Kuelekea Novemba, 10: Je, Tanzania na Afrika kwa ujumla inatumia vipi sayansi kulinda amani na kuleta maendeleo?

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Salaam wanaJF,

Ulimwengu unaelekea kuadhimisha Siku ya Sayansi kwa Amani na Maendeleo Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Novemba 10 ya kila mwaka.

Siku hii ina lengo la kuangazia umuhimu wa sayansi katika jamii na uhitaji wa kuhusisha sehemu kubwa ya jamii katika mijadala juu ya masuala ya kisayansi. Pia, inahimiza umuhimu wa sayansi katika maisha yetu.

Katika kuihusisha jamii na sayansi kwa ukaribu, siku hii inalenga kuhakikisha wananchi wanataarifiwa kuhusu masuala yanayoendelea katika ulimwengu wa sayansi. Aidha, inalenga kuelimisha juu ya nafasi ya wanasayansi katika kupanua uelewa wetu kuhusu dunia, sehemu tunayoiita nyumbani.

Kauli mbiu ya 2019 ni: "Open science, leaving no one behind" yaani ‘’Sayansi iliyo wazi (inayofikiwa), hakuna anayeachwa nyuma’’

Hii haimaanishi sayansi kuwa ‘’wazi’’ au ‘’inayofikiwa’’ tu na kada zinazofanya tafiti, bali wazi na inayoweza kufikiwa na jamii nzima.

Pamoja na juhudi na hatua zilizokwisha pigwa katika miaka ya hivi karibuni, bado kuna utofauti katika maeneo mbalimbali katika nchi tofauti, hasa likija suala la watu kuifikia na kutumia sayansi, teknolojia na ubunifu mbalimbali na kufaidi matunda yake.

Moja ya mambo ambayo ni matunda ya ubunifu wa kisayansi imekuwa ni mitandao ya kijamii. Nguvu ya matumizi chanya ya mitandao ya kijamii imeweza kubadili hali ya demokrasia na uchumi katika nchi nyingi za Afrika kutokana na kuwaunganisha wananchi wa kada zote.

Nguvu hii kwa namna fulani pia imeleta hofu kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa barani kote. Nchi kadhaa za Afrika kama vile Gabon, Sudan, Chad, DRC n.k zimewahi kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa sababu za kisiasa na ‘’kiusalama’’.

Je, watu katika Tanzania na bara la Afrika kwa ujumla wanaifikia sayansi na teknolojia kwa uhuru na kufurahia faida zake?

Je, Tanzania na Afrika kwa ujumla inatumia vipi sayansi kulinda amani na kuleta maendeleo?

Nawasilisha.
 
Bahati nzuri Rais Magufuli Ni mwanasayansi. Hatuna wasiwasi ni ubunifu, mipango na utekelezaji.
 
Back
Top Bottom