Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Naomba kuibua mjadala huu,
Kwanza wote tunakubaliana kuwa Tanzania inahitaji viwanda ili kusonga mbele kiuchumi lakini swali ni kwa namna gani tunaweza kufika huko. Kwa hiyo badala ya kulaumiana tu au kila mmoja kufikiri mwenzake ndio mwenye wajibu naomba kila mwenye wazo achangie hapa;-
1. Unafikiri ni kwenye sekta zipi hasa tunaweza kuwekeza viwanda vipya (kwa mazingira ya Tanzania) na ni viwanda gani "Specifically"? na kwanini hapo?
2. Unafikiri ni kwa namna gani tunaweza kuanza, tuanze vipi na kwa nini?
3. Unafikiri ni maeneo gani hasa yanayotakiwa yawekezwe na watanzania wazawa na yapi yanaweza kuwekezwa na wageni na kwa nini?
Nafikiri mjadala huu unaweza kusaidia kitu kama sio vitu.
Elewa kwamba wewe una wajibu kama alivyo na wajibu mwingine na mwingine; Tuache kulaumu na kulalamika, saidia unapoweza hata kama ni mawazo mradi tu usiseme "Lazima tutakwama!" maana kuna watu wenye mzimu wa kukata na kukatisha wengine tamaa.