Kuchangia harusi au maendeleo?

Kuchangia harusi au maendeleo?

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
Noma.jpg
Nichague lipi?
 
Wa TZ wanaenzi sana Harusi na kifo jamani, hili la elim labda tuanze sasa
 
Mara nyingi watu wanataka kukubalika kupitia harusi ila elimuu hhhhhhh kila mtu alizaa mwenyewe

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Kwa wakereketwa wajanja ka mimi tulishaling'amua hili na sasa niko very selective kwenye michango ya harusi, kwani haileti maana sana kuchanga mamilioni ya mahela yote yaliwe siku moja na mbaya zaidi NDOA zenyewe zinakuwa si za uhakika kadri siku zinavyokwenda, kuna jamaa mwaka jana alifunga ndoa kwa receiption ya kishindo lakini huwezi amini kilinuka na walitengena siku iliyofuata wakiwa honey moon. Tusomeshe watoto wa Taifa letu jamani.
 
Yani hili la harusi loo
nampango wa kusitisha kuchangia maana kila mwisho wa mwezi kwa mshahara wangu kuna fungu la kuchangia harusi au sendoff au kitchen party
 
wa tz hawana utamaduni wa kusupport elimu, sema mambo ya cherekochereko hapo unamjua m tz ni nani.
 
Siku hizi Harus zimekuwa sehemu,ya kujuana,kufahamiana,kupunguza ma stress,kupunguza ma pressure n.k.Ndo maana watu wanashadadia ma cherekochereko.Bt shule kwa wengi hawana hata chembe ya mwamko hii ni kutokana na baadhi ya wanaf.wakishajua anachangiwa ndo bidii ni F.hazimuumi as if zinaokotwa.Nina mf.wa wanaf.wanalipiwa na SHDEPHA yaani hata uniform huwa wanalazishwa kwenda kuchukua kwenye ofis zao,darasani ni tabulalasa.C bora nizigonge hata Serengeti ya Bariiiiidii.
 
Wanandoa wenyewe walishaoana siku nyiiiingi sana tunachangia divorce.
 
Ukitaka kuoa, tafuta hela, pika chakula watu wale, huna hela kafunge ndoa yako kimya kimya rudi nyumbani pumzika na ubavu wako. TUSICHOSHANE.
 
Tatizo watu wengi hawachangii elimu kutokana na -ve attitude.mwingine watoto wake wote wamefeli na mipesa anayo so we kajaribu kuomba mchango hapo kuhusu kusoma utasikia jibu lake.mwingine ni wivu tu kwamba "aah nimlipie ada akipata kaz aje anidharau" mwingine "kwani atanisaidia mimi si atawasaidia ndugu zake"tukiacha haya nafikiri tutachangia elimu
 
Mtun akichangia Harusi ana uhakika atakula na kunywa, lakini akimchangia mtu masomo, mtu aliyechangiwa atakuwa kama Mwizi na fisadi wa mali ya waliomchangia kwa faida ya familia yake! Bora tuendelee kuchangia watu kuoana!
 
Wabongo mtu akiwa anaumwa anaomba msaada wanamchunia akifa wanatoa mchango wa msiba hapo hua sielewi
 
Wa TZ wanaenzi sana Harusi na kifo jamani, hili la elim labda tuanze sasa

Kubadilika inawezekana pia. Mimi nimeshachangia watu wawili ambao wanataka kupata ada ya kujiunga na chuo baada ya kukosa mkopo lakini wamepata nafasi na wanafanya vizuri sana darasani.Ndio tunaanza hivyo kubadilika though it will take time.
 
Wale mnaotaka harusi hamna hela jamani si muwe mnafunga kwenye misa za usiku mf chrismas pasaka mwakampya au jubilei saa sita mnarudi zenu home mnaliangusha kesho yake mnapiga boto kifamilia imetoka heee nnini kuumiza kichwa!
 
Waafrika tuna shida kubwa sana. Tunapenda sana starehe. Tunapenda sana sherehe kama sehemu ya starehe na watu wako tayari kuchangia pesa kiasi chochote kwa ajili ya starehe lakini si kwa ajili ya maendeleo.....HILI NI TATIZO KUBWA SANA LITAKALOCHUKUA MIAKA MINGI SANA KUMALIZIKA.
Wakati wenzetu wazungu utuchangia pesa nyingi kwa ajili ya maendeleo yetu sie huwa watu wanafikiria sherehe na wako tayari hata kuomba msaada nje kwa ajili ya kuendeshea sherehe.
Wewe angalia bajeti yetu kwa mfano, utacheka sana jinsi enterteinment ilivyopangiwa pesa nyingi kuliko madawa yatakayonunuliwa kwa ajili ya zahanati au angalia bajeti ya chai jinsi ilivyo kubwa kuliko pesa wanayopewa wanafunzi 1000 wa chuo kikuu kama mkopo!
NADHANI TULILOGWA
 
Tuchangie kusoma, are you serious? Tanzania tungekuwa tumesoma na kuelewa kitu uhuru wa mwananchi na sheria tusingeruhusu Kikwete aendelee kuwa rais ama hata mawaziri wake wezi. We need a revolution, petition iko wapi jamani jeshi letu?
 
Back
Top Bottom