Kudhalilishana tu

Kudhalilishana tu

mamii2

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2014
Posts
356
Reaction score
108
Hi wana JF wote!

Weekend hii bhana nilienda kumtembelea best angu mmoja hivi sasa katika tembeatembea tukakutana na mbaba mmoja hivi jirani ake, baada ya salamu akapita zake best akaniambia namuonea huruma kweli huyu baba siku atakapogundua tabia ya mkewe sijui itakuaje,

Ni hivi huyu mke wa huyu jamaa ana tabia ya kusimulia madhaifu ya Mme wake kwa mashoga zake anadai kuna siku moja huyo mwanamke alikuwa anawasimulia;

''Yaani huyu mwanaume natamani nimuache hata leo kitandani hawezi chochote yani kinachonifanya niendelee kuishi naye ni kwa vile ananijali na ananipa kila nachotaka lakini kwenye swala la 6/6 ni sawa na ananichafua tu. Ila nina mtu ambae ananifikisha ninavyotaka''.

Wakati anaawaambia hayo mara akapigiwa simu na mume wake basi akawaambia ''ngoja niende huyu ----- ananiita naona anaongea kwa ukali kweli sijui kapatwa na nini''.

Anavyodai alivyofika kwake huko kamkuta mmewe kafura hatari kabla hajakaa kapokelewa na kibao hajakaa sawa kingine ''nini mume wangu mbona unanipiga nimefanya nini?''. Mume wake kwa hasira, ''nimekusikia yote uliyokuwa unawaambia mashoga zako''.

Mwanamke akaachia kicheko akamwambia, ''Mume wangu hicho ndo kinakufanya unipige me pale nilikuwa najaribu kukulinda mme wangu kuna shoga angu mmoja nasikia anakutaka na anasema atafanya chochote il aweze kukupata, kwa hiyo nilifanya vile ili kumkatisha tamaa si unajua ninavokupenda Mme wangu''.

Basi mwanaume akanywea akasema, ''basi samahani mke wang nilifikri una mtu mwingine zaidi angu'' mwanamke tena akamjibu ''ninavokupenda mme wangu njoo unipe haki Yang kwanza''.

Basi walivyomaliza mchezo wao mwanaume akapitiwa usingizi, yule mwanamke kaenda kuwasimulia mashoga zake kila kilichoendelea alivyomaliza akawaambia ngoja nirudi asije akaamka akanikosa.

Wakati anaudi kwake shoga ake mmoja akachukua simu akampigia simu akamwambia tunajua kila mlichokifanya mkeo kaja kutuambia mwanaume alichojibu huyu mwanamke vipi anatoka nje harakaharaka anakutana na kutana na mkewe mlangoni katoka kuoga kamuuliza unatoka wapi alichojibu ''mme Wangu si unaona nimetoka bafuni kuoga baada ya shuhuli pevu ulionipa?".

Basi mwanaume hakuwa na la kufanya zaidi ya kufikiria kuna watu wanataka kuwachonganisha.

Mimi kwa upande Wangu sikufurahishwa na tabia ya huyu mwanamke, hamtendei mwenzie haki hata kama ana mapungufu hakupaswa kumuacha mwenzie uchi hivi. Sijui ingekuwa ni wewe ungefanyaje?
 
Ndiyo mjue nyie wanawake ni zaidi ya Delila.. Tutaishi nanyi maana ni mtihani tumepewa.
 
Huyo mwanamke ana matatizo sijui niseme ya akili.

Maana unapomtangaza mwanamme wako kuwa ana madhaifu kama hayo hao anawaeleza watamsaidia nini zaidi zaidi anamueleleza mmewe na kujichoresha .Wanawake wa sasa staha na heshima hakuna kabisa yaani hajui jinsi watu wanavyomuona mpumbavu.

Wapo wengi sana siku hizi
 
Huyo mwanamke hana akili jamani.Yani mapungufu ya mumewe kwanini wasivumiliane na watafute solution?Mbaya zaidi mashost nao sio mashost maana wamwishaanza kumsaliti.Ndio maana mie sipendi ushost kabisaa na sitaki mashost maishani mwangu
 
Ndo mjue sasa mambo mnayoyafanya wenyewe, umemdhalilisha hujui kama mko mwili mmoja maana yake hata wewe uko uchi mbele ya jamii so sad wanawake hawa!
 
Kama haya ndiyo yanayofanyika saloon.......mke wangu nitakuwa namsuka mwenyewe geto......
 
Hii stori inachekesha kweli. Kwani huyo kidume ameshindwa nini kuji-evaluate perfomance yake kisha atazame kama anachoambiwa kuwa kimesemwa na mkewe kuhusu yeye kina uhalisia?
 
Nimeamini jf inawaharibu sana,hivi na wewe kweli unaamini stor kama hii yani ni porojo tu hamna kitu hapa.

Nimehisi hivyo pia, ila nimechangia makusudi maana juzi nilikuta kitim tim saluni moja, wanawake wanachambana, siri zinamwagika, umbea kama kazi. Tulibaki kutazama tu. Yes! Ni story, lakini haya mambo yapo.
^^
 
Wanawake kama hawa hua hawana kazi yakufanya ni ma goal kipa,na huvamia mji anaweza kua ametoka kwao na maadili mazuri tuu ili na yeye aonekane yumo kundini anaanza kujilaanisha,huyo mumewe wala asinge mpiga vibao angemuliza
ivi unajua mapungufu yako kwenye 6 kwa 6? anaupata wapi huo mda wakuisafisha K yake akiwa yuko na mashoga? au kwanini asutulie kwake anarandishwa na nini kama si umbea nakutaka kujitia kundini? wala kumsema mumewe haijawa dawa yakutokuibiwa,ajifunze maleze ya kumlea mumewe kwanza asione mwengine anaefanananae,angekua mmbunifu mume hata angekwenda kwa changu kwa malezi na heshima unayompa atarudi tuu kwako ajiulize kule alifata nini... atabaki hivyo hivyo asujijua huyo........
 
huyo angekua muandishi wa habari au daktari kashamwagiwa tindikali siku nying, na huenda hatupo nae tena
 
Huyo mwanamke lazima atakuwa anaishi uswahilini tena hana shughuli ya kufanya zaidi ya kukaa vijiweni na kupiga stories.
 
Hii imekaa kihadithi, hadithi, ila ujumbe umefika, cku zote wanaume hujitahidi kutafuta njia ya kuondoa madhaifu ya wake/wapenzi wao ila baadhi ya wanawake hutafuta kujua na kutumia madhaifu ya waume/wapenzi wao ktk namna ya kujipatia maslahi binafsi.
 
Ndiyo mjue nyie wanawake ni zaidi ya Delila.. Tutaishi nanyi maana ni mtihani tumepewa.

Pole kama imekugusa, hata mimi nilijisikia vibaya sana lakini pia sio wanawake wote wako hivi
 
Ndo hivyo mkuu mtu anakujali na kukupa mahitaji yako yote unamlipa hayo kweli

QUOTE=Gemmy;11344627]Huyo mwanamke ana matatizo sijui niseme ya akili
Maana unapomtangaza mwanamme wako kuwa ana madhaifu kama hayo hao anawaeleza watamsaidia nini zaidi zaidi anamueleleza mmewe na kujichoresha .Wanawake wa sasa staha na heshima hakuna kabisa yaani hajui jinsi watu wanavyomuona mpumbavu.
Wapo wengi sana siku hizi[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom