Kuelekea mechi ya VPL, Simba SC dhidi ya Azam FC, desturi ya ushindi inaendelea

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Nyasi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumatano ya Oktoba 23, 2019, zinatarajia kuwaka moto kwa mpambano mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika tishini, katika ile patashika ya Vodacom Premier League VPL, ambapo Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali, watakapokwaruzana na Wana Lamba lamba Ice Cream, Azam FC.

Katika kuendelea na desturi ya ushindi kwa asilimia 100 huku ikiwa imeshinda mechi zote zilizochezwa mpaka sasa, kikosi cha Simba SC chini ya kocha Professor Patrick Aussems, kimejiandaa vilivyo kuwapa burudani Wanasimba na Wadau wa kandanda pamoja na kuweza kupata ushindi na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa VPL.

Kulitaka Mwana...Kulipewa Mwana

Wanasimba na wapenda soka popote pale, jitokezeni kwa wingi kuwashangilia Mabingwa wa Nchi wenye kuonyesha radha ya mpira uwanjani, yaani burudani pamoja na ushindi...

Kandanda la viwango vilivyothibitishwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF..NguvuMoja

tapatalk_1571757206169.jpeg
IMG_20191022_181043_764.jpeg
 
Leo tunataka kakolanya aanze maana ameonyesha kitu cha tofauti kwenye match za kirafiki imefika mda sasa aishi akae kando but simba ushindi leo lazima
 
Back
Top Bottom