawili kwa siku kuwaelimisha kinachoendelea. Na nitaitetea serekali kama jambo ni sahihi, ila nitaiponda pale ammbapo inaendelea kukandamiza demokrasia.
  Pia, nitashiriki katika maandamano yote yanayokuja. Sitawaachia wamachinga na walalahoi peke yao kuanzia leo. Maandamano ya kuupinga mchakato wa kupata katiba mpya ndio kwanza nitashiriki kikamilifu.
   
 2. s

  samoramsouth Senior Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tuko pamoja katika hilo, ni kwa ajili yetu na vizazi vijavyo
   
Loading...