Kuchangamkia fursa: WaTZ tuna matatizo!. Pongezi Rais Magufuli kuwa M/Kiti SADC, usiposaidia WaTZ kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tu!.

Wanabodi,
Baada ya mkutano wa SADC, wageni wameondoka, sasa turejee kwenye maisha yetu ya kawaida ikiwemo kuendelea kuelezana ukweli sometimes ukweli mchungu kupitia hizi makala zangu za “Kwa Maslahi ya Taifa”. Makala ya leo kwanza ni kutoa pongezi kwa rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, naamini kwa uwezo wake, kama ali transform Tanzania kwa muda mfupi, kutoka nchi ya shamba la bibi, hadi kuwa nchi ya heshima na kupigiwa mfano, hivyo ndivyo atakavyo I transform SADC kuziwezesha nchi za SADC kuchangamkia fursa za SADC kwa nchi wanachama.

Hili ni bandiko la kuuleza ukweli mchungu kuwa katika suala zima la kuchangamkia fursa za kiuchumi na kibiashara, sisi Watanzania tunamatatizo!. Hivyo natoa pongezi zangu kwa rais Magufuli kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti SADC, na kutoa wito kwake, kufuatia Watanzania kuwa ni watu wenye matatizo katika kuchangamkia fursa za kiuchumi, asipo wasaidia Watanzania kuchangamkia fursa, tutaishia kuwa watazamaji tuu wa fursa za kiuchumi kama ilivyo sasa kwenye fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Japo mimi sii mchumi, na wala sijui Watanzania tunamatatizo gani katika kuchangamkia fursa mbalimbali hali inayotufanya tubaki nyuma nyuma, lakini kwa vile nimeona tuna matatizo, jukumu langu kama mwana habari, linaishia katika kutoa taarifa tuu kuwa kwenye kuchangamkia fursa, Watanzania tuna matatizo, na Watanzania tukiwa na matatizo, inamaana Tanzania tuna tatizo. Hakuna kitu kizuri kama mtu kukubali udhaifu wako au matatizo yako, ukiisha kubali unamatatizo, huku kujikubali ndio hatua ya kwanza ya kukabiliana na matatizo yako, na mwishowe kuyapatia ufumbuzi wa kudumu. Katika hoja ya kuchangamkia fursa, lazima tujikubali kuwa sisi Watanzania, tuna matatizo, hivyo namuomba rais Magufuli katika uenyekiti wake wa SADC, aanze na charity which begins at home, kwa kuisaidia Tanzania na kuwasaidia Watanzania kuchangamkia fursa za SADC kisha azisaidie nchi nyingine zote za SADC kuchangamkia fursa za SADC bila kusahau fursa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimesema kwenye kuchangamkia fursa, sisi Watanzania tuna matatizo, kwa sababu Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa fursa nyingi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini kama tumeshindwa kuzichangamkia fursa hizi kikamilifu kwa soko la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambalo liko next door, what are the chances kuchangamkia fursa za soko la SADC ambali liko mbali?, bila Watanzania kusaidiwa na serikali yetu kwa uhamasishaji kama uliofanyika kwenye kuuhamasisha huu mkutano wa SADC, na kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania kuchangamkia soko la SADC, tutaendelea kuwa watazamaji kwenye regional trade, kama hali ilivyo sasa kwa mizigo mingi ikipitia bandari Dar es Salaam, halafu Watanzania tunaifuata huku inakokwenda kama Uganda.

Tanzania inaongoza kwa fursa za SADC na EAC kwa sababu tumepaka na nchi 8, katika ya hizi nchi nane, nchi 6 ni land locked countries, nchi nne ni za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, na nchi 4 ni za SADC, DRC, Msumbiji, Zambia na Malawi. Nchi zote hizo, zinaagiza bidhaa mbalimbali ambazo tunazo, lakini wanaagiza kutoka nchi za mbali, na kuzipitishia bandari zetu, barabara zetu, reli yetu na kuzipelekwa kwao, wakati sisi tungeweza kuchangamkia fursa hizo.

Ninaposema Watanzania tuna matatizo, kimataifa ni nchi ya Tanzania ndio tuna matatizo, kama watu wako wana matatizo, then nchi yako ina matatizo. Mfano kuna kulio kikubwa cha uharibifu wa mazingira kutokana na kukata miti ya kuni kwa nishati ya kupikia, na kuchoma mkaa, wakati tayari tumeishagundua gesi asili. Hata kabla ya ugunduzi wa gesi asili, Tanzania tuna viwanda vya kujaza gesi ya kupikia ya LPG kwenye mitungi na kutumia majumbani, huwezi amini nikiwaambia nendeni pale kwenye mpaka wa Namanga, mshuhudie malori ya gesi ya kupikia kutoka Tanzania, yanavyopeleka gesi Kenya. Hii maana yake mahitaji ya gesi Kenya ni makubwa kuliko uwezo wa Kenya kujitegemea, hivyo wananunua gesi nyingi kutoka Tanzania, huku sisi Watanzania wenyewe tukipikia kuni na mkaa!.

Hii inamaanisha wenzetu Wakenya wamehamasika zaidi kutumia gesi kuliko sisi, huku sisi tukiendelea kutumia kuni na mkaa na kuharibu mazingira yetu, wakati serikali yetu ikiimba nyimbo za utunzaji mazingira, utunzaji vyanzo vya maji kama utunzani misitu na upandani miti bila kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia. Moja ya sababu zinazowafanya Watanzania wa hali ya chini kushindwa kutumia gesi ni bei ya gesi na majiko ya gesi na mitungi ya gesi zenye vat, kama tungetoa msamaha wa kodi kwenye gesi ya kupikia na vifaa vya gesi, tungepata hasara ya kupungukiwa mapato lakini tungeokoa sana mazingira, hivyo ikifanyika a comparative analysis ya hasara ya kuondoa kodi kwenye gesi, na faida za kimazingira, ungekuta taifa linafaidika zaidi kuliko kuathirika.

Sasa tumegundua gesi asili na tunajenga mtambo wa kuchakata gesi, LNG pale Madimba, unaweza kukuta LNG yote inasafirishwa kupelekwa nje kwenda kutumiwa na wazungu wenye pesa, halafu sisi masikini wa Tanzania tukiendelea kutumia kuni na mkaa!. Hata mafuta ya Uganda yatakapitia bomba la mafuta pale Chongoleani Tanga, tangu kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta la Uganda, Watanzania tungekuwa makini katika kuchangamkia fursa, ungekuta saa hizi tayari tunatengeneza refinery yetu ya mafuta kusubiria mafuta ya Uganda, ili tununue crude oil kutoka Uganda, tusafishe tutumie na ikibidi kuuza nje, tuachane na bulk procurement kununua mafuta nchi za nje, lakini amini usiamini, tunaweza kushuhudia mafuta ya Uganda yakipitia kwetu huku sisi tukiendelea kuagiza mafuta nje ya nchi.

Ukiangalia mahitaji ya soko la SADC na la EAC, utashuhudia bidhaa nyingi zinaagizwa nje ya bara la Afrika na sisi kufaidika kama wasafirishaji tuu kupitia bandari, reli na barabara zetu, ndio maana azma ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli kujenga Tanzania ya Viwanda, rais Magufuli ameona mbali, hii ni fursa, lakini ili hii fursa Tanzania ya Viwanda iweze kuleta manufaa ya kweli kwa taifa letu, ni kwa Watanzania kusaidiwa kuzibaini fursa za bidhaa zinazohitajika katika soko la EAC na SADC, tutengeneza viwanda vya bidhaa hizo zitoke Tanzania kama jinsi China ilivyo hub ya viwanda vya components kwa dunia nzima. Kwa vile Tanzania tunategemea kilimo, then Tanzania ya kweli ya viwanda ni Tanzania ya agro processing industries, kuwekeza kwenye kilimo kama ulivyo mradi wa ASDP II, ndio ulipaswa kuwa priority no. 1.

Mh Rais wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli akihutubia mkutano wa n SADC baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti amezungumzia mambo mbalimbali yakiwepo mambo ya kiuchumi na kusistiza kuwa nchi za SADC bado hazijatumia vizuri rasilimali zilizopo ili kukuza uchumi wa nchi hizo. Amesema kuwa pamoja na nchi hizi kuwa na kila kitu lakini bado uchumi wake umekuwa wa kusua sua na kutolea mfano wa miaka kumi uchumi wa nchi hizi umekuwa unashuka badala ya kukua. Mh Rais Magufuli kuonyesha uzalendo wake na kusimamia kile anachokiamini amewanyoshea vidole secretarieti ya SADC kwa kushindwa kuja na majawabu ya nini kifanyike kukuza GDP ya nchi za SADC.

Amewataja marehemu Baba wa Taifa Mwl Nyerere, Agostino Neto, Mandela, Mzee Mugabe na wanzilishi wengine wa SADC kuwa walikuwa na malengo makubwa, lakini bado ndoto za wazee hawa hazijafanikiwa vizuri, hivyo kama alivyotimiza ndoto ya Mwalimu Nyerere kwa Tanzania kama kuhamia Dodoma na umeme wa Stigler, tunamuomba rais Magufuli aitimize ndoto ya waanzishi wa SADC kiuchumi.

Mh Rais kwa suala la biashara amesema kuwa hakuna sababu nchi wanachama kuagiza bidhaa nje kama bidhaa hizo zinapatikana SADC. Amesema kunatakiwa kufungua milango ili wananchi wa nchi hizi kujua fursa zilizopo katika nchi mwanachama na kutolea mfano ziara yake ya mwezi May nchini Zimbabwe, alishangaa nchi hiyo kuagiza nafaka nje wakati Tanzania kuna ziada ya kutosha ya nafaka. Hivyo kwa soko la SADC na EAC, kuna mahitaji ya bidhaa nyingi ambazo nchi moja inazo na nchi nyingine haina, lakini bidhaa hizo zinaagizwa nje na zinaingia soko la EAC na SADC wakati sisi wenyewe kwa wenyewe tungeweza kuzalisha.

Rais Magufuli ameendelea kushangaa nchi za Afrika licha kuwa na rasilimali nyingi lakini bado Afrika ni masikini na inalalamika hali duni ya kiuchumi, amesema nchi za kiafrika si maasikini hivyo ziache kujitangaza kuwa ni duni mbele ya mataifa mengine.“Tusikubali kusafirisha tu malighafi nje ya Afrika, hii inaatufanya tuwe tunasafirisha ajira. Nchi zetu si masikini, narudia tena nchi zetu si masikini tunao utajiri wa kutosha kwenye madini, mafuta na ardhi yenye rutuba. Vitu vyote vinavyotufanya tuwe matajiri tunavyo, kwanini tushindwe kupiga hatua,” alisema Rais Magufuli, hivyo sasa tunamuomba rais Magufuli baada ya kulitambua hili, autumie uenyekiti wake kuibadili hali hii.

Rais Magufuli ametolea mfano tunaagiza sukari, vyakula, mafuta katika nchi za mbali wakati baadhi ya mataifa ya SADC yanazo bidhaa hizo tena zinapatikana kwa bei nafuu, na kuahidi mwaka wake wa uongozi ameamua kuongozwa na kaulimbiu ya mazingira bora ya viwanda, ufanyaji biashara na kutengeneza ajira..

“Bado hatujafanikiwa katika ukuaji wa uchumi, niseme kweli bado tunasuasua. Na tusipobadilika hatutaweza kufanikiwa katu. Bado tupo nyuma katika lengo letu la kiuchumi, uhaba wa taarifa unasababisha tunashindwa kujua wapi pa kuuza bidhaa zetu,” alisema Rais Magufuli.

Tumtakie kila la kheri rais Magufuli katika kuijenga SADC mpya kama anavyoijenga Tanzania mpya.

Viva Magufuli,

Viva Tanzania,

Aluta Continua.

Paskali
Mkuu bandiko lako lipo vizuri lina ukweli ila tatizo ni kuwa waTanzania tumejaliwa kuwa na hoja zinazoshawishi(silver tongue) lakini katika upande wa utekelezaji tunafeli mfano wafanyakazi wa maliasili wenye jukumu la kulinda na kutuelimisha sisi wananchi juu ya madhara ya kutumia kuni na mkaa ndo hao watumiaji wazuri wa hiyo mikaa wanayoipata bure kutoka kwa wananchi wanapofanya doria. Mifano ipo mingi Je sisi wananchi wa kawaida tutawezaje kufuata utaratibu wakati wanaosimamia huo utaratibu awapo tayari kufuata.?
 
Back
Top Bottom