zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,835
Kuelekea Maadhimisho ya Nyerere Day tarehe 14.10.2020.
Akiwa kama muasisi na Baba Wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya .
Likiwemo la kusaidia Tanganyika kupata uhuru wake kutoka kwa mabepari na mabeberu mnano tarehe 9.12.1961.
Anakumbukwa kwa mengi pia alizisaidia nchi nyingine za kiafrika kupata Uhuru wake.
Sasa ni miaka takribani 21 hatunaye tena lakini nukuu,maneno na ujasiri na ukakamavu na uongozi vitabaki kuwa kumbukumbu tosha kwa wale tuliosoma historia yake au hata wale waliomshuhudia akiwa hai
Tukielekea siku ya maadhimisho hebu tujikumbushe aliyoyafanya mwalimu na jinsi uongozi wake ulivyotukuka.
Unamkumbuka Mwalimu kwa lipi hasa?
Hizi ni baadhi ya nukuu za Mwalimu Julius Nyerere
"Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo"
"Elimu sio njia ya kuepukana na umasikini bali njia ya kupambana na umasikini"
"Uchumi katika nchi haupimwi na maskini wanaotumia usafiri wao Bali na matajiri wanaotumia usafiri wa umma"