Kuelekea uchaguzi mkuu wa DARUSO

miss confidence

JF-Expert Member
Jul 9, 2016
393
273
Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi mzima wa chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM) na Serikali ya wanafunzi wa chuoni DARUSO ambapo Leo serikali hii iliyokua madarakani kwa takribani mwaka mmoja sasa chini ya Rais wake Leon na Makamu wake mkuu Shamira Mshangama inaenda kumaliza muda wake ili kupisha uchaguzi mwingine kwa lengo la kupata serikali mpya na viongozi wapya ambapo zoezi zima la kuvunja Bunge linafanyika katika ukumbi wa THEATRE hapa chuoni.......

Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa kupata serikali mpya ya DARUSO napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wana JF wote has a wale wana UDSM kutoa tathmini juu ya serikali inayomaliza muda wake siku ya Leo katika mihimili yake yote mitatu Bunge, Mahakama na Serikali kuu kwa kutoa ubora na udhaifu wa kila muhimili na wizara zote za DARUSO bila kusita kumtaja kiongozi yoyote wa DARUSO kwa mazuri kama yapo na mabaya kama yapo aliyoyafanya kwa kipindi chote cha mwaka mmoja madarakani.......

Vilevile napenda kuwakaribisha kutoa mapendekezo na mtazamo wenu kama sehemu ya wanafunzi wa UDSM juu ya serikali itakayokuja katika uchaguzi utakao fanyika wiki chache zijazo.....

Napenda kuwasilisha kwenu wakuu.
 
Vp haugombei miss confidence niwe upande wako? Ila ofcoz kwa kias serikali hii,ya leon wamefany mazur ila mengi wamefeli kama kuweka wi-fi mabibo hostel,kushusha nauli ya shuttle kutoka shs.400 kwenda 300,pia suala la kuwashawish uongozi wa chuo kuweka mazingra mazur ya kusomea hasa kuweka fan katik venue ambzo zinabeba wanafunzi weng na kusababisha joto kali,zile fans wazoweka yombo 2 ule ni utani ase sio fans zile.ni hayo tu!
 
Kwani Daruso kwa wanafunzi wa udbs mbona muamko mdogo?Rais lazima itokee hapo kwenye majengo kuu kuu
 
Hakuna la ziada lililofanyika.

Serikali ijayo ijipambabue Kama serikali ya Wanafunzi wa Chuo kikuu cha taifa.
 
Jitahidini tu bavicha wasiingie ili utulivu uendelee kuwepo, Sina zaidi Mwenyekiti, migomo na maandamano imekuwa historia
 
Wakuu kuna jambo na hitaji kujua Kuhusu business administration evening class upoje Yani Ada, na muda wa kuanza na kumaliza vipindi nimeangalia prospectus na guide book haija elezwa
 
Back
Top Bottom