Habari kwenu!
Wanawake wengi enzi za uchumba hujituma sana na kuonyesha kwamba kweli ni wanawake wanaofaa ktk ndoa lakini wanapoolewa tu hubadilika kama ifuatavyo:
1. Alikuwa msafi sana lakini akiolewa uchafu unaanza.Kosa kubwa sana
2. Alikuwa anajituma ktk upishi mara tu baada ya kuolewa basi anaanza kumuachia house maid afanye kila kitu, mwisho wa siku mwabwana wasio na uvumilivu wanamfanya na house maid kuwa mke wa pili.
3. Kujituma ktk tendo la ndoa kunapungua.Kosa kubwa sana maana ndoa bila tendo la ndoa hakuna ndoa.Uchafu, uvivu, kukosa ubunifu kunasababisha ndoa kutetereka.Usishangae kabla ya ndoa wote mlikuwa mnafika lakini baada ya kuoa usishangae akakuambia baby kojoa basi nikalale, Au bado hujakojoa tu?Tena kama amezaa ndiyo usiseme. Vitu kama hivi ni kosa kubwa sana.
4. Kiburi kwa kudhania kwamba kufunga ndoa ndio wamemaliza kila kitu huku wakisahau kwamba penzi linahitaji kupaliliwa kila siku.
Onyo kwa dada zangu wa kikristo:Ndoa ya mke mmoja isiwe kigezo cha nyinyi kubweteka pia muelewe kwamba shetani yuko kazini kila saa na wanawake warembo wanazaliwa kila siku.Ukizubaa utaletewa virusi ndani mwako bila kujua.
Katika mchakato wa kuelimishana nyote mnakaribishwa kuchangia.
si kweli nafikiri swala la nyumba ndogo limetokana sana na kushindwa kujidhibiti kwa wanaume na pia kuweka tamaa za kimwili mbele kuliko kitu kingine chochote na pia kukosa hofu ya Mungu kabisa,kwani swala la mwanamke kujibweteka ni swala ambalo mume anaweza kumweleza mke wake wapi anapwaya na wapi afanye marekebisho na kama mke ni mwelewa mambo huenda mswano.
suala la wanaume nao wakiingia kwenye ndoa kutomjali mke..kumuona mke kashafungwa kifungo hawezi kutoka kutompa nafasi ya kumsikiliza .kumnyima haki yake ya ndoa mf wakati wa uchumba unajituma mno uonekane ngangari lkn ukioa ni wa kubeep tu namengine kibao nayo mjue husababisha ndoa kuharibika! Si mwanamke tu hata mwanaume aweza leta adhari ktk ndoa.
Ni ukweli mkuu muhimu kila mmoja ajitahidi kufanya ndoa inakuwa mpya kila siku.."...ni mpya kila siku asubuhi uamifu wako ni mkuu"
Wkt mwingine YES, Wkt mwingine NOO...Wanaume nao wamezidi...Kuna baadhi ya wanaume bila nyumba ndogo hawezi....Anaona km anapewa maharage kila siku...anataka kubadilisha mboga
Mada yako ingeweza kuwa sawa kama ungesema "ni moja ya sababu za nyumba ndogo" lakini sio kusema "ndio chanzo kikubwa" kwasababu kuna ndoa zingine mwanamke ndio muwajibikaji kuanzia kwenye kutafuta hela hadi kitandani wakati li jamaa lenyewe lipo tu
Hebu jaribu kutenda haki bana!
me nashangaaga hii makitu, mkeo mvivu ukimuoa, mkeo mchafu ukimuoa, wenzio wanammendea wanatamani usafiri,