Joseph Ludovick
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 382
- 506
Haya ni maoni yangu binafsi.
Muelekeo wa siasa za taifa letu zinatia simanzi kwa sababu hazielekei kumkomboa mnyonge, bali kujenga katabaka ka vibwanyenye vyenye kuishi kutegemea jasho la wanyonge. nimekuwa katika upinzani kwa muda sasa, na tunavyoenenda imenipasa kutoa maoni na uchambuzi huu ili kwa pamoja ikiwa tutapenda tuangalie mustakabali utakuwaje katika jamii yetu muda mfupi ujao. nitazungumza kiujumla na kwa ufupi, mtazamo wangu juu ya siasa za sasa na kutoa hitimisho litakalotokana na hoja zilizojenga mada yangu.
Najua na ni kawaida kuwa kuna ambao hawatapenda haya ninayoandika, na watakaokimbia kusema tunatumika.nadhani hayo sasa tumeyazoea.TULIPO siyo pazuri kama taifa kwa sababu ya hali ngumu ya maisha kwa watu wetu. Wakati suluhisho la matatizo hayo likionekana kuwa mbali kabisa na kipaumbele cha viongozi wetu. Kwa mambo yanavyokwenda, nimefanya tafakari juu ya haya.
URAIS
Nionavyo mimi kwa sasa tumeacha kabisa kufikiri kama mwalimu alivyokuwa akifikiri juu ya uongozi na hatma ya taifa. kwa maoni yangu mimi Dr.Slaa peke yake ndiye anawaza uongozi katika namna ya Mwalimu Nyerere. Hoja za kijana kuwa rais hazina mashiko katika zenyewe kwani ujana pekee siyo kigezo cha uongozi. kuna wazee wenye mawazo na matendo ya ki ujana zaidi ya vijana na kuna vijana wenye mawazo ya kizee kuliko wazee wenyewe.isitoshe namna hawa vijana wanavyoongelea jambo hili ni ushahidi tosha kuonyesha kuwa hawana hekima kutosha kuwa rais wa nchi kama tanzania.
Lipo simulizi kwenye Biblia ambapo waisrael walidai wapewe kiongozi kijana.alipoteuliwa, akashauriwa na vijana wenziye na akatoa maamrisho kuwa kama mtangulizi wangu aliwachapa kwa fimbo, mimi nitatumia gongo. yaani kila kitu akakizidisha kwa ubaya. ingawa kijana anaweza kuwa rais lakini kwa nchi yetu ilivyo sasa hataweza.tusubiri mazingira na nyakati zikifika.
KATIBA
Japo katiba ni muhimu sana kama mother law, lakini pia kama social contract, nadhani watanzania wengi bado hawajui hata umuhimu wake achilia mbali kujua articles za katiba. kwa hiyo mpaka sasa ninathubutu kusema kuwa HATUNA MTU anayetetea katiba kwa ajili ya wananchi.maana uteuzi ulizingatia makundi na uwiano wake.kwa kweli makundi hayo yanatetea maslahi ya makundi yao. hoja inaweza kujengwa sasa kuwa si hayo makundi ndiyo wananchi wenyewe? jibu langu ni kuwa ni hapana kwa sababu hapo kila kundi lina mmbo yake ambayo yaweza kuwa yanakinzana na ya kundi jingine.
Isitoshe wabunge wa bunge la katiba wanawakilisha matakwa ya yule aliye wateua ama kuwapendekeza. lakini watanzania ni walewale.ujanjaujanja.wabunge wengi katika bunge la katiba ni hawahawa wavurugaji katika mambo mengine. udhu wa ghafla utakuja eti kwa kuwa ni wajumbe wa bunge maalum? hitimisho hapa ni hapana.
Kwa hiyo binafsi siioni katiba mpya, na ikija haitakuwa bado on the side ya wanyonge bali wanasiasa, ambao wote wanafanana kwa namna nyingi.rasimu hii ya warioba ikipita CCM wataikwamisha kwenye kura ya maoni. ama isipopita, UKAWA wataikwamisha siyo kwa kura ya maoni maana huko watashindwa bali kwa kuasisi vurugu. kwa ufupi hapa kuna giza.
CCM
Pamoja na udhaifu wake mbalimbali, chama hiki bado ni kikubwa kuliko vyama vya upinzani vyote kwa pamoja. kwa sasa scale yake ya kupendwa imepanda kuliko miaka miwili iliyopita. kwa hiyo ni sawa kusema hapa kuwa kitashinda uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu. Nimesema kuwa DR.SLAA,ni pekee kwa maoni yangu anayewaza kinyerere juu ya uongozi. pamoja na hayo kama mambo yanaendelea hivi yalivyo, mgombea wa CCM ndiye atashinda urais. na ninao uhakika hatakuwa Dr.Slaa.
CCM kama chama ni kikubwa,kina mfumo imara, organisation thabiti,maadili makini,na kwa kweli kiko karibu na watu.(huu ukaribu unahitaji Qualification).na kina wana mikakati mizuri na mibaya walio makini zaidi. bado kina raslimali watu na mali nyingi kuliko wengine.(hoja ya kusema eti walichukua za umma haina mashiko) hata sera za chama hiki as such, ni nzuri na practical kuliko vyama vingine japo kuwa zimekuwa blurred. kwa hiyo tutegemee CCM kuendelea kuwa madarakani kwa miaka kadhaa.
CHADEMA
Kina falsafa nzuri hasa ya nguvu ya umma. Sera na itikadi zake ni popo na hii falsafa ya nguvu ya umma ni nadharia tu kwa sababu umma hauna usemi wowote ndani ya chama kwa hiyo katika namna nyingi maneno na matendo ya chama hiki hayaendani. Ni chama kikubwa japo msingi wake siyo imara.hakijajua hadi leo maana ya viongozi wa ngazi ya chini. kimeshindwa mpaka sasa kupeleka mamlaka ngazi za chini.hata kanda tu imeshindikana.
Chama hiki kimeandamwa mfululizo na watawala nacho kimejibu hila kwa hila. makosa mawili hayafanyi baya kuwa jema. chadema hawapaswi kuiga tabia mbovu toka kwa watawala.
Chadema imeshindwa kabisa kutumia vema nguvu kazi na hazina ya vipaji ilivyonavyo katika chama.nathubutu kusema na ninajua mimi mwenyewe kuwa sekretariat ya chama hiki imechoka sana na haina tena mawazo mapya.lakini ni haohao wanategemewa kutuvusha mbele. Msigwa huwa anasema kufanya jambo lilelile kwa namna ileile na kutegemea matokeo tofauti ni uwendawazimu. nadhani chama changu kiutafakari ujumbe huu wa mjumbe wa kamati kuu. tumekuwa tunatumia mbinu zilezile kila wakati na kupata matokeo yaleyale. kwa nini tutegemee matokeo tofauti? na itakuwa hivi uchaguzi wa mitaa na uchaguzi mkuu. hakuna miujiza.
Ninaweza kusema kuwa aliyosema wassira na wabaya wa chadema,kuwa chama hiki kitakufa, yanatimia.chama kinakufa.kimsingi kimekufa. Kuondokewa makamu mwenyekiti, naibu katibu mkuu, wenyeviti wa mikoa ,wajumbe wa kamati kuu, viongozi wa jumuiya za chama, viongozi wa wilaya na majimbo,na wengine kwa makundi siyo jambo la kuongelea katika namna ya kusema oooooh hao ni mamluki, wasaliti nk. tunahitaji kujitathmini na kujipanga upya na hasa juu ya oganaizesheni na maadili.
Wabunge wengi wa sasa wa chadema hawatarudi bunge lijalo, japo tutapata wapya kwenye majimbo mapya.wabunge wetu wamekuwa superstars zaidi kuliko watumishi wa watu.watapewa somo la ubunge wa kitanzania una maanisha nini.Muone mtu kama SHIBUDA, pamoja na makeke yake,hakuna anayeweza kumuangusha jimboni kwake.
Nifupishe tu kwa sasa kuwa chadema kina wakati mgumu sana sasa na siyo kwa sababu ya kuhujumiwa (japo hujuma hazikomi na wala hazitakoma. na chadema nao wanafanya hujuma kwenye vyama vingine), lakini hasa kwa sababu ya matatizo yetu sugu ya ndani.
CUF
Chama hiki ambacho dhahiri, kimeshindwa kujinasua na dhana ya udini, kwangu mimi kwa sasa hasa bara hakijui hata kinataka nini. kinaimba nyimbo za cuf zanzibar.ambako sasa kiko serikalini na inaonekana kimenogewa. historia ya serikali za kitaifa ya karibuni kenye na zimbabwe,imeonyesha uchaguzi unapofika, wapinzani hufukuzwa rasmi serikalini. ndicho kitakachotokea zanzibar. habari ya kuondoka uongozini kijana Mtatiro bado haijaacha taswira nzuri kwa chama hiki kikongwe.dhana ya uongozi wa kiimla na kifalme, umeota mizizi huko.kifupi CUF inahitaji kuji redefine kama chama cha upinzani.
NCCR-MAGEUZI
Ninefikiri chama hiki baada ya kash kash nyingi, sasa kipo kwenye renaiscence. kinarudi kwenye mstari wake wa kuwa champion wa mageuzi.Kazi kubwa waliyofanya uchaguzi mkuu uliopita,na kazi nzuri inayofanywa na wabunge wake bungeni chini ya mbatia, sasa NCCR ndiyo almost imekuwa mboni ya wapinzani. hoja za wabunge wa NCCR ndizo zimekuwa hoja kali za kuyumbisha serikali.nawapongeza hawa jamaa na nadhani wanafanya kazi kama timu moja kwa sasa.
nadhani wataongeza wabunge wengi uchaguzi ujao, na hakuna maajabu ikiwa kitapata wabunge sawa na chadema au kikawazidi.ninafikiri kuwa NCCR ndiyo hasa chimbuko la madai ya katiba kama lilivyo jina lao.ninawatakia heri sana.
ACT-TANZANIA
Hatimaye chama hiki kidogo hatujui sawasawa malengo ya chama hiki kuanzishwa japo waanzilishi wanatupa misingi kumi ambayo kwa kweli ni mizuri. kinadai kinataka kufufua unyerere. yako baadhi ya mambo ya ajabu sana juu ya chama hiki. kwanza ni chama ambacho kinapigwa vita na wapinzani wenziye.hili ni jambo la aibu hasa kwa chadema kuona sasa kinapinga demokrasia ya vyama vingi.
Chama hiki kimesema na kurudia malengo yake lakini kinaambiwa kinaua upinzani.kwa hiyo hiki ni kihunzi cha kwanza kukiruka. chadema kwa sasa wanahitaji na kutamani wawe chama peke yao.
Lakini je chama hiki kinayo future gani?
Kwa maoni yangu, itategemea baadhi ya mambo. mfano kama ni kweli kuwa ZITTO na KITILA wako nyuma ya chama hiki, basi uhai wake utategemea kwanza watu hawa wawili wajitokeze hadharani na kuanza kujenga chama chao na kama hilo litatokea, chama hiki kitakuja kuwa chama kikubwa sana hivi karibuni tu. maana, kuna watu WENGI wako frustrated katika vyama vyao vya sasa, watakuwa wamepata pahala pa kupumulia. katika kufikiria mbali,na kama CCM ikimeguka kuelekea uchaguzi mkuu na mgombea mwenye nguvu huko akatemwa akaamua kujiunga ACT, mimi sioni ugumu kuwa chama hiki kinaweza kutoa rais wa awamu ijayo. na hizi siyo ndoto.
Ilivyo sasa, wengi katika chadema wanaitukana ACT mchana lakini usiku wanalala huko.muda utawafichua.
UKAWA
Muungano huu ni muhimu sana. lakini kwangu mimi UKAWA hauna future yoyote.kwa hiyo sihitaji kutumia nguvu nyingi kuelezea jambo hili. tayari kuna kushikana uchawi katika UKAWA. mtu kama Julius Mtatiro katibu mkuu wa ukawa kushambulia gazeti la Tanzania Daima akiliita la Mbowe eti limemwandika vibaya, na of course haikupaswa, ni dalili za huko tuendako.tusubiri tuone. tayari wametakiwa na maaskofu kurudi bungeni bila masharti. je watawavimbia viongozi wa dini? kusema eti lazima ijadiliwe rasimu ya pili sawa. lakini isipojadiliwa si kuna kura ya maoni? na zaidi si kuna uchaguzi mkuu? Kwa hiyo UKAWA waache visingizio,warudi bungeni mara moja na wala wasikashifu maaskofu wetu.
HITIMISHO
Kutokana na hayo hapo juu, political situation yetu siyo nzuri.tunawayawaya kama machela Upinzani umekuwa kama tawala na hatuna pa kutokea.ikiwa ni hivi tusishangae CCM itakuwa madarakani kwa miaka mingi mbele.