Mimi ni mtumishi wa umma wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nina kesi ya jinai inayonikabili tangu mwaka 2007, ambapo ushahidi wake ulifungwa tangu tarehe 12.06.2011, na kinachosubiriwa ni kutolewa 'ruling' kuwa nina kesi ya kujibu au la, lakini hadi leo October 27, 2011 mahakama haijatoa uamuzi huo. Je katika hatua hii nitumie mbinu gani ili niweze kupata haki yangu mapema kwa sababu hata kesi yenyewe nilibambikiziwa na mbunge wangu. Naombeni msaada wa kisheria wa jinsi ya kuilazimisha mahakama itoe 'ruling' ya kesi hii. Nilisimamishwa kazi tangu waka 2007 hadi leo ninakula nusu mshahara na familia inateseka sana jameni kutokana na kesi jinai .