Kuelekea mechi ya VPL' Simba SC dhidi ya Azam FC, ni kweli mchezo sio ushindani?

Ikiwa ni siku moja imebaki kuelekea kwenye mchezo wa Vodacom Premier League VPL, ambapo Jumapili ya January 7, 2021 wakati Bingwa Mtetezi Mnyama Mkali Simba SC, itakapokwaruzana na Wana lamba lamba Azam FC kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 kutokana na kila timu kuhitaji ushindi na kujikusanyia alama tatu muhimu ili kuongeza ushindani kwenye kinyang'anyiro cha kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania.

Mpaka sasa kwenye msimamo wa VPL, Simba SC inashika nafasi ya pili kwa alama 38 kwa michezo 16, huku Azam FC wakishika nafasi ya tatu kwa alama 32 kwa michezo 17.

Baadhi ya mashabiki na wadau wa soka wanasema mchezo huo si wa ushindani kwasababu Azam FC wakipambana na Simba SC ni tofauti kabisa wakicheza na Yanga SC

Je kwa mtazamo wako utakuwa mchezo wa aina gani? kweli mchezo huo si ushindani au ni vile tu uwezo wa Simba SC ni mkubwa kuliko Azam FC?

Mpira Biriani... Mpira Ice Cream
Azam ni mtoto wa simba,ba hiyo timu ilianzishwa kwa ajili ya kuikata makali yanga,leo watakazana sana,mara paaap watafungwa 2 bila na simba kimtindo mtindo
 
Magazeti ya Tanzania yana dhambi sana
Screenshot_20210207-091252~2.jpg
 
Back
Top Bottom