Kubweteka kwa wanawake mara baada ya ndoa ndiyo chanzo kikubwa cha nyumba ndogo

Narudia tena na tena, mwanandoa yeyote hana sababu yoyote ya msingi au halali ya kuwa na mpango wa kando eti sababu ya madhaifu ya mwenza!
Kama mke mchafu, mvivu, kiburi basi mume naye aweza kuwa mvivu, mkorofi, hawajibiki kitandani, naniliu ndogo, hamudu kutunza mke na watoto, mbabe etc etc!
So tukitumia mapungufu kama justification ya kuchepuka hakuna wa kusalimika!
TUVUMILIANE, TUELEKEZANE NA TUHESHIMIANE.
OOtherwise mtoa mada naunga mkono hoja! wanandoa wote tupalilie ndoa zetu! Msiwaachie wanawake peke yao!
 
ni kweli inabidi wajitahidi(sustainable maintanance ya characters) ili kuupeka uke mwenza na numba ndogo kama hawa hapa chini

10304705_287486394744387_4926143711381215330_n.jpg

huu mpambano refa yuko wapi?
 
Mada yako ingeweza kuwa sawa kama ungesema "ni moja ya sababu za nyumba ndogo" lakini sio kusema "ndio chanzo kikubwa" kwasababu kuna ndoa zingine mwanamke ndio muwajibikaji kuanzia kwenye kutafuta hela hadi kitandani wakati li jamaa lenyewe lipo tu

Hebu jaribu kutenda haki bana!

kweli, kweli kabisa, kweli tupu
 
Hata baadhi ya Wanaume pia wanazembea wakishaingia kwenye ndoa, kwenye uBF na uGF kila weekend lazima wakajirushe na mrembo sehemu kali kali, kwenda lunch na dinner pamoja mara nyingi tu kwa week. Kila mara anakumbuka mrembo kwa simu, text messages na zawadi mbali mbali. Ngoja amuweke ndani kama mkewe zile outings za mara nyingi kwa week zinakata, mara nyingi anapendelea kuwa na marafiki badala ya kuwa na mrembo. Hukawii kusikia mrembo akilalama kabla ya ndoa alikuwa akinijali sana sasa hivi walaa sijui ndio uzuri wangu umepungua au mapenzi ndiyo yamechujuka.


 
Last edited by a moderator:
Chanzo kikubwa cha michepuko na kuvunjika ndoa ni shetani. How?
Unapofunga ndoa takatifu ni muunganiko wa three persons. Ambazo ni mke, mume na Roho wa Mungu. Mkitunza uwepo wa Mungu ktk maisha yenu, kwa kupendana, kuheshimiana, kushirikiana, kujaliana, kuombeana you will be safe.

Msipotunza hivyo basi mnamtimua Roho wa Mungu na nafasi lazima ijazwe so Shetani anaingia. Akiingia ndio upendo wa awali hupotea, chuki, hofu, wivu, uvivu, kuviziana, kutoaminiana, na mengine mengi ya hivyo hutamalaki.

Hiyo ndio root cause ya matatizo ya ndoa, ndio maana yaitwa Takatifu, so maintain huo utakatifu itaendelea kudumu.
 
Back
Top Bottom