Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Watu wapenda nchi kwa sasa tunajadili matatizo yetu ili tuje kuyatafutia mtu wa kuyatatua. Nchi hii ina watu wengi tu wanaofaa uongozi na sio huyo mzee usiye na uhakika hata wa afya yake.
 
huyu mzee anautaka sana urais kwa udi na uvumba naamini atakosa kwa sababu-

-kuna makundi yanaogopa kisasi cha huyu jamaa hata wale waliopokea hela zake
-Migiro hata kama hapendwi anaelekea kupata baraka za mwenyekiti
-Richmond bado ni mzimu unaomuandama

anyway mtazamo wangu tu pengine nimekosea time will tell ,
 
Pasco hivi pale Nyerere alipomlebo EL ni mla rushwa kutokana na utajiri aliokuwa nao usiokuwa na maelezo alimuonea wivu tu ama aliuona ukweli fulani ama alikuwa MUONGO? Lakini la pili huyu material president wako hapendi kulaumu ufisadi kama ndio uliotufikisha hapa hata siku moja nae anamipango na kelele kama hao wengine..to me hakuna chochote kwa EL hata kama umekuwa obsessed ama addicted kiasi gani..ni mmoja wa wahujumu uchumi like others full stop
 
EL haingii hata chembe kwa Mh. Mwakyembe! kwanza ni fisadi na huo ndio ukweli na tuelezwe hizo fedha zote anapata wapi kama sio za akina RA ili waweze kuja kutumaliza kabisa? Raisi anatakiwa awe mwadilifu kama Mh. Mwakyembe na sio vinginevyo!
 
Watanzania kama sumu inajaribiwa mdomoni, jaribuni kumweka lowassa kama rais, mtalia na kusaga meno! Huyu jamaa ana hila, fitna na mlipiza kisasi wa waziwazi. Kina nape na wenzake mjiandae!
 
mmaranguoriginal mie ningependa kujua tamaa ya Lowassa ni nini?

Kama umeipima naomba nijue umeipimaje.

Natanguliza shukrani
 
Last edited by a moderator:
Kweli Lowasa angefaa lakini kuna jambo linalonipa wasi wasi nalo ni hili: Pesa anazotoa ktk Harambee anazitoa wapi?? Pia anategemea kuzirejesha kupitia njia ipi?.
 
Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimemkubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK!, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai mwenyewe kuwa yuko fit, japo he looks sick!), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, then matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali!..., mkatae!.

Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa matarajio katiba mpya pia ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.
Nafanya mapitio tuu!.

Pasco
 
Hakuna kazi ngumu kama kumkampenia EL, Pasco you are on MISSION IMPOSSIBLE
attachment.php
haha...kipanya alinifurahisha sana hapa....
 
Last edited by a moderator:

Mwisho.
Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Pasco.
Nafanya rejea nikilinganisha na kinachoendelea sasa kwenye vikao vya chama cha Mapinduzi, CCM!.

Pasco
 
Nina wasiwasi Mzimu wa JK.Nyerere utamwengua EDO-2015 kama ulivyommaliza S.Sita hata kabla ya Oct. 2015.
Kwa hiyo ni vizuri Friends kutoku sahau hili.


[h=1]J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'[/h]
S. Sita ambaye alikua Compaign Manager wa J. Kikwete na E. Lowasa kwa pamoja aliinuka na kumtetea sana Lowasa hadi kufikia kusema hizo ni tuhuma tu hazijathibitishwa na pia kua Lowasa ana mvuto mkubwa kwa wananchi na anakubalika sana.

Baada ya kusikia "upuuzi" huu Nyerere hakusubiri Sita amalize hadithi zake alimkatisha na kumwambia "Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa, na kama ni mzuri kanywe nae chai". Wana-CC wengine wajitahidi kuwatetea Lowasa na Malecela kwa nguvu kubwa maana tayari walikua na makundi. Kutokana na hilo Nyerere alisema "Niko tayari kurudisha kadi yangu ya chama, CCM sio baba yangu wala mama yangu. Kuna wagombea wana uchu sana wa kwenda Ikulu. Mimi nimekaa pale ikulu kwa miaka 25. Ikulu si mahali pa kupakimbilia, ni mzigo. Ukiona mtu anakimbilia ikulu ujue huyo ni wa kuogopwa kama ukoma hasa anapotumia pesa. Je amepata wapi hizo pesa na atazirudishaje??". Kutokana na tishio hilo pamoja na nguvu kubwa aliyokua nayo A. Mrema wa Nccr ilibidi wana-CC hao kunywea hivyo Malecela na Lowasa wakachinjiwa baharini. Majina 5 yakapelekwa NEC na hatimaye majina ma3 yakapelekwa Mkutano Mkuu (Mkapa, Kikwete na Msuya) na mwishowe Mkapa akachaguliwa kuwa mgombea wa CCM
 
Hata madudu ya Richmond, alitaka kuwafurusha na kutaifisha kila kitu ila alishindwa!, kutokana na "mwenye mitambo!".

Halafu unadai ni mjasiri na mtendaji mzuri.
Hahahaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom