Naomba kutoa maoni yangu kuhusu mkutano wa CCM unaokwenda kufanyika hivi karibuni.
1. Ikiwapendeza naomba wachague mgombea mwingine wa Urais anayekubalika zaidi na wananchi. Hii itasaidia kutotumia nguvu na gharama kubwa wakati wa kampeni.
Lakini kuna shida gani akisimama mtu mwingine wa CCM kutetea kiti cha Urais badala ya aliyepo? Je, yeye atakuwa amepungukiwa na nini zaidi, kwa sababu kama ni mafao ataendelea kupata kama wanavyoendelea kupata wastaafu wengine. Nadhani yeye angejitahidi kurudisha heshima yake kitaifa na kimataifa na kisha angewaachia wengine huku akiwa bado na heshima yake ile ile iliyokuwepo mwanzo.
2. Wamwachie Lissu na wengineo huru na kupiga marufuku vitendo viovu kama vile utekaji na kuumiza watu. Hii itawarudishia imani kwa wananchi, kwa hiyo hawatapata shida sana kwenye kampeni za Uchaguzi.
3. Waache Demokrasia ichukue mkondo wake na wasikubali hata kidogo kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2025 pasipo CHADEMA. Hii itarejesha taswira mpya huko Duniani, kwani kwa sasa taswira imedorora sana.
Nasisitiza kwamba, wangemwacha asafishe njia vizuri na aondoke salama bila shida na kwa kufanya hivyo angekuwa amewatengenezea njia nzuri sana wanawake.
Huko mbeleni hata angetokea mwanamke akagombea kiti cha Urais watu wangemuunga mkono sana wakimkumbuka huyu wa sasa kwa mazuri yake ya pekee.
Nawasilisha.