Kuelekea Derby ya Jumapili, Ahmed Ally amekata pumzi?

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Kama tujuavyo Jumapili hii kuna mtanange wa Watani wa jadi Simba vs Yanga. Katika mchezo huu Simba ndio mwenyeji huku Yanga akiwa mgeni, kama tunavyojua lazima kunakuwepo na hamsha popo na hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa timu mwenyeji kuhamasisha mashabiki wao wajae kwa wingi uwanjani.

Mpaka sasa hakuna hamasa yoyote kutoka kwa msemaji wa Simba, je ndio tuseme amekata pumzi au amenusa ameona hawana ubavu wa kuifunga Yanga kwa hiyo hawataki mashabiki wengi uwanjani ili aibu waipate wakiwa wachache?
 
Hii ni Simba bro, Ahmed akiingia mtaani siku moja kuhamasisha ni sawa na yanga aingie wiki mbili.
 
Kama tujuavyo Jumapili hii kuna mtanange wa Watani wa jadi Simba vs Yanga. Katika mchezo huu Simba ndio mwenyeji huku Yanga akiwa mgeni, kama tunavyojua lazima kunakuwepo na hamsha popo na hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa timu mwenyeji kuhamasisha mashabiki wao wajae kwa wingi uwanjani.

Mpaka sasa hakuna hamasa yoyote kutoka kwa msemaji wa Simba, je ndio tuseme amekata pumzi au amenusa ameona hawana ubavu wa kuifunga Yanga kwa hiyo hawataki mashabiki wengi uwanjani ili aibu waipate wakiwa wachache?
Kwa joto lililopo kuhusu hii mechi, inajaza bila hamasa
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Kama tujuavyo Jumapili hii kuna mtanange wa Watani wa jadi Simba vs Yanga. Katika mchezo huu Simba ndio mwenyeji huku Yanga akiwa mgeni, kama tunavyojua lazima kunakuwepo na hamsha popo na hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa timu mwenyeji kuhamasisha mashabiki wao wajae kwa wingi uwanjani.

Mpaka sasa hakuna hamasa yoyote kutoka kwa msemaji wa Simba, je ndio tuseme amekata pumzi au amenusa ameona hawana ubavu wa kuifunga Yanga kwa hiyo hawataki mashabiki wengi uwanjani ili aibu waipate wakiwa wachache?
Hii mechi ina viashiria ya Simba kupoteza nukta 3, kutokana na ubora wa timu ya Yanga katika upambanaji kiwanjani. Tatizo ya mechi hizi za watani wa jadi mara nyingi huchezwa sana nje ya uwanja kuliko kiwanjani, kwa sababu hiyo ni ngumu sana kuitabiri na kwa wale wa kubeti ndiyo kabisa wanaenda kuchana mkeka. Mara nyingi Simba siku ya Jumapili inawabeba wao, lakini wakati wa kucheza ni siku ya Jumapili 5-11-2023, saa 12:00 jioni na jua linazama takriban saa 12:15 kwa siku hiyo, hivyo kuipa Simba utangulizi wa dakika 15 za mwanzo, jua likipinduka tu na kuzama siku ya Jumapili inakuwa imekwisha hivyo yale mambo ya watu wa falaki yanukuwa ndiyo kusema vijana wa Jangwani ni mwendo wa kushambulia kama nyuki na kuwakosesha raha watoto wa Msimbazi.
Hii mechi ni muhimu kwa Yanga kwani ndiyo itakayowajenga kisaikolojia pindi watakapocheza na Al Ahly ya Misri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom